Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ukweli ni kwamba football imebadilika sana nje ya uwanja hasa baada ya soka la ulaya kuvutia wawekezaji wengi kutoka Asia na marekani hivi sasa kila team inajiimarisha ili izalishe mapato makubwa kupitia.
1 matangazo.
2 mapato ya uwanjani
3 mauzo ya wachezaji
Nk
Ni ngumu sana club kama Tottenham ambayo imesheheni vipaji vingi kuweza kumwachia mchezaji wake bila kuutunisha mfuko wa Daniel Levy.

Kuingia kwa middlemen kwenye soko la wachezaji kumeweza kuchangia sana kupandisha viwango vya bei na mishahara ya wachezaji, kwa kifupi ni kwamba bargaining power ya hizo pande mbili kwa sasa ni kama sawa hivi.

Vilabu vikubwa kupunguza uwekezaji kwenye academy au kutokuwapa vipaumbele vijana vinavyowazalisha kwenye academy zake kumeongeza demand ya readymade players na kufanya bei ipande maradufu.

Mathalani hivi sasa kuna vilabu zaidi ya 17 ambavyo havizalishi vipaji vikubwa sana lakini ndiyo vinavyotegea sana readymade players na ndiyo zenye ukwasi mkubwa sana hivyo hali kama hii competition ni kubwa sana.
Mfano uingereza man united, Chelsea, Man city , Arsenal, Liverpool vyote hivi vinategemea ready made players soko lazima liwe ghali.
 
Ila mkuu naomba nikukumbushe kuwa, kwa Uingereza United ndio timu yenye academy productive kuliko nyingine
 
Ila mkuu naomba nikukumbushe kuwa, kwa Uingereza United ndio timu yenye academy productive kuliko nyingine
Ni sahihi kabisa lakini kwa hivi karibuni imechomoa wachezaji wachache lakini wengi wamekwama kufikia top level.
List ni ndefu kidogo.
1 januzaj
2 bithwick Jackson
3 Timothy fosu mensah
4 Rashford
5 Keane
6 Powell
7 Gibson
8 James Wilson
9 Lingard
10 Pereira
11Evans
Etc
Unaweza ukaona list hiyo yote walioko kwenye top level ni wawili tu lakini nao bado hawajawa dependable players kama kizazi cha Ferguson cha 1992
 
Mkuu tukiangalia hizo timu ulizo taja. Mfano Barca au Madrid au Bayern ni kati ya timu ambazo wanaangalia zaidi Ku tawala sio tu ligi za ndani ila ulaya Kwa ujumla wake. Presha yake ni tofauti na aliyo Kuwa anapewa Fergie baada ya kutawala ligi ya uingereza. Ndio maana sio ajabu kusikia wajerumani wanamuona Pep kama failure Kwa alicho kipata Beyern wakati amewapa makombe ya ligi misimu yote pale. Au Barca wakachukua kombe la ligi halafu kocha akafukuzwa the same to Madrid. Au kipindi kile Inter wanamchukua Mou walikuwa wamebeba kombe la kwao Kwa miaka mitatu mfululizo chini ya Mancin ila target yao ilikuwa ni UEFA.


Kwa hiyo its either tulikuwa na Malengo ya kutawala ligi ya EPL( kama ni hivyo tulifanikiwa) auu alivumiliwa na management kuhusu michuano ya nje.

Tukirudi kwenye kwanini Fergie alikaa muda mrefu kwetu?
Kwanza sababu zinazo weza mfanya kocha akae muda mrefu au mfupi ni Matokeo anayo pata, uhusiano wake na management ya juu pamoja Na Malengo ya club(huu mtazamo wangu)
Naweza kusema sababu kubwa ya Fergie kudumu, ni timu yetu walikuwa wana mvumilia tunapo Kuwa tupo down Kwa kuamini tutapanda tena. Ila timu kubwa nyingi hicho kitu hazina.
 
Kuna Pogba, Lingard, Rashford, Drinkwater pia
 
Mkuu mbona nimezitaja hapo mwishoni. ( kama kuna niliyo isahau hapo nikumbushe)
Statistics ninazoziongelea, ni mfano unaposema United alipigwa na Barca Fainali, unaacha kutaja kuanzia hatua ya makundi vigogo aliowapiga mpaka akafika hapo fainali.

Vivyo hivyo na kwenye hatua za nusu alizofika, unaacha kutaja vigogo aliowachapa mpaka akafika nusu fainali na kutolewa
 
Hii ni kuanzia 2001/2002 hadi msimu wa mwisho wa Fergie. Msimu ambao haupo hapo Basi tuliishia Makundi. Ukiangalia hapo Kwa miaka kumi tulifanikiwa kumtoa juve na Barca pekee(ma giant walio Kuwa kwenye ubora). Ac Milan tuliye mfunga sihitaji kumzungumzia alikuwa kwenye hali gani.
 
Kiukweli sijazielewa vizuri hizo screen shot zako, ila kama AC Milan aliyefungwa 7 unaamini alikuwa na hali mbaya (wakati alifika hapo kwa kutoa vichapo kwa timu nyingine), mbona Deportivo humtambui kama Giant maana kwa wakati huo alikuwa hakamatiki?
 
Amemsajili sane akiwa mdogo akaona kipaji chake akampa nafasi akamwamini hadi sasa dogo ni miongoni mwa wachezaji tegemeo Wa city. Amekuwa akimpa vidakika kadhaa Phil Phoden ambaye ni kinda. Mfano sisi Angel Gomes au Tahit Chong wangekuwa wanapewa hata vidakika vya kudanganyishia
 
Si lazima wawe ma superstar, Bali wawe nguvu kazi za kuaminika kwa timu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…