Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Lakin utambue man u hawez kucheza kati au kutawala hasa kwa timu kama Barcelona,

Man u miaka yote kwa timu zinazopossess huwa hachez mpira wa katikati, zaid huwa anatumia counter attack akitumia zaid winger za kulia na kushoto ,

Na hiyo ndio njia pekee ya man u kupata matokeo ,

Na kitu kingine kitakachowaponza ni kumkabidhi MTU amkabe au atembee na messi, hiyo itawaletea madhara makubwa ,kwanza sio rahis kumkaba,pili mtaacha nafas kwa wengine waadhibu,

Kama umemsikiliza mou anasema njia ya kuwadhibiti barca ni kuziba mianya yao ya mipira ,huku mkicheza counter, hapo alikuwa anazungumzia jinsi inter ilivyoidhibit barca kipind chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sishangai maana aliyeandika hivi ni LUKAKU
 
Wewe naona unataka nipotezea muda tu...Kama mpka sahv huelewi maana ya kibonde bac tafuta mchezo mwingine ushabikie
Mm nashabikia Man city, kwann unataka nitafute mchezo mwingine, inamaa wewe ndo upo sahihi tu huwezi kosolewa. umekosea sasa unataka nikubali tu unachosema, mbona humu jamvin watu wanaeleweshana na wapo wanaokosea ila wanaelewana tu. ila sorry kama hupendi kukosolewa. kuna watu huwa hawapendi kukosolewa wanakuwa wakali mpaka wanasema asietaka na aondoke, ukimkosoa atasema sipangiwi.
 
Huu ndo ushujaa mkuu,Hata kama unajua mechi Fulani huwezi kushinda unajitapa kuwa unashinda ndo football hiyo
Wewe ndo ulietusemea kwamba sisi tulikuwa tumejiandaa kisaikolojia blaa blaa...lakini sisi Utd utamaduni wetu ni kuwa kila game tunayotia mguu tunajua tunaenda kushinda, kama ikitokea vinginevyo sawa, lkn mentality yetu siku zote tunajua kila game tunaenda kushinda!!
Eti ki_dimaria kikaja kulewa Old Trafford, kilichomkuta huko ufaransa angalau ana stori ya kuwasimulia wajukuu zake!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
upo sahihi sana brother tunahitajika kumtafuta DIRECTOR OF FOOTBALL kama walivyofanya wapinzani wetu wakubwa barani ulaya kwa haraka, tatizo kubwa nililoliona mimi baada ya kuondoka sir alex ferguson ni kwamba klabu nayo iliamua kuivunja misingi yote ilioanzishwa na ferguson kwa miaka takribani 25, kazi aliyokuwa anaifanya ferguson ilipelekea klabu isione umuhimu wa kutafuta DOF ndio maana utamaduni wa kuajiri DOF ulikuwa ni mgeni ndani ya klabu japkuwa klabu nyengine kama barcelona, juventus, sevilla walishakuwa na utamaduni huu.

kuanzia david moyes hadi jose mourinho ukiangalia sajili nyingi zilizokuwa zikifanywa zilitokana zaidi na vipaombele vya mwalimu na si falsafa ya timu ndio maana tumeshuhudia ndani ya klabu yetu tumejaza wachezaji wenye kuendana na falsafa ya manchester united na wale wasioendana falsafa.

waangalie manchester city tokea wamlete Txiki Begiristain, Ferran Soriano. na josep guardiola wamekuwa wakifanya biashara ya usajili kwa kuangalia zaidi mchezaji atakayeendana zaidi na falsafa ya timu kiuchezaji na kwa ushahidi wa hilo jaribu kurejea sajili za danilo, walker, sterling, bernardo silva, ederson, jesus, sane, gundogan hawa wote wana uwezo wa kucheza soka linalofundishwa na guardiola, hata ukiangalia umri wa wachezaji wao wanaowasajili wengi wao wana wastani wa miaka 22- 26.
hivyo basi hata kama itatokezea siku moja josep guardiola ataondoka manchester city kikubwa watakachokifanya ni kutafuta mwalimu atakayeendeleza falsafa ilioasisiwa.

