Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakasema anakuja mou hapo kwako tukamsubiri na kumpiga wakasema tumebahatisha sababu uwanja wetu wakasema nenda kwa mwarabu tukaenda na kumpiga wakasema ooh sababu ni mji mmoja hakuna ugenini wala nini binadamu akikuchukia kila baya atakuzushia ni sauti ya mlevi mmoja ilisikika
 
Wanaosema kwamba kwa kuwa ni timu za mji mmoja basi hakuna tofauti kati ya mechi ya ugenini na nyumbani hawajielewi

Kama huamini angalia stats za United na City (kila mmoja akiwa nyumbani nani ameshinda sana, na wapi?)

Angalia Arsenal na Tot, au Chelsea au Westsham

Pamoja na mambo ya hali ya hewa kuwa ile ile na timu kutokuwa na uchovu wa kusafiri, lakini idadi ya mashabiki uwanjani inaweza kusaidia timu kuwa na nguvu uwanjani au iwe wanyonge. Hapa kuna watu watasema kama ni mji mmoja hata timu pinzani wanaweza kujaza Uwanja, NO, HAIWEZEKANI. Timu mwenyeji ndio inaamua idadi ngapi ya tickets iende kwa wapinzani na ngapi iende kwa mashabiki wao. Kuna % flani imewekwa na mamlaka msimamizi ili timu pinzani isije kukosa ticket hata moja.
 


a) mechi 11 tumepata point 11.
a1) mechi 5 tumepata point 13

b) mechi 5 tumefunga magoli 10 na tumeruhusu magoli 3
b1) mechi 11 tumefunga magoli 15 na tumeruhusu magoli 16

mechi 3 za mwisho (aston villa, sheffield united na brighton) tumefunga magoli 8 kati ya hayo 15 tuliofunga dhidi ya timu ndogo na wakati huo huo tumeruhusu magoli 6.

kufunga magoli 8 ndani ya mechi 3 si mbaya sana na ni dalili moja wapo inayodhirisha kuimarika kwa safu yetu ya ushambuliaji kwa hizi mechi za karibuni lakini kuruhusu magoli 5 ndani ya mechi 2 si dalili njema kwa safu yetu ya ulinzi.

huyu kirusi wetu (kwa mujibu wa brother fuentte na Darmian ) atarudi lini?
huenda ukawa ndio usajili wetu mpya pale mbele.
ndiye mwanadamu atakayeusambaratisha mjadala unaowahusu jesse lingard na andreas perreira.

mara paaap pogba anarudi uwanjani lakini bwana ole anamrudisha namba 8 kama ilivyokuwa mechi za mwanzoni.
ndipo nitakapoamini hata wazungu wana roho mbaya
 
Unadhani kwa wachezaji hawa hawa man utd ingekuwa na Brendan Rogers kama Coach je,ingekuwa kama Leicester city?.
 
Ole hana tabia ya kukandia au kutumia lugha yenye ambiguity kwa wachezaji wake, napenda anavyo wakumbatia wachezaji wake kila baada ya game.

Angalia anavyomzungumzia pogba..inawezekana akamuuza bila hata kumtupia neno ovu. Hakumpenda fellain na Sanchez na lukalu sio kwa sabb hawajui,lkn kwa sabb ya ufaza, kama mafaza vile. Ole hamfanyii mtu kazi, anafanya kile anachikiamini

Ni muongeaji sio mlalamikaji. Ole hana stress hicho kinamfanya asipanic hovyo. Kingine ole hana komedy hata kidogo. Utani ule wa kawaidaaa sana. Ni kama Ferguson.
By so doing hata wachezaji wake hawana na hataki upuuz wa mazoea mabaya, pogba anapenda upuuuzi, anachezacheza lkn angekuwa na sura ya ole angekuwa mtu bora duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…