Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Yaani mashabiki wa namna hii ni tatizo sana mkuu

Wazee wa kudandia treni kwa mbele,

Mashabiki real kwa hizo timu upcoming ni wa kuhesabika
Yes hizi timu zinamashabiki wa msimu. Walijiunga baada ya mafanikio.

Mwaka 84 mzee Hughes akiwa mchezaji wa utd kocha mzee Artickson. wengine timu hawajui zinatokea wapi
 
Kwani main target za Mou msimu Wa kwanza walikuwa ni kina nani na akawakosa? Hivi kocha kununua wachezaji Wa Β£30 mil inamaanisha kwamba ndio hela alopewa atafute wachezaji Wa kiasi hicho? Mi nijuavyo lindelof na Bailly ni machaguo ambayo Mwl aliamini ni sahihi. Labda beki Wa pembeni na penyewe ilikuwa sahihi kumnyima kwa sababu shaw alikuwepo na kilichoonekana ilikuwa ni kama kocha ana chuki binafsi kwa mchezaji ilihali bodi ya timu iliamini mchezaji ana potential. Beki 2 haikuwa tageti sana ya Mwl. Kuhusu winga ni vilevile tu Mwl alionyesha kutompenda martial hata kufikia kutaka dogo aondoke wakati wenye timu waliamini dogo ana kitu kikubwa ndani yake. Shida inakuja kwamba hata wachezaji alonunua kwa mapendekezo yake wanashindwa kufanya kilichotarajiwa na Mwl na pia wenye timu. Hata Mimi nisingetoa hela kirahisi rahisi
 
Madrid ana makombe 14 ya ulaya manne kwatwaa juz sasa hayo kumi yapo mfukoni kwako? Chelsea tulia wewe huna cha kusema lazima povu la wivu likutoke
Mkuu kati ya mim na www nani anapaswa kuwa na wivu, tangu Web astaafu hauna Epl mimi nimeshabeba kadhaa... Hata hii leo mim niko juu yako ki msimamo.... Timu kubwa nayo kukaa miaka yote hiyo bila kombe tena mnawachezaji bkra kabisa kuwahi kutokea kama akina Pogba πŸ˜‚ LukakuπŸ˜‚ LingardπŸ˜‚ na Rashford πŸ˜‚ ni aibu... Mwisho wa siku ukubwa unaishia kwenye makaratasi
 
Mkuu mimi sio timu kubwa, aibu yako wew timu kubwa kwamba tangu Web astaafu ni vitoto tu vinachujua mbele yako πŸ˜‚
hizi comment zako sisi wengine zinaendelea kutuletea maumivu brother, hebu jaribu kutupumzisha japo kwa nusu siku.
timu ndogo zinachukua makombe ila sisi wakubwa tunaimba historia.
hahahahaaaaa ila muna haki wapinzani wetu kwa nyakati hizi kutumwagia mvua ya kejeli na matusi kwa sababu hali hii tulionayo kwa miaka hii tumejitakia wenyewe.
 
Madrid walikaa miaka 6 hadi mourinho alipowapa la liga ni suala la muda na kupita vipind vibaya kwa akili yako tembo akikonda anafanana na paka unategemea siku chelsea atakuwa manchester united? Najua una maumivu kisingizio chako ni web timu inabeba club bingwa ya ulaya hadi na club world cup ngazi ya vilabu ni web? Uwe unaficha ujinga wako chelsea ulipigwa fainali moscow terry aliambiwa akose penat au web alimshika miguu anelka? Huna tofaut na vilio vya mbaazi zikikosa maua kizur na cha kupendeza nimekufumua fainali ya uefa yule refa sijui alikuwa ni web?
 
