Nawasalimu wakuu. Na mimi naomba nitoe Mtazamo wangu kuhusu timu yetu kabla ligi haijaanza.
Kwanza nadiriki kusema tumefanya usajili nzuri(kiasi) kutokana na matakwa ya kocha japo hatujafikia hatua tuliyo penda(wengi wetu).
Usajili wa Wan na HM, kurudi kwa Mensah na Tuamzabe utatusaidia kuimarisha defense yetu ambayo kwa muda mrefu ilikuwa majanga. Kwa upande wa ulinzi tume improve kutoka tulipo Kuwa misimu kadhaa iliyo pita. Tuombe MUNGU injuries zikae mbali na wachezaji wetu.
Kati kati bado tuna tatizo. Kwa Kuwa kuna watu wamepungua na ilibidi tutafute replacement, ila kwakuwa Malengo yetu sio kugombea ubingwa(ukweli mchungu) na basi tuwape muda watoto ambao wako talented kama Mctomminay,Perreira na back up ya (Tuanzabe na Mensah) + Fred+Pogba+Matic(japo amechoka ila hakuna kijiji kisicho na wazee) huku tukifanya addition ya kiungo katika madirisha mawili yajayo(January+next summer).
Japo binafsi nilitamani sana kama tunge mpata BF.
Kuhusu wings, naona tume improve,hasa kutokana na uwepo wa WB upande wa kulia ambako kulikuwa na tatizo sugu. Naamini AW+James/Dalot tutakuwa na Uwezo wa kupeleka mashambulizi kutokea kulia pia. Kushoto ndio ilikuwa strength yetu na haijavurugika, huku tukiomba Shaw asiende wodini tena.
Upande wa ushambuliaji. Kwa mtazamo wangu naona Ole amefanya uamuzi sahihi kumuacha Lukaku na kuto sajili mtu. Kwa nini nasema amefanya kitu sahihi?
Kwanza Ole alikuwa haamini kama Lukaku ana fiti Kwenye profile yake(hii haimaanishi Kuwa Lukaku ni mbovu na sita shangaa kama atakiwasha huko aliko kwenda). Ni jambo la kawaida hasa Kwenye Mpira wa sasa.
Lakini pia ukiangalia tetesi Nyingi za washambuliaji tulio Kuwa tuna husishwa nao hawana tofauti sana kiuchezaji na Lukaku. Na kwa nilivyo muelewa Ole hataki timu iwe na mshambuliaji mmoja wa ku stick mbele, anahitaji wachezaji wanyumbulikaji, na hii itasaidia Kuwa na vyanzo vingi Vya magoli. Kutoka kati kwenda mbele. Rashford,Martial,Sanchez,green wana fit Kwenye hiyo profile. Kwa hiyo hakukuwa na haja ya kuongeza MTU kama hawa watu wapo na
Note: Malengo yetu sio kugombea ubingwa.
Kwangu Mimi kitu alicho feli OLE ni kuidhinisha Jones,Smalling,Young,Rojo kupewa mikataba mipya wakati wangeweza kuondoka na kusiwe na madhara.
Mwisho niwashauri mashabiki wenzangu Kuwa msimu huu inabidi tushushe matazamio yetu(lower expectations) na tujiandae kwa Matokeo yoyote. Njia rahisi ya kufuzu uefa ni kushinda Europa.