Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Umeona sasa, hapo inabidi mshinde au siyo.
Sisi Man United tutawachia majirani zetu washinde ili watuwakilishe vema kwenye sherehe za ubingwa. Hatuwezi kukubali kukosa vyote aise ..itakuwa ni aibu kwa jiji zima la Manchester..

Wewe pambania uefa atleat ushinde hata gemu moja ..maana kumpiga Barca gemu zote mbili hutaweza..
 
Mechi ya kesho mnatoka draw na everton.

Jumatano mtampiga Man city 3-1, alaf mechi ya chelsea mtapoteza 1-0.

Nipigwe mawe yasipoteka haya matokeo.
 
Bila Manchester United imara hakuna Liverpool imara.

Hebu fikiria kina AROON wa Arsenal wanavyotupigia kelele! Komaeni turudi kwenye ushindani.
Mkuu man u kuwa imara mpaka watakapo tengeneza uongoz imara ,hii man u ya kusajiri kwa sifa hakuna anayeiogopa, itaendelea kushuka na kushuka zaidi,

Liver pambanen na mech zenu, man city hana cha kupoteza , msitegemee manyua hii mbovu iwasaidie
 
Takribani yamebaki masaa 2 kabla kipute kuanza kupigwa pale Godsonpark, moja kati ya mechi ngumu kwa United lakini pia mechi muhimu sana

Kikosi kikichosafiri kimekwenda bila Ashley Young na Ander Herrera lakini sehemu kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza wamesafiri

Mechi ya leo itakuwa ngumu sana kwetu kwa sababu kadhaa. Kwanza, kwa sababu tupo ugenini, toffees wameonesha wana uwezo wanapokutana na wakubwa, juzi juzi tu Chelsea kisha Arsenal wametolewa kamasi pale Godsonpark.

Kingine kinachiweza kuifanya mechi kuwa ngumu, ni kama OGS hajawaandaa vizuri kisaikolojia wqchezaji, maana siku kadhaa zilizopita tumetoka kupigwa na Barca, hivyo hii inaweza kupunguza confidence yetu, lakini ukweli utabaki kuwa Everton is no where near Barca, ability wise.

Kwa upande wetu tuna uwezo wa kupata matokeo, yaani ushindi. Tukumbuke hii United ndio ile ile iliyoshinda mechi 12 kati ya 14 baada ya OGS kuwasili pale OT. Hivyo hatuna haja ya kuwa na wasiwasi sana.

Pia, fomu yetu nje ya OT sio mbaya kwa hiyo hatuna sababu ya kuihofia Everton (hapa nieleweke haimaanishi OT hatupati ushindi)

Tumalizie na stats

Everton Vs Manchester United

Michezo waliyoshinda 69, Waliyopoteza 88, Waliyodroo 43

Everton nyumbani, kwa miaka 10 iliyopita
Wameshinda 6, Wamepoteza 12, Wamedroo 4

Everton nyumbani, kwa miaka 5 iliyopita
Wameshinda 2, Wamepoteza 7, Wamedroo 2

Tangu Oktoba, 2015 Everton wamepoteza mara 6 na kutoa droo mara 2, hawakupata ushindi wowote

Line up ninayoipendelea (kwa mujibu wa waliosafiri)

Degea, Dalot, Darmian, Smalling, Lindelof,

Fred, Scot, Pogba

Rashford, Lukaku, Martial
 
Dalot! Martial! Hawa ndio wachezaji watakaomng'oa OGS Old Traford. Yaanni Martial anamuweka nje Mata! Sijisumbui kuangalia hii mechi. Ngoja nipeleke watoto beach. Pumbaf.
√Sasa kwa alivyocheza Young gemu ya Barcelona anaanzaje kucheza leo??

√Martial ni hovyo pia ila ukimpanga Mata mbele ya Martial hayo yatakuwa masihara..maana Mata ameshachoka..yaani ni sawa kusema Amber rutty ni mrembo kumshinda Amber Lulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…