Manchester United (Red Devils) | Special Thread

AMECHOKA

KUMBE hata Ole Gunnar Solskjaer anachoshwa na kikosi chake cha Manchester United. Kocha huyo raia wa Norway amekiri kuangushwa na safu yake ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Marcus Rashford.


Solskjaer alidai kuwa wakati mwingine eneo la ushambuliaji limekuwa likishindwa kutimiza majukumu yake ya kufunga mabao licha ya nafasi nyingi kutengenezwa.


Hata hivyo, alisema kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikashusha straika mwingine mpya ili kuwaongezea nguvu akina Rashford, Anthony Martial na kinda Mason Greenwood.


Mapema msimu huu, mabingwa hao wa zamani wa England walimuuza straika wao Romelu Lukaku kwenda Inter Milan kwa kitita cha pauni milioni 73, pia, walimtoa kwa mkopo Alexis Sanchez kwa wababe hao wa Italia.


Solskjaer hakusajili mchezaji yeyote katika safu ya ushambuliaji zaidi ya kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi na kiungo kwa kunasa saini za Harry Maguire, Aaron Wan-Bissaka na Daniel James.


Tetesi za usajili barani Ulaya zinaihusisha timu hiyo na kutaka kusajili straika mmoja kati ya Mario Mandzukic wa Juventus na Callum Wilson wa Bournemouth.


“Ni kweli, tuliwaruhusu Sanchez na Lukaku kuondoka, wala hauhitaji mtaalamu wa sayansi kujua kama tutafanya usajili katika eneo la ushambuliaji, tutajaribu kufanya hivyo.


“Ulikuwa muda wa Lukaku kuondoka hapa, hata yeye alijua hilo, jambo muhimu ni kuziba nafasi hiyo kwa kusajili mchezaji sahihi ambaye atakuwa hapa kwa muda mrefu.


“Sokoni kuna wachezaji wengi, tunahitaji straika mwenye uwezo, atakayeendana na falsafa za Manchester United, lazima tuzingatie hilo,” alisema.


Kocha huyo aliendelea kuitoa kasoro safu yake ya ushambuliaji kwa kusema wanachangia kwa kiasi kikubwa kuirudisha klabu hiyo nyuma kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya kufunga.


“Unaweza kujionea mwenyewe, eneo pekee ambalo lina shida ni ushambuliaji, safu ya ulinzi tupo vizuri, sisi ni moja ya timu tulizofungwa mabao machache England.


“Hakuna utulivu kwenye ushambuliaji, hakuna anayeweza kufanya maamuzi sahihi, tunahitaji muda kulifanyia kazi hilo, najua tutakaa sawa baadaye,” alidokeza Solskjaer.


Katika michezo saba ya Ligi Kuu England, safu ya ushambuliaji ya Manchester United wamefanikiwa kufunga mabao nane.​
 
Ishu sio kumuuza Lukaku..ishu ni je alimuuza ili awape nafasi Martial na Rashford??..Kwanini hakuingia sokoni kutafuta straika mzuri??..
According to stone (Mwandishi wa habari wa BBC na mtu wa karibu wa Ed Woodward), Ole amemuambia Ed Woodward anahitaji wachezaji 9 Ili Man UTD ikae vizuri, na maneno haYa Ed ameambiwa kabla Dirisha la usajili halijafunguliwa.

Mkuu tuna matatizo makubwa as a club, Structure nzima ipo ovyo, huo usajili si tatizo Sana Kushinda issue ya Majeruhi, Nasikia Dogo Greenwood na yeye ameumia, kila mchezaji akija tu Man United anakuwa injury prone, mpaka AWB Sasa nae amekuwa hivyo hivyo, dalot karudi mechi 1 tayari nae Majeruhi, martial tuliambiwa kaumia kidogo mwezi wa Pili unaisha, pogba, lindelof, lingard, Shaw etc kila unapogusa Ni Majeruhi tu, issue hii IPO toka Fergie aondoke man U 2013 na Mpaka Leo haijatatuliwa.

Nyepesi nyepesi nyengine Ni kwamba Ed anamtoa kwa mkopo Matt judge akapate uzoefu zaidi, timu Kama Man U ndio kichwa chetu hicho tunakitegemea kusajili watu.
 
Kudadeki huyu bwana EDIUJI huyu hata simuelewi
 
Kiungo kiko vizuri kwa hiyo? Maana hajaongelea au ndo mchezaji hatari Lingz Anatosha hahah
 
Kiungo kiko vizuri kwa hiyo? Maana hajaongelea au ndo mchezaji hatari Lingz Anatosha hahah
Nimemshangaa sana,Rashford ndio sio mfungaji na wala sio 9 wakumtegemea ila timu haitengenezi nafasi kabisa, namba 10 hamna.

Nilisema humu sio kwamba tunasema Lukaku na Sanchez hawakutakiwa kuuzwa, unawauza umemleta nani? Unaona hapo Martial majeruhi,Rashford kichwa panzi na Greenwood ndio huyu majeruhi. Analialia nini sasa?😂

Unabaki na Rashford kama #9 wako na Lingard kama kiungo machachari mpika magoli unategemea nini kama sio kushuka daraja?
 
Weka source mkuu otherwise huu ni umbea kama umbea mwingine.
 
Point yangu umeielewaaa..? Spurs kocha wake seven years yupo na team ikafika final UCL. Apewe muda ole
 
Chief kuna kitu kimoja unakosea... klopp imemchukua misimu mitano kujenga Liverpool ndo maana unaona mafanikio yao leo.. so ole aachwe apewe muda ajenge TEAM afumuee kila kitu then tuone matunda... hata kocha wa spurs kuingia final UCL sio jambo dogo.. took them 7 years.
 
apewe muda kama anahesabu yeye alikuwa hajui kama kwenye kuingo atabaki na scot,fred,matic na pogba,hakujua mastriker atabaki na rashford,martial na greenwood ? na amembakiza young kwenye timu wakazi gani ? hajui anachofanya...
Chief ole hana mwaka
 
Kabla ya huo usajili itakuwa kashasepeshwa.
 
mkuu umekifahamu hicho nilichoandika?
njia pekee ya kumfanya ole gunnar solskjaer ajenge hiyo timu yake tunayoitamani itamlazimu ahakikishe klabu inashiriki ligi ya mabingwa.

mwache afanye overhauls inayoambatana na recruitment ya vijana kutoka academy lakini ni lazima mwisho wa msimu aipeleke timu champions league kwa njia yoyote (familia ya glazer hawana shida ya kombe kwa sasa)

kinyume chake klabu haitokuwa tayari kusubiria miaka mitatu bila ya champions league kama walivyofanya liverpool kwa hoja ya kujenga timu, kufanya hivyo kutapelekea klabu ikose mapato kupitia kwa wadhamini wake wakiwemo adidas.

jenga timu yako lakini tunahitaji timu iende champions league ili tupate hela yetu kamili kutoka kwa matajiri
 
Kuna jamaa amefanya analysis perfomance ya Manchester United msimu huu so far

Open Play Struggles
6- Manchester United have only scored six goals from open play this season which ranks them joint-15th.

Set Piece Incompetence
0 – Manchester United have failed to score from a set piece this season other than penalties which ranks them joint-20th.

Set Piece Incompetence II
3 – Manchester United have conceded three goals from set pieces this season other than penalties which ranks them joint-18th.

Area of Shooting
7% – Manchester United have attempted seven percent of total shots in the opposition 6-yard box which ranks them joint-13th.

Area of Shooting II
46% – Manchester United have attempted 46 percent of total shots from outside the opposition box which, in terms of shooting closer to the opposition goal, ranks them joint-18th.

Chance Creation
83 – Manchester United have created 83 chances this season which ranks them 7th.

Ball Security

97 – Manchester United players have been dispossessed a staggering 97 times this season already which ranks them 19th.

Quality of Shooting
0.115 – Manchester United averaged 0.115 xG per shot which ranks them joint-12.

Quality of Finishing
Manchester United are the only ‘Big 6’ team to score less goals than their xG this season.


Quality of Possession
5.80/20.0% – Manchester United rank 7th for total passes per 90 but rank 15th in through ball attempts per 90 (5.80) and 20th in through ball accuracy (20.0%).

Quality of Possession II
1.97 – Manchester United average 1.97 clear goal-scoring sequences per 90 which ranks them 18th.

Quality of Possession III

52.2% – Manchester United average a success rate of just over 50% on long balls which ranks them 18th.


Quality of Possession IV
5.91/29.4% – Manchester United average 5.91 tempo-changing passes per 90 (attempts) which ranks them 9th but their accuracy of 29.4% ranks them 18th.


Quality of Possession V
8.23 – Manchester United average 8.23 passes per 90 within 20 yards of the opponent's box which ranks them 13th. This is despite having the 3rd best possession in the league.

Quality of Possession VI
15.1% – There is only a 15.1% chance Manchester United will shoot in any given possession play they have which ranks them 19th with only newly promoted Sheffield United worse off.


Half Time Team Talk
0-3 – Manchester United have conceded three goals with no reply between 46-60 minutes of games this season which ranks them joint-20th.


Sustaining Leads
1.80 – In the Premier League this season 18 different teams have gone into half time leading. Manchester United average 1.80 points per game when in this situation which ranks them 16th from 18 teams.


Summary:
If one was to scan through this thread they will see general rankings far below any place Manchester United should find themselves in. It is the result of incompetent coaching, inadequate attitude and underwhelming quality.
 
Klopp ana reference huko nyuma,alishaijenga Dortmund huko nyuma akachukua back to back Bundesliga mbele ya Bayern na akaifikisha Dortmund fainali ya Champions league.As a manager OGS amefanya nini so far
 
Chief ole hana mwaka
Yes hana mwaka lakini tangu apewe timu kwenye EPL ameshafundisha mechi 39 ambazo ni sawa na msimu mmoja
Amecheza 39 ,ameshinda 18 draw 9 kafungwa 12 magoli ya kufunga 55 magoli ya kufungwa 42 Winning % ni 46.1%
Champions league kacheza mechi 4 kashinda 1 kafungwa 3,Uropa kacheza mechi 2 kashinda 1 draw 1

Time is not the right answer if wrong man is in charge

I think umeona Lampard anachofanya Chelsea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…