Watu wepesi sana kusahau
Kuna baadhi ya makocha ndo wanauwa viwango vya wachezaji kama yule Goundoz wa asenal na Herela au matic ukilinganisha hawa wa Man u ni wazuli zaidi lakin et hawana hadh
 
Mkuu nimekuelewa sana lakini kuna maeneo inabidi tuweke sawa

Ni kweli Lindelof na Bailly walikuwa ni machaguo ya Mourinho, lakini si machaguo ya kwanza

Mou amekuwa akieleza kila msimu unapoelekea kuisha kuwa kazi yake ni kutoa list of names katika namba anayotaka kununua, kwa hiyo hapa huwa anaweka orodha hata ya wachezaji 4 au 5 kwa mpangilio wa umuhimu ili Ed anunue mmoja wapo

Kwa rekodi ya Mou ya kutaka wachezaji ambao ni already proven players, tutajidanganya tukisema Lindelof na Bailly walikuwa ni machaguo ya kwanza ya Jose. Wale walikuwa ni potential zaidi, na Ed huwa anapenda potential players sababu ya resale value yao. Kwahiyo hawa walikuwa ni machaguo ya kwanza ya Ed na Glazer family kwa kuwa ilikuwa ni convenient kwao kibiashara kuwa na mchezaji ambaye unaweza kumtumia miaka 8, na bado ukaja ukamuuza kwa Β£ 40 mil.

Ukirudi kwa beki za pembeni, Mou alikiwa anajitaji sana beki wa pande zote 2, wa kulia na kushoto. Kulia hakuweka mkazo sana kutokana na dhana ya kuweka kipaumbele, ambapo aliona kushoto ni tatizo zaidi. KWENYE HILI JOSE ALIKOSEA, HUWA SI PATIENT KWA WACHEZAJI VIJANA WANAOPOTOKA. Hii imejitokeza hata kwa Martial ambaye alitaka kuondoka kwa sehemu hiyo ilisababishwa na JosΓ© lakini na yeye Martial alikiwa ana shida kwenye attitude yake.

Kuhusu kununua baadhi ya wachezaji na kuto click kama kocha alivyotazamia, Jose hatakuwa wa 1 wala wa mwisho. Nimetoa mfano jana kwa Guadiola wa Claudio Bravo, pia kuna Mhisipania mmoja alikuja msimu 1 tu City kisha akarejea Hispania (ukihitaji jina nitakutafutia). Fergie aliwanunua akina Djemba Djemba, Bebe, Oberten n.k ambao wakaishia kuwa ma flop

Mil. 30 ni ndogo sana kwa beki wa kati kwenye post Ronaldo, Bale, Pogba and Neymar Market, unless uwe unataka uwe timu ya mid table kwenye msimamo wa ligi ya Premier kama akina Everton
 
Watu wakitoka kuvuta bange wanasema mou anafundisha kukaba wakati team haizuii wala haishambulii
sasa mkuu hata wew ukiukizws Mou anafundisha nini utajibuje, mana kama ni attacking ndo hayo magunia ya kina Lukaku... Kama ni kukaba ni hizo dakika karibu tatu mpira unatafutwa kwa tochi
...
 
Mkuu naona povu limekua jingi... Sasa kama mnajua ni kipindi cha mpito kelela na majigambo ya nini.. Mlimsajiki Pogba kwa usajili wa kuvunja rekod hapakutosha humu πŸ˜‚ baadae akaja Lukaku game kama tatu za kwanza akawa anafunga basi ndo alikua striker bora duniani... πŸ˜‚ Mashabiki wa Man u mna taabu sana na timu yenu KUBWA bila Web hamna timu ombeni arudi ndo pona pona yenu... Zike enzi za Rooney kufunga goli na Web anashangilia zilisha pita.. Sasa pambaneni na sura halisi ya Man u πŸ˜‚... Mwaka unaenda wa nane huu mwisho tutagikia umri wa mtu mzima πŸ˜‚
 
Kuna kipindi walianza kusema lingard ni bora kuliko messi
 
Aliekupiga uefa ni nani? Refa alikuwa web mi sisomi post zako naangalia juu ulivyoanza kisha najua idea yako nzima
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tatizo mna kelele sana.. Yani mkishinda game moja huwa hapatoshi humu na timu yenu kubwa πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…