Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nilijiandaa kisaikolojia kupokea matokeo yoyote ligi ikianza baada ya kuona harakati zetu za usajili zilijaa tetesi za magazetini bila uhalisia wowote.

Dirisha la usajili limefungwa tukiwa tumesajili wachezaji watatu na nusu. Nasubiri maajabu kutoka timu yangu pendwa ya man u.

Ni maajabu kwa timu kama man united kufanya vibaya kwa sababu ya kutokusajili vizuri.

Lakini ni maajabu pia kwa timu kama hii kufanya vizuri katika ligi yenye timu zaidi ya 8 zenye ubora wa hali ya juu.

Tukutane Sinza kijiweni jumapili kushuhudia maajabu.
 
mkuu cooper ameongea wish ya OLE ni kama ya mashabiki, alitaka midfielder creative na winger wa kulia kabla ya dirisha la usajili, ila woodward ndio amefeli kudeliver,
kuhusu winga wa kulia bado naikumbuka comment yangu nilioiandika humu ndani baada ya kutangazwa usajili wa daniel james.
nilisema OGS atakuwa amefanya kosa kubwa sana la kuruhusu usajili wa bwana mdogo ikiwa ana mipango ya kusajili winga mwengine kwa sababu ed woodward hatoweza kulipa tena fedha kwa usajili wa mchezaji anayecheza nafasi ya winga.

hatimaye yametimia​
 
Kimsingi tukubali kwamba MU haitaki kufanya mabadiliko yoyote yaan hatuna plan yoyote kurudi kwenye mafanikio tulio kuwanayo....maana hatueleweki kama tunataka kufanya investment kama ilivyo kwa man city au kutafuta wachezaji kwa njia ya academy....yaan hatuna tafauti na Everton au westham.....ambaye anaelewa kinachofanyika MU atuambie tuelewe? Au anaeiona MU ikipigania ubingwa au kuchukua kikombe chochote aweke wazi?
Ebu linganisha spurs na man u?
Ebu linganisha arsenal na man u?
Ukiangalia apo kwa msimu huo unaokuja spurs anapossibility ya kutoa ushindan kuliko man u...inawezekana akabeba hata kikombe kimoja...angalia kocha aliyepo na mwenendo wa timu...vile vile kwa arsenal mwangalie kocha wa arsenal then linganisha na anacho kifanya kocha wa man u?
Apo sijaongelea liverpool na man city maana kuwaongelea nikujiaibisha
 
Ukiniambia mimi ni rank timu zipi zilizosajili vizuri (kwa top six) kulingana na mahitaji yao, wa kwanza nitampa Man City, wa pili Spurs na wa tatu atakuwa United kisha Arsenal na Liverpool. Chelsea wao hawakusajili kabisa
mkuu unataka kutuambia ya kwamba arsenal hawakuhitaji mlinzi wa kushoto?
arsenal hawakuhitaji mlinzi mwenye uzoefu kama david luiz?
arsenal hawakuhitaji kiungo mwenye uwezo kama alionao dani ceballos?
arsenal hawakuhitaji kiungo mshambuliaji na mfungaji mfano wa pepe?

pepe licha ya kufunga magoli mengi msimu uliopita pia ndiye mchezaji wa pili kwa kuhusika na utengenezaji wa magoli kwenye ligi ya ufaransa, kwa viwango vya wachezaji tulionao yupo mwenye uwezo wa kumweka nje pepe?
yupo mchezaji mwenye uwezo wa kumweka nje lacazette na aubameyang?
ukimuondoa pogba yupo kiungo mshambuliaji mwenye uwezo wa kumweka nje ozil huyu aliyeshuka kiwango na hamasa ya upambanaji?

kosa kubwa walilolifanya arsenal ni kumsajili mchezaji kwa fedha nyingi halafu wakambakisha kwa mkopo, dhambi hii ndio itakayowatesa kwa sababu mpaka dirisha linafungwa wameshindwa kupata mlinzi mwengine wa kati mwenye uwezo?

mkuu usisahau msimu uliopita arsenal walimaliza juu yetu kama bado kumbu kumbu zangu zipo sahihi.
 
