Jana tulishinda vizuri sana, Yule kijana wa KiKorea alinifurahisha sana baada ya kuweka bichwa wavuni, yaani ukitaka kuwabagua vijana hawa ili umsifu mmoja kuliko mwengine, hilo naona kama haliwezekani kwa Man U. Vijana wote wanasakata kabumbu maridadi sana, Owen alinifurahisha sana baada ya kuniinua katika Kochi nililokaa na kuwacha kahawa yangu ipowe kutokana na furaha ya kusherehekea bao hilo, bao lilikuwa maridadi sana, Yaani hawa Man U, wananistaajabisha kwa utaalamu wao. Yaani Ferguson akiamua kumuweka mtu Bench, wale wanaocheza huwa wazuri zaidi, jamaa hii ni hatari kwa Arsenal na Chelsea.Na yule reserve wetu mstaarabu, Mr Fluke dude O'shea huwa ananifurahisha sana anapoingia uwanjani, huwa mara nyingi zaidi huja na matunda maridadi sana.
Real Madrid wanataka kutufujia timu yetu kwa kumchukuwa Ronaldo, I was very dissapointed with that speculation. Wametangaza dau kubwa la mshahara Euro millioni kumi 10 kwa mwaka, hii itamfanya mchezaji wetu aanze kubabaika na dau hilo.