Big Sam: Manchester United wasipojitazama wanashuka daraja
Staa wa zamani wa Man United, Lee Sharpe anaamini Harry Kane atakwenda kuwa suluhisho la matatizo ya Man United, hivyo wakamsajili tu bila ya kujali kwamba atawagharimu karibu Pauni 300 milioni huko.
. UNAMJUA Sam Allardyce? Yule kocha mwili jumba, Waingereza wenzake wanamwita Big Sam, hakutaka kuwaficha Manchester United na kuwaeleza ukweli, watashika daraja kama hawatafanya haraka kusajili mshambuliaji wa kuja kuwafungia mabao.
Man United wapo pointi mbili tu juu ya kuangukia kwenye shimo la kushuka daraja baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa kwa Newcastle United.
Wababe hao wa Old Trafford wamefunga mabao tisa tu msimu huu, manne waliyapata kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Chelsea, lakini sasa straika aliyeaminiwa, Marcus Rashford amekuwa hovyo, hajui hata goli lilipo.
Big Sam, ambaye amepata umaarufu kwamba wa mtu anayefuatwa kuokoa jahazi timu inapokuwa kwenye hali ya kushuka daraja, anasema kwamba kocha Ole Gunnar Solskjaer anatakiwa kutafuta suluhisho la haraka, la sivyo mambo yatamchachia.
"Hili jambo halipo nje ya uwanja wake na kwamba wapo kwenye hali hiyo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi wengi. Wachezaji wanaonekana kushindwa kuwa fiti kwa wakati na hilo ndio tatizo," alisema Big Sam na kuongeza.
"Kuna usumbufu pia wa huyu (Paul) Pogba kutaka kuondoka. Nadhani hakuchagua njia nzuri ya kuliwasilisha hilo na si kusema, nataka kuondoka. Shida yao kubwa Man United haipati mabao, wakimaliza hilo, wamemaliza kazi."
Staa wa zamani wa Man United, Lee Sharpe anaamini Harry Kane atakwenda kuwa suluhisho la matatizo ya Man United, hivyo wakamsajili tu bila ya kujali kwamba atawagharimu karibu Pauni 300 milioni huko.