Hebu angalia hilo gape la uefa na ilichukua muda gani mpaka kuipata? Kama unaifahamu man u ya 2008 ni work on progress karibia miaka 6 mpaka fergie ilibidi atafute kocha msaidizi ambaye alikabidhiwa mikoba kama kocha mkuu, timu ilikuwa inafanya vibaya mno tulikuwa mpaka tunatolewa makundi uefa (refer benfica) hata ligi mourinho alitusumbua kipindi hiki. Kocha msaidizi akaleta vijana wake wