Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Robin Van Persie na Zlatan ndo usajili bora wa mwisho kuufanya United.
 
Tatizo kubwa la Man Utd ni timu nzima.

Hata Lukaku ni striker mzuri ila kama una winger kama Martial unategemea nini? Kiungo kipo hovyo, beki kimeo yani shida tupu.

Lukaku ataenda timu inayompa mipira kwa wingi utaona atakavyokuwa moto.
 
Sidhani kama siku za karibuni tutakuja pata wachezaji kama Rio na VDS.

Walikuwa viongozi haswa.
 
Daaa hao wahuni wana zali sana
Hawa Wahuni Wanabahati kubwa,Walitakiwa wawe washapisha nafasi za watu muda mrefu,labda Mtukwao inashika nafasi.

Wahuni hawa nitafsri sahihi ya kuvuna zabibu katika Mtini.

Miaka zaidi ya minane Old Trafford walau hata sifa ya kuvaa tambala la Ucaptain wanapwaya,Mpaka unafikiria Bwana mdogo MCtominay avae kitambaa,bwana domo zito degea bado anapwaya.

Inawezekana Man United pia tunatatizo la kiongozi ndani ya Uwanjani(Captain).

Hawa jamaa tunaweza kwenda naona mdogo mdogo mpaka msimu wa 24/25...Wanatafuna mijihela Man United kimya kimya bila Wasi.

Kuna baadhi ya mashabiki wanaomba wahuni hawa watoke ili mioyo yao ipone.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Hahahaha kuhusu lugha umenikumbusha kuhusu Tevez, alishindwa kabisa kujifunza lugha ya Malikia

Antonio huko nyuma akiwa Wigan na wakati anahamia United, niliijua hiyo story ya kushindwa kui master lugha ya kiingereza, lakini alivyokaa United na baadaye akakabidhiwa kitambaa cha unahodha sijui kama tatizo la lugha liliendelea (logic yangu, ni mchezaji anapewaje ukapteni kama hana uwezo/anawasiliana kwa tabu na wachezaji wenzake?)

Valencia aliwahi kusema alivyokuwa anacheza huko kwao Ecuador, kuna siku alikuwa home na Familia ya kwao wanaangaalia mechi moja pale Nou Camp, akawaambia ipo siku nitacheza hapo, basi Familia yake wakiwemo wazazi wake wakamcheka sana. Anakwambia miaka kadhaa mbele (alivyokuwa United, akaichezea United dhidi ya Barca pale Nou Camp). Hii story ilinifundisha jambo kubwa sana kwenye maisha yangu

Antonio ni fighter sana, lakini umri umemtupa mkono. Ngoja tusubiri mbadala wake kwenye usajili dirishi hili.
 
Ya walikuwa viongozi,Na Man United ya sasa sioni kiongozi Uwanjani.


Kuna kipindi cha nyuma watu wakata wanamlinganisha Degea na VDS nikainamisha kichwa chini kwa ishara ya huzuni.

Degea bado sana kuvaa viatu vya VDS achilia mbali kulegeza kamba ya viatu vya Shumaico.
Sidhani kama siku za karibuni tutakuja pata wachezaji kama Rio na VDS.

Walikuwa viongozi haswa.
 
Watuletee yule Zyech wa Ajax atembee pembeni
Hakim Ziyech RW (26 years)-release clause £25m
Tomas Partey DM(26 years)-release clause £43m
Toby Alderweilerd(30 years) release clause £25m
Jumla ni £93 unapata wachezaji wazuri na wenye uzoefu na viwango
Tatizo our decision makers know nothing kuhusu football wapo wachezaji wazuri sio wa bei kubwa ambao wataimprove United
 
Uongozi wa AJAX umesema upo tayari kumuachia Hakim Ziyech kama atahitaji kuondoka msimu huu.
 
Kuna kipaji kipya cha mpira ukimwangalia uchezaji wake ni kama mesut ozil tofauti yy na ozil yeye ni mfungaji alafu anacheza mpira wa speed.. Anaitwa Kai havertz ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ana miaka 19.. Ana magoli 11 kwenye ligi yao na assist 6 hivi ni raia ya ujerimani na ananipiga bayer leverkusen.. hapo man utd hatumuoni huyu kijana tulambe dume kwa bei ya kawaida.. he is very talented young player.. Pengine msimu ujao akitakiwa pesa ndefu itatumika kwa anaye mhitaji.. ningekuwa na uwezo ningepiga simu au ningeshauri tumchukue huyo kijana anacheza ligi kuu ya ujerumani aka Bundesliga... Wadau mtafuteni mulete ushuhuda me niliwahi muona mechi moja kwenye star times live match toka hapo nikasema nimfatilie anakipaji Sana huyo ni *Kai havertz*
 
Kuna mahala nilisoma kuwa Man u inamfanyia Monitoring Kai Harvetz kiukweli ni mchezaji mzuri japo epl inapressure kubwa kuliko ligi zingine
 
juzi kati tulisikia uongozi wa timu yetu ulimpa De Gea wiki moja ili asaini mkataba mpya ama wampige bei....lakini mpaka leo kimya sijui imeishia wapi ile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…