lakini ukija kwetu mambo ni tofauti kuanzia sajili za makocha, sajili za wachezaji na mifumo ya makocha wote waliokuja wametelekeza misingi yetu.
  • alipokuja david moyes kosa kubwa la kiufundi walilofanya manchester united ni kumruhusu atelekeze benchi lote la ufundi aliloliacha ferguson, hii ilikuwa ni dalili ya kwanza ilio dhahiri yenye kuonyesha anguko la klabu kiutamaduni, haitoshi klabu ikaruhusu usajili wa marouanne fellaini ambaye haendani kabisa na mfumo wetu wa kiuchezaji, barcelona wasingeliruhusu upumbavu huu aliotufanyia moyes japokuwa na wao wameanza kupoteza muelekeo kwenye usajili.
  • kituko chengine ni ujio wa LVG na falsafa yake ya 3-5-2 na kumiliki mpira kwingi bila ya mipango, mpaka unafika nyakati unajiuliza tokea lini manchester united na kumiliki mpira kwa muda mrefu bila ya kufika golini?. Usajili wake pia ulikuwa ni wa ajabu ajabu ndio maana wachezaji wake wengi waliishia kufeli.
  • alipokuja jose mourinho kama ni wafuatiliaji wazuri wa mahojiano yake utagundua ya kwamba jamaa alitaka klabu iachane rasmi na tamaduni yake ya matumizi, jose alitaka tuwe kama manchester city, madrid ya zamani au psg kwenye market. Alivyokuwa anataka yeye ni kwamba kama itatokezea amesajili mchezaji halafu akashindwa kuendana na matarajio yake basi atafutiwe mwengine jambo ambalo ed woodward hakuvutiwa nalo. Kiupande fulani mourinho madai yake yalikuwa ni ya msingi kwa mfano ishu ya winga wa kulia, kushoto pamoja na walinzi wa kati, lakini baadhi ya madai yake hayakuwa sahihi hususani mahojiano yake baada ya kufungwa na sevilla pale aliposema sevilla wana wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza kikosi cha kwanza cha man utd. Uwepo wa OGS unajaribu kutuonyesha madhaifu ya jose mourinho na wakati huo huo uwepo wake unajaribu kutuonyesha madai sahihi ya jose mourinho.
director of football anafanya kazi tofauti kutegemeana na mahitaji ya klabu husika, ishu muhinu zaidi wanahusika zaidi na ishu za negotiations kwenye usajili wa wachezaji hivyo basi inategemea zaidi na mahitaji ya klabu ya manchester united, lakini mwisho wa siku mwenye maamuzi ya kutafuta wachezaji anaowahitaji kwenye timu ni kocha na benchi lake la ufundi, ina maana director anapaswa kufanya kazi kwa ukaribu na kocha mkuu huku akipeleka repoti kwa CEO ambaye ni ED WOODWARD.

cha msingi ni kupata DOF mwenye uwezo wa kusaka wachezaji watakaoandikwa vizuri kwenye historia ya klabu siku za mbeleni na pia atakayekuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ukaribu na benchi la ufundi kwa masikilizano pamoja na kushauriana juu ya mwenendo wa klabu, bila ya kusahau tupate wachezaji wanaoendana na modern game, ni bora kupata wachezaji wanaojituma lakini wawe na vipaji kuliko kuwa na wachezaji wanaojituma lakini wakakosa vipaji vya soka kama sajili zetu tulizozifanya miaka 6 iliopita.

Mwaka 2010 ndani ya klabu ya real madrid kulizuka mgogoro mkubwa wa kimaslahi kati ya jose mourinho na DOF jorge valdano. Kama kawaida yake mourinho alihitaji striker mpya wa kumuongezea nguvu na hili lilitokana na gonzalo higuain kupata majeruhi lakini pendezo lake lilikataliwa na jorge valdano, wawili hao wakawa hawazungumzi kwa muda mrefu na mwishoni hatimaye madrid wakafanya maamuzi ya kumuondoa JORGE VALDANO, ni matumaini yangu tatizo hili halitajitokeza ndani ya manchester united.

Tatizo kubwa ambalo pia naliona kwa sasa ni kwamba bado hatujamfahamu ole gunnar solskajer kwenye soko la usajili kiundani zaidi, hatujui kama OGS ni asset kama walivyo makocha wengineo mfano guardiola, jose mourinho au jamaa ni liabilities kama alivyokuwa LVG na david moyes. Kama jamaa atakuwa ni hodari kwenye kutafuta wachezaji wanaoendana na ubora tunaouhitaji basi ushirikiano wake na DOF utakuwa ni wa mafanikio makubwa sana lakini kama itakuwa ni kinyume chake basi tujiandae kisaikolojia kutafuta mwalimu ajaye dirisha lijalo la usajili pamoja na DOF mpya.

