Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mpira ungedunda kama sio hawa majaruhi tulionao na kadi ya Pogba.
Kiongozi usikate tamaa.

Majeruhi yasikunyime raha.

Huwa tunaongea kwa upenzi/ushabiki/utani n.k, ila kwenye KABUMBU maajabu yanawezekana na huwa yanatokea.

Mfano mlipocheza na JUVE, alikupigeni Goli Moja kwenu na nyie mkaenda kumpiga kwake Goli 2 kwa Moja.

Na afadhali hivi sasa naweza kusema mnaelewana, kuliko mlipokuwa na MOURHINO pamoja na yote mkatoka na Ushindi wa Bao Mbili kwa Moja ugenini
 
Hahahahahaha mkuu umenichekesha sana kuhusu uwezekano wa Herera na Matic kuwepo kwenye game ya PSG

Kiufupi hiyo haitawezekana, japo inasemekana Matic na Martial wapo karibu na game ya Arsenal wanaweza kucheza

Ndugu yangu Wazungu ni watu ambao ni honest sana (kwenye mambo ambayo yapo wazi) na ku cheat kwao ni kashfa kubwa sana. Kwa hiyo kudanganya kwamba hao jamaa hawatakuwepo halafu ghafla kwenye mechi wakawepo haitawezekana

Ila kuna positivity kuhusiana na kikosi chetu kama ulivyosema. Kwanza madogo hao ni watu wasiojulikana kwa PSG hivyo kudeal nao inaweza kuwa changamoto kwao.

Pili madogo watataka waoneshe uwezo wao kwa ajili ya future yao na tatu PSG wanaweza waka relax wakiona hawa madogo hawataweza kuwafanya kitu, na hadithi ya yule aliyedharau mwiba na mguu ukaoza ikadhihirika.

Kubwa zaidi ni matokeo ya jana ya Madrid na Ajax yamethibitisha anything can happen katika soka, iwe nyumbani au ugenini

Jambo lingine United wanaenda kucheza wakiwa hawana pressure kwani watu wanaamini kuwa tumeshatolewa. Hii inaweza kusaidia kucheza mpira kwani pressure kwa wachezaji huwa sio nzuri

Kiufupi game ni ngumu na United bado anaenda kama underdog lakini mpira siku zote umekuwa mchezo usioboa sababu ya interesting results

Let's wait and see mkuu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
OGS asema kwa sasa ana mkataba na United tu. Tutakumbuka kuwa ni Desemba 3 tu club ya Molde (alipokuwa OGS) walisema kuwa OGS amekubaliana na club yao kwa miaka 3.

Pia wakati anakuja United, Molde walisema kwamba wanatuazima OGS mpaka May. Ghafla leo kuna story hii.

Hili picha linaelekea patamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioni tukipata chochotw kwa PSG leo kikosi kilichosafiri sio cha kushindana na hawa jamaa
 
Gareth bale ameisha..hapo tunapaswa kuleta watoto very talented..kama kina Tahiti chong au Sancho
Hili nakubaliana naww sanchez timu imemshinda kbs na haya majeraha ya mara kwa mara ndio yanamaliza kbs


Tukatafute mtu nadhani tukimpata gareth bale atatusaidia na hivi madrid wanavyomzingua ndio wakati wa kumfuata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pogba hatocheza, ana kadi nyekundu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Martial
Ronaldo
Nani
De Gea
Valencia
Shaw

kwa kusindikiza comment yako
 
Leo hii kabla jimbi hajawika mashetani wekundu watakuwa wameaga mashindano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu natanguliza pole kwenye msiba unaotarajiwa kutokea leo na hapo jumapili (marehemu atakufa mara mbili)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…