Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu unaposema dominance ambayo hata fergie alishindwa cjaelewa ipo katka misingi ipi, kwa sababu man city epl kachukua mara mbili mfulurizo ila fergie alisha chukua mara tatu mfulurizo twice.
Sasa cijaelewa mbili inakuwaje dominance afu tatu isiwe.
Dominance niliyomaanisha ni kudhibiti club zingine zote kutochukua Ubingwa kwa mfano kwa miaka kumi Pep atakosa ubingwa labda mara mbili ingawa hii haijawa practical bado ila naamini kama atafikisha miaka minane pale Manchester city anaweza chukua EPL saba au sita tofauti na Mzee Ferguson ambae miaka 26 pale Old Traford kachukua EPL 13, sasa njoo kwa Pep miaka aliyokuwepo Barca Alikosa La Liga mara ngapi

Dominance ya kiukweli ipo Germany kwa Bayern , Italy kwa Juventus right now na France kwa PSG kwamba unakuta miaka kumi Bayern kakosa Bundesliga mara mbili tu na Dominance kama hiyo imeshaingia EPL kama Pep ataendelea kubaki miaka mingi

Na sio ya Mzee Ferguson miaka 26 Ubingwa mara 13 yaani nusu ya miaka yake ya Ukocha pale Old Traford ndio kachukua ubingwa
 
We jamaa sina Staha kwani nimetukana au kutumia lugha gani mbaya humu?
 
chief, aliyekutana na adhabu ya magoli saba alikuwa ni marehemu tito villanova.
 
Kuna Post hapo mbele nimesema hii Dominance imeshaonekana kuingia ila haijawa Practical

Msimu huu namuona Pep akichukua EPL na msimu ujao naamini itakuwa hivyo maana sioni wa kumzuia asichukue EPL. Spurs wanao uwezo kama watasajili ila wana lack Class , MUFC imeshaingiliwa na inatafunwa na mdudu anaitwa uzawa kama ilivyokuwa kwa Liverpool, kuhusu Chelsea sidhani kama tajiri wao ana moyo tena baada ya kufanyiwa figisu figisu za kambi ya nchi za Magharibi na chuki ya Waingereza kwa Warusi na kuhusu Arsenal wote tunaifahamu
 
Lini aseno kabeba kombe la epl mara tatu
Only united ndio kafanya ivi peke yake
 
Mechi gani pep alipigwa saba na buyern.....kama barcelona sidhani kama kocha alikua ni yeye
 
Na sio ya Mzee Ferguson miaka 26 Ubingwa mara 13 yaani nusu ya miaka yake ya Ukocha pale Old Traford ndio kachukua ubingwa
ngoja nichomoe nyuki waliolala muda huu:

kwa uoni wangu dhaifu miaka minne ya mwanzoni tokea akabidhiwe timu sidhani kama itakuwa ni sahihi kumhukumu sir alex kwa kushindwa kufanya vizuri kwa sababu aliikuta timu ikiwa ovyo sana na ilihitaji muda kuingiza idea na sera mpya za uendeshaji wa klabu ndani na nje ya uwanja ikiwemo kurudisha nidhamu bora ya kiuchezaji , tukumbeke ya kuwa hakuikuta united ikiwa kwenye ubora kama ilivyo nyakati hizi kifedha na hata kimipango endelevu.

kwangu mimi nautizama zaidi udhaifu wa fergie kutoka mwaka 1999 alipobeba treble hadi mwaka 2008 ambapo ni takribani miaka 10 ambayo alikaa bila ya kubeba ubingwa wa ulaya na wakati huo huo ndani ya miaka 10 hiyo kama nitakuwa nipo sahihi amebeba ubingwa wa ligi takribani mara sita, inawezekana zipo sababu nyingi zilizopelekea kukaa tena muda mrefu bila ya kubeba ubingwa wa uefa ikiwemo ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani kama vile ac milan, munich, madrid, na wababe wengineo.

je ligi kuu ya uingereza nayo ilikuwa ni dhaifu sana ndio maana fergie alikuwa anabeba ubingwa mara kwa mara kabla ya ujio wa matajiri wengineo mfano wa roman na mansour?

je inawezekana ujio wa matajiri mfano wa abramovich ulichochea kumtoa ferguson usingizini na hatimaye akatengeneza tena timu ya ushindani kama ya mwaka 1999 iliofanya vizuri kwa miaka mitatu mfululizo ndani na nje ya uingereza?


kwa timu aliyoijenga fergie nyakati zile baada ya kutoka kushinda makombe matatu (kizazi cha giggs,nevile brother, cole, yorke, beckham, solskjaer, keane, scholes, butt, stam) na nguvu aliyojaaliwa kuwa nayo kimatumizi ambayo aliijenga kwa nguvu na jasho lake mwenyewe (rejea usajili wa rio, veron, nistelrooy, rooney, berbatov, nani, anderson) hakupaswa kukaa tena miaka 10 ndipo abebe tena ubingwa wa ulaya, angalau ingelikuwa kila baada ya miaka 5 amebeba ubingwa basi ningelizidi kumpa heshima ya kuwa manager bora wa karne.