  1. kuandaa mipango imara ya uendeshaji wa klabu kuanzia academy kwa kuweka kipaombele cha umri kwa wachezaji tunaowatafuta, kama tungelikuwa makini miaka iliopita hatukupaswa kuruhusu dili la rafael kwa darmian, falcao kwa chicharito, cleverley kwa schneiderlin na schwensteiger.
  2. kuhakikisha utamaduni wa klabu unafuatwa vilivyo na makocha waliopo hususani linapokuja suala la usajili wa wachezaji, barcelona wamewasajili arthur melo, de jong ni kwa sababu wanaendana na utamaduni wao lakini ukija kwetu ni tofauti, tunacheza counter attack lakini usajili tunaoufanya ni wa marouanne fellaini na juan mata.
  3. DOF anapaswa kuwa ni daraja kati ya viongozi wa klabu na kocha mkuu na si kinyume chake, kama DOF atakuwa ni paka wa familia ya glazer itakuwa ni kazi bure.
  4. awe ni mtaalamu kwenye sekta ya usajili na kusaka vipaji ili kuepusha tena kuuziwa wachezaji kwa bei za gharama, mfano usajili wa fred kutoka shakhtar donetsk.
  5. masikilizano na kushauriana ndio msingi wa mafanikio.

wiki mbili zilizopita niliona habari ya arsenal kumuhitaji monchi awe DOF ili afanye tena kazi na unai emery.
leo hii nimeona taarifa ya sevilla wanahitaji kumrudisha monchi ndani ya klabu yao.
kama namuona monchi muda huu anavyotikisa gilasi yake ya wine.

The Spanish club’s president Jose Castro said: "We're looking for the best Sporting Director, and that is Monchi.
“We have begun negotiations and we want to reach an agreement soon. Our conversations go very well with him. We hope to reach an agreement soon.”
 
Mkuu umeeleza vzr sana , hakika upo deep, kwasasa bila DOF timu itakuwa inayumba na sokon unajikuta unauziwa magarasa au wachezaj wazur ila hawaendan na mfumo

Mfano mou alipomleta Fred, au Sanchez, mm siamini kama hawa wachezaji ni wabovu ila naamin mou hakupata ushauri mzuri kutoka kwa DOF, kama angekuwepo

Pale arsenal tulimleta bwana mmoja fund sana anaitwa Sven mislitant

Huyu bwana amekaa arsenal miez michache lakin kazi yake tumeiona, kwa bajet ya £70m ,alienda Italy akatuletea toreira, anaenda ujeruman akatuletea golikipa ambaye kwasasa ameshamstafisha babu cech ,

Huyu bwana alikuja kushindwana na kocha emery kuhusu wachezaj , emery anamuhitaji Denis Suarez coz anaona atafit mfumo, Sven yeye ana watu wake mfukon, wakashindwa kuelewana, amesepa

Bwana Monch naona anarud sevilla,

Hivo tunamgeukia Marc overmas , ambaye amefanya kazi kubwa hapo Ajax wakiibua kina mattjs, de jong n.k

Kwasasa DOF kwenye timu hakwepeki, tofauti na zaman makocha kama fergi, Wenger hawakuhitaji DOF ,now soka limebadilika

Man u kwa bajeti yenu ya usajiri hamtakiwi kuhangaika hivi, mnapokuwa na DOF mzuri na bajeti ni Nene , haichukui madirisha mawili mabadiliko utayaona tu, kama inavyotokea kwa city,



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nlivyokua nkisema kati sikumaanisha kuposses bro.. Nlikua namaana nyingi kuharibu mipango yao kutokea kati mfano messi ni play maker wao mzuri ila anachukua mipira kati na kuanza kufanya planning hivyo tukikivuruga kati vizuri basi tutawaweza.. I hope..

Wachezaji wengi nakumbuka wamejitaidi kumzuia messi kutokea kati refer kante ya france kumzuia kati uku beki line yetu ijitaidi pia.. Ila tukisema beki akamkabe maalum messi huenda tukajitaidi ila siamini ilo..

Ile inter kwa kumbukumbu zangu na mou alivyosema waliwaacha wauchezee mpira kwakua hiyo ni cariba ya barca na ni ngumu kuizuia ila wao walikua wakijitaidi kuharibu mipango ya kutokea kati hadi kwa Lucio uku chini
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nikupongeze kwa analysis nzuri,
Yote uliyosema ni kweli.
Mimi kwa upande wangu nikiri sio mpenzi wa possession based football, ile kama ya barca. Maana naamini kuna njia nyingi za kushinda mechi.

Ninachokitaka tukipata mpira isiwe rahisi kuupoteza pale kwenye midfield. Nadhani hii inasababishwa na baadhi ya players tulionao, kama ulivyosema. Watu kama Smalling, young etc hawa wanaturudisha nyuma.

Anyway, naimani ole akipewa nyongeza ya players +pre season, ili tatizo litapungua kama sio kupotea.
Tuwe kama Man u ya SAF, timu pinzani wanakuwa na mpira but wanajua wakipoteza tuu mpira wamekwisha.





Sent using simu mbovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…