M Z A N Z I B A R I
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 21,697
- 117,129
nilijua utanijibu hivi na si kwamba nilikuwa sifahamu sababu ya klopp kumpanga milner badala ya alexander arnold.Alimuweka Milner ile nafasi sababu Milner anajua kukaba ili man Utd wasiitumie left flank
kwa kuangalia kikosi cha man utd kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kumfanya klopp aingie uwanjani huku akiwa tayari na wazo la kujilinda kwa kuhofia mashambulizi upande wa kushoto?
ndio maana nikasema makocha baadhi ya nyakati wana nidhamu ya uoga, hutumia mwamvuli wa game plan kwa ajili ya kuficha khofu zao