Martial ni mzuri sana Mchezo ukiwa wa wazi zaidi, kitu Ambacho Newcastle kipindi cha Kwanza hawakuruhusu Mchezo kuwa wa Kasi na wa wazi.
Walichofanya walikaba na kuzuia njia zote Ndio mana Leo kipindi cha Kwanza hukuiona Man United uliyoitegemea na ni kutokana na aina ya Mpinzani unayecheza Naye.
Pia kumbuka kipindi cha Kwanza Man United walicheza sana mpira wa upande wa kushoto, na Newcastle walimkaba sana Martial, Mashambulizi yetu yalikuwa yanatokea upande wa kushoto, it was a game plan, Newcastle walikuwa imara sana katika beki ya kati na Katika eneo la Kiungo.
Kipindi cha Pili tulibadili Mfumo na Mpira kuchezwa pande zote lakini hasa katikati baada ya Newcastle kuanza kufunguka na wao.
Martial anatakiwa kubadilika, bado anatakiwa kujituma zaidi na kucheza Mpira Kama Rashford alivyobadilika, anatakiwa kuonyesha uwezo wake, Kipaji pekeee bila juhudi na Malengo atakuwa mchezaji wa kawaida.
Match ya Leo Kwangu alikabwa zaidi na zile drible zake nyingi hazikufanikiwa hata kwa upande wa Pogba na Matic.
It was a tough game, Match Kama hizi Huwa haziwi nzuri wala kuwa na Magoli Mengi.
Tumeshuhudia zaidi ya Mara 5 Hivi Mpira ukisimama ili wachezaji kupatA matibabu, ilikuwa match ngumu Kidogo.
Kwangu kwa match za namna Hii, ni vema kuanza na Lingard kuliko Martial.
Tumpe Nafasi Martial ni mchezaji mzuri sana sana Ila anakosa focus na njaa, ameridhika mapema, anasahau kuna Balon de' or ambayo CR7 na Mess wameichukua Mara 5 kila mmoja.
Sent using
Jamii Forums mobile app