kwangu mimi namtizama sir alex kama ni mwalimu ambaye ndoto yake kubwa aliyokuwa anaipigania ni kuona anavunja kwanza utawala wa liverpool kimafanikio kwenye ligi kuu ya uingereza na si kuvunja mafanikio ya liverpool na timu nyenginezo kwenye ligi ya mabingwa.

mbona guardiola ana champions league mbili kwa miaka 10 ya ufundishaji wake soka?
mbona mourinho ana champions league mbili kwa miaka 15 ya ufundishaji wake soka?
mbona ancelotti ana champions league tatu kwa miaka yake 24 ya ufundishaji soka?
mbona zidane ana champions league tatu kwa miaka yake minne ya ufundishaji soka
maswali na majibu
tumuache sir alex ferguson apumzike.
 
Alivyokuwa nayo saba sasa hivi ana mangapi na Manchester ana mangapi in total? Au umehisi tu kubwabwaja?

Liverpool ndo timu yenye makombe mengi Uingereza yote immediately baada ya kuwa crowned Super Cup!

Huu mjadala nadhan sasa utarud rasmi na natabiri utapamba moto sana.

Mwaka 2001 baada ya Liverpool kuchukua Carabao , FA na Europa , Liverpool wakasema wamebeba Treble , man u wakasema hizo ni mickey mouse ,

Baada ya sasa Liverpool kuchukua UEFA super cup , naona mjadala unarud tena , nani ni most successfull in england , ubishi unakuja kutokukubaliana je NGAO YA JAMII ,UEFA SUPER CUP nazo ni Trophies? Kitendawili kinatakiwa kiteguliwe hapo.

Maana hayo mataji kwa Spain ,Italy, France , wanayahesabu vzr tu .

Kama tutayahesabu hayo kama mataji kwa england
Basi nadhan man u anakuwa most successfull team in england ,kwa tofauti ya mataji kama sijakosea ni 2-3, tukiyatoa anakuwa Liverpool kwa tofauti ya taji 1 ,
 
Eti lazima , ww jamaa unaendaga chaka sana
 
Miaka 26 ubingwa 13 haijafikia level ya Dominance wanayoifanya Bayern, Juve na PSG

Hiyo Dominance ya type ya kina Bayern na PSG ndio naiona Pep akiileta EPL

Off course nitakuwa mnafiki nisipokubali kuwa Fergie ni moja ya makocha wenye mafanikio makubwa duniani. Ferguson ni kocha bora kuliko Klopp au Ancelotti ila naona Pep ni kocha bora kuliko Fergie ingawa muda haujaniruhusu vizuri
 
Ila akiwa Bayern alichabangwa saba na Barcelona, mechi moja Messi akimlamba chenga maridhawa Boateng akaanguka na Messi akatikisa nyavu. Sina kumbukumbu nzuri ya idadi ya magoli.
Ilikuwa aggregate ya 5-3 Bayern/Guardiola akipigwa Knockout na Barça ya Enrique
 
Mkuu unaongea nadharia sana

Huyo Pep mwenyewe kaja England, msimu wa kwanza nusura akose big 4

Sasa unasema atachukua kwa miaka 10 mara 8 akose mara 2, unaijua future mkuu? Unajua Pep atakaa pale City miaka 10? Kwanza kwa kocha kuweza ku handle timu kwa miaka 10 bila vuguvugu la kufukuzwa au kuondoka ni ndoto,SAF aliweza na Wenger ndio walioweza kukaa zaidi ya miaka 10.

Unaongea kitu ambacho hakijatokea kwa base gani, na mimi nikisema ndani ya hiyo miaka 10 nina uhakika OGS atachukua makombe 8 utabisha kwa Hoja ipi? Wote hatujui nini kitatokea lakini for sure City haiwezi ku dominate ligi kwa mfumo huo kwenye ligi ya Uingereza kama yanayotokea ligi nyingine. Au umesahau juzi juzi Leicester City ametufundisha hilo kwamba hata timu usiyoidhania inaweza kuchukua kombe ligi ya Uingereza.

Kuhusu SAF hata usijaribu kumfanisha na Pep. SAF wakati anachukua United, United haikuwa title contender ilikuwa ni timu ya katikati tu mwa ligi. Lakini Baada ya kuichukua Man United akaifanya kuwa timu ya kugopwa Ulaya.

Halafu SAF hakuchukua mara 13 kwa miaka yote, usisahau makombe ya FA, Carling na UCL na ngao ya hisani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…