Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu nafikiri team ya Ferguson pamoja na uimara wake bado sajili nyingi nilikuwa tia maji tia maji.

Nimesema mwanzo kuwa kipindi cha 2000- 20008 ushindani epl haukuwa mkubwa kama sasa kwani kulikuwa na team chache sana ambazo ni title contender leo hii unazungumzia timu nyingi zimewekeza sana na pressure ya ligi imeongezeka.

Ferguson kwenye dressing room yake aliweza kumaintain strong personality za class of 92 na wachezaji wengine kama kina Ferdinand na Nemanja Vidic, Wayne Rooney etc.

Lakini hebu jaribu kuanzia 2008 upwards mchezaji gani pale Man united aliyesajiliwa akaja kuwa top level player ? Wengi walikuwa back up players ukiondoa Van Persie na Berbatov.

Kuanzia kipindi hicho ushindani wa ligi ulimpush Ferguson kuanza kusajili complete players lakini wengi walidumu kwenye team kwa muda mfupi tu.

Hebu jaribu kuangalia incidence za usajili wa Eden Hazard, Lucas Moura, Luca Modric na Wesley Sneider ulivyokuwa handled pale Man united.

Yawezekana kweli man united iliendelea kufanya vizuri sokoni kwa Ushawishi wa club na Kocha aliekuwepo kipindi hicho. Hauoni Kenyon alivyoibadili Chelsea ndani ya msimu mmoja tu ?
 
Mkuu usisahau Arsenal Invicible na chelsea ya Mou, kipindi hiki hakukuwa na Top 6 lakini ligi ya uingereza ilikuwa vizuri sana na ndio jina la top 4 lilipoanzia. Kwa miaka mfululizo kuanzia 2005 hadi 2008 timu ya uingereza ulikuwa huikosi fainali champions league.

Man u tulipoteana sana, kuna wakati tulikuwa tunatoka makundi uefa, mabango ya Fergie out yakaanza Old trafford, ndio ikaja hio rebuild ya Queiroz ya kina ronaldo, Rooney, Tevez etc na kama nilivyosema comment ya nyuma hicho kikosi cha man U 2007 kwa ligi ya sasa kina uwezo wa kubeba kombe kirahisi tu.

Na build yetu sisi haikuchukua tu Ligi ya uingereza bali tukawa powerhouse Uefa pia ndani ya miaka 4 tukaingia fainali 3, hivyo mafanikio tuliyoyapata kenyon alivyoondoka ni makubwa kuliko alichofanya kenyon man utd na chelsea.
 
Ilo jini kenyon nasikia lilikua na mpango wa kuinunua newcastle sijui umeishia wapi?????
 
Hazard alitamka kwamba timu itakayobeba uefa ndo ataenda ..ikatokea wanaume tukawa mabingwa basi ndo mchiz akatimba ndan ya Stamford Bridge... Daraja takatifu..

Kila la kheri Chelsea
 
Ferdinand naye kaanza kupiga U-turn sio??
 
Ila mkuu valencia sio Boko, jamaa alikuwa na chenga moja ila kwa msimu anakupa assist za kutosha. Msimu wa 2011/12 jamaa alikuwa na assist 13, kuna mafundi kibao Epl hizo assist wanazisikia tu.
Valencia na Young wamekuja kuwa boko baada ya Ferguson kuondoka, ila alipokuwepo walikuwa ni wachezaji muhimu sana na kama valencia amechangia kwa kiasi fulani kwenye makombe mawili ya mwisho amabapo alitoa assist nyingi sana
 
Mkuu hivi aliyemsajili Eric Djemba Djemba alikuwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…