Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hahahahaha Pogba bana kama umekatazwa kuongea na Simply ameongea ina maana anapinga alichoambiwa na uongozi wa timu
 

I am who I am
I do What I waana do
Endelea Kuattack, But at the End You'll achieve nothing... Coz I'm not gonna change for your request...
If I wanna change, I'll change kwa My own free will...
I'm delightful kwamba umeconfess kuwa unaniattack intentionally na si accidentally..

Endelea Kuattack bro ukidhani unagain something wakati ukweli Ni kwamba unawatse muda wako tu.
 
Sasa mbona ameongea hahahaa
Pogba na Maurinho wote wasepe tu

Aondoke Pogba????????????
Mkuu Mimi unaweza sema siujui Mpira lakini Kwenye timu siwi na Mchezaji Kama Pogba nikasema aondoke...
Kipaji cha Pogba kimefichwa na siasa za Mourinho! Subiri aondoke Mourinho aje Kocha Mwenye siasa rafiki na Wachezaji uone Mziki Wa Hugo Pogba unayesema aondoke.
 
Umenena fact mkuu jamaa anakipaji sana yani....vitu vidogo vikibadilika ndani ya club atakuwa moto
 
tatizo la viungo wa jana matic slow na fellain slow sasa tutashambuliaje vizuri bila kuwa na kasi. Hawa watu kucheza pamoja ni kama kuzubaisha timu tu

Hata imi nilishindwa kumuelewa Mourinho,tunacheza nyumbani kutafuta ushindi unaanza two holding halafu wote wapo slow. basi anagalau japo kipindi cha pili angemtoa mmojawapo kumuingia Fredy,matokeo yake tukawa tunamtegemea Fellain mipira ya kross ili afunge da.
 
Mkuu unapozungumzia kros unanigusa sana yani sisi hatunaga mbinu zaidi ya kufunga kwa kros....yani plan A tukizidiwa tumategemea vichwa.....ni plan nzuri ila ingebidi tuwe tunaupiga mwingi timu pinzani ichanganyikiwe iwe rahisi kufunga hizo kros
 
Huwa namuona kocha wa buyern aliestaafu ni mjengaji wa timu sijui kwa nini bodi haimfikilii kumshawish zidane sizani mkuu mana nje ya champions lig hanna cha maana ni mzur ktk mech za mtoano mbio ndefu chenga
umesahau ya kwamba jupp heynckens ana miaka 73 ya kuzaliwa na kwa umri alionao haipendezi kuendelea kufanya kazi kwa mwaka mzima bila ya kupumzika, tunapaswa tuwe na huruma kwa mababu zetu.

kuna tofauti kubwa sana kuifundisha bayern munich inayocheza bundesliga na manchester united inayocheza ligi kuu ya uingereza. Mpira wa uingereza umevamiwa na mabepari wasiokuwa na huruma kwenye kutumia fedha zao kwa ajili ya kutafuta furaha japo kwa muda mfupi. jaribu kufikiria huku uingereza leo hii everton wanalipa pound millioni 50 kwa ajili ya richarlison wakati kule ujerumani bayern munich ndiye mwenye uwezo wa kufanya matumizi kama hayo.

majirani zetu liverpool takribani miaka 10 walitiwa ujinga na upumbavu uliokithiri kupitia vyombo vya habari vya nchini uingereza na hatimaye wakawapa kazi makocha wasiokuwa na uwezo hata wa kufundisha fyatueni fc ya chato na kilichotokezea ni mwendo wa kusajiliwa wapumbavu na wazembe kama vile dossena, krygiakos, david ngog,aquilani, andy carroll, bellamy, kolo toure, fabio borini, konchesky n.k. Tusipokuwa makini tutaivunja rekodi ya liverpool ya kuajiri makocha wa ovyo na kuendelea kutujazia wachezaji wa ovyo kama lindelof, fellaini na darmian matteo.