Wakuu Licha ya wengi kulaumu kuhusu kuuzwa lukaku Mimi nilivyomuelewa solskjaer ni kuwa lukaku hakuwadanganya anafutilia kwenye pressing style yetu, kocha anahaki ya kumkubali na kumkataa mchezaji kwasababu anazoona yeye zinafaa.....mwisho tusubiri ligi ianze ndo tulaumu maamuzi ya solskjaer ila Mimi naamini pengo la lukaku halitaonekana labda pengo katika midfield
 
Hili nalo neno mkuu, kwa akili ya Woodward haangalii kiwango, potential, Wala Nini, kwenye vitabu vya mahesabu ameshatick winger.
 
sipingi sera ya kuwapa nafasi ya kucheza timu kubwa wachezaji wanaotokea kwenye academy, tatizo ni kwamba hii timu kubwa tulionao ina matatizo mengi ambayo si rahisi kutatuliwa na wachezaji wachanga.

kama tungelifanya usajili wa nguvu kama ule wa real madrid msimu huu halafu tukaingiza damu changa kutoka academy basi nisingelikuwa na khofu yeyote ya kufanya vibaya kwa timu yetu msimu huu.

hawa vijana wetu mfano wa tahit chong, greenwood, gomez wangeliufurahia zaidi mpira wao kama ingelikuwa wamezungukwa na mafundi mfano wa bruno fernandez, pogba, pepe, james madison, harry kane, ndombele,thomas mounir.

Mfumo huu ndio aliokuwa anautumia sir alex ferguson wa kuingiza damu mpya kwenye kikundi cha mafundi wenye kujielewa ndio maana klabu ilifanikiwa kupata faida ya vijana kwa muda mfupi mfano wa ronaldo, scholes, neville brother, beckham n.k
unadhani wayne rooney, beckham, scholes, ronaldo na wengineo ingeliwachukua miaka mingapi kwa kikosi hiki tulichonacho kuufuahia mpira wao?

jaribu kufikiria unazungukwa na ashley young, phil jones, jesse lingard, darmian, rojo kwenye timu unadhani itakuwa ni rahisi kukuza kiwango chako?

angalia mfano mwengine wa barcelona , msimu wa mwisho wa rijkaad barcelona tuliwatoa nusu fainali kwa goli la mtakatifu paulo, hii ina maana ya kwamba barcelona hawakuwa na timu mbovu na ndio maana guardiola msimu wake wa kwanza alifanya mabadiliko madogo sana ya usajili na kimfumo.

barcelona ile ilikuwa na etoo, henry, hleb, marquez, pique, abidal, toure, xavi, iniesta ndio maana ilikuwa ni rahisi sana kwa wachezaji wenye vipaji mfano wa bosquet, pedro, pique kukuza viwango vyao kwa sababu walizungukwa na wachezaji watakaowafanya waufurahie mpira wao kwa uhuru tofauti na timu yetu ya sasa iliojaa maiti wa soka.
 
Hili nalo neno mkuu, kwa akili ya Woodward haangalii kiwango, potential, Wala Nini, kwenye vitabu vya mahesabu ameshatick winger.
kama ningelikuwa solskjaer ningelimlazimisha sheikh woodward aniletee jadon sancho au philipe coutinho.
kwa jinsi bwana yule anavyopenda kiki angelitumia nguvu yoyote kufanikisha usajili huo hata kwa kumhonga wakala paundi millioni 20.

lakini unaweza kukuta bwana ole ndiye aliyekataa usajili wa majina na si ed woodward kama tunavyojiaminisha
 
Wanavyodai Sancho anakuja UTD Kama longterm plan, huwenda dirisha lijalo Kama tutafuzu Champions league.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…