Kocha apewe muda... klopp imemchukua misimu mitano kuwa hapa walipo... kocha wa spurs msimu wake wa saba huu nothing ole aachwe ajenge TEAM.. apewe muda
uongozi wa manchester united kwa kushirikiana na mashabiki wengi wetu kwa kiasi kikubwa tunamhukumu mwalimu kwa kuangalia zaidi matokeo aliyoyapata.
namaanisha ili kocha apewe muda wa kutosha ni lazima awe na tiketi mkononi ya kuipeleka manchester united kwenye michuano ya ligi mabingwa haijalishi kwa kupitia mlango wa nyuma (nakusudia europe league kama alivyofanya jose mourinho).
liverpool ya miaka mitano iliopita haikuwa ajabu kiupande wao kukosa kushiriki ligi ya mabingwa kimapato na pia ndani ya uwanja ndio maana
jurgen klopp alipewa muda na hivyo hivyo kwa upande wa
tottenham hotspurs japokuwa na wao wameshaufahamu utamu wa ligi ya mabingwa ndio maana
andre villas boas alipofanya vibaya kibarua chake kiliota nyasi.
manchester united pamoja na kampuni ya adidas walisaini mkataba wa vifaa vya michezo wenye thamani ya paundi millioni 750 kwa kipindi cha miaka 10 (wastani wa paundi millioni 75 kwa mwaka), inasemekana kwenye mkataba huo kuna kipengele wameekeana cha kupunguza asilimia 30% (kutoka kulipwa millioni 75 hadi millioni 53 kwa mwaka) ya malipo endapo klabu itashindwa kushiriki ligi ya mabingwa kwa miaka mfululizo kama nitakuwa sipo sahihi wadau wengineo watakuja kunisahihisha.
usisahau pia klabu inawakata asilimia 25% ya mishahara wachezaji pindi klabu inaposhindwa kushiriki michuano ya uefa kila mwaka, hii inaonyesha dhahiri klabu haipo tayari kupoteza mapato yake kwa hoja dhaifu ya kujenga timu.
wewe jenga timu yako uwanjani lakini hakikisha unatupa tiketi ya uefa kila mwaka na hiki ndicho wanachokiwaza mabeberu waliovamia mchezo wa soka.
tujaalie leo hii timu ya liverpool ifundishwe na steven gerrard ambaye tayari wajinga wa kiingereza wanampigia upatu arithi mikoba ya fundi jurgen kloop halafu washindwe kushiriki uefa mfululizo unadhani wale wamarekani wataendelea kumpa muda wa kutosha wa kuendelea kujenga timu?
unajua kama liverpool wanaelekea kwenda kusaini mkataba wa kufuru na kampuni fulani kubwa duniani?
beberu hana rafiki kwenye fedha