tulitiwa ujinga na vyombo vya habari vya uingereza na tukawapa nafasi david moyes na kaka yake luis van gaal na tukaamua kuwapotezea walimu wazuri. walipofanya vibaya vyombo vile vile vikawageuka na kuwagongelea misumari yenye uzito wa tani 7 kwenye miili yao na pia kuanza kuwawekea rekodi zao mbovu walizozivunja.
kwa jinsi wazungu wanavyopenda starehe bila ya kujali umri wao, huenda mrithi wa jose mourinho atakuwa yupo kwenye fukwe na bukta yake ya fiesta akisubiri ujumbe wa tafadhali nipigie kutoka kwa ed woodward.
swali linaloumiza kichwa muda huu
ni yupi mtu sahihi wa kurudisha heshima ya klabu ndani ya uwanja?

  • kama ni hoja mafanikio tusishau ya kuwa klabu imeshawapa nafasi ya kazi makocha wawili wenye CV nzuri.
neno ta ra fergie liwe ni ta ra mourinho
TUJISAHIHISHE ILI TUSICHEKWE TENA
 
Mkuu damushin unajua sana soka aiseh unalogic za maana, unaelezea fact na historia unahusisha, good job..... Mbona chelsea wanaupiga mwingi bhana sembuse sisi
umenipa heshima kubwa sana zinazonizidi kimo changu ila sinabudi kuzipokea kwa mikono miwili.
kupenda kwangu mpira tokea nikiwa na umri mdogo sana kumenifanya niufahamu mpira na wachezaji kama nimesomea fani hiyo, nikikwambia nina uwezo wa kumgundua mchezaji hodari na mchezaji mbovu kwa muda mchache sana unaweza kuniamini?
cha ajabu wazungu wanatumia msimu mzima kwa ajili ya kumchunguza mchezaji.

nakumbuka mechi ya kwanza ya liverpool kwenye jukwaa lao baada ya kuwafunga west ham magoli manne niliwambia mbona huyu mohammed salah pumzi yake imekata ghafla mapema yote hii na nilichojibiwa kwenye thread yao
  • mkuu muhammed salah leo amefunga goli moja halafu unasema amekata pumzi utakuwa una wazimu.
  • mwengine akanijibu bado mapema na inaonekana pressure ya kuhofia kuumia tena inamkabili
  • mwengine akanijibu tatizo la salah inaonekana anataka kukimbilia kuweka heshima aliyoiweka mwaka jana.
  • mmoja akanijibu salah amekuwa akikaa maeneo ya firmino.
uzi wa toa likes pata likes umeniathiri sana kiasi ambacho hata kama mtu atanijibu ovyo huwa namgongea like ya bure
namshukuru mungu kadri siku zinavyosogea mbele mashabiki wa liverpool wameanza kuliona tatizo la salah.
hapa ndipo nilipoanza kushabikia mpira na manchester united ikawa ndio timu ya kwanza kuiona kwenye televisheni ikipata ushindi.

hahahahahaaaa kama Arsenal wangelishinda mechi hii basi ndio ingelikuwa timu yangu, ahsante sana dwight yorke kwa kuniepushia ugonjwa wa kushabikia washika bunduki na kwenye mechi hii alifunga hatrick

unamkumbuka luke chadwick?
 

Mkuu umeandika vizuri...ila naomba nikuulize kwa muono wako umafikiri nani ambaye akipewa team pamoja na pesa ya usajili atatukwamua.
 
Ushauri kuifanya Man United iendelee kuwa big team.
  1. Mpeni Mou madaraka kama yale aliyopewa na Chelsea aunde timu inayoendana na mfumo wake. Pia awajenge wachezaji ambao watakuwa Loyal kwake kama akina John Terry, Frank Lampard, Didier Drogba, Petr Čech nk
  2. Mpeni pesa ili awanunue wachezaji anaowataka na wala sio mnampa pesa nusunusu
  3. Mpeni muda wa kutosha kama mlivyompa Ferguson
 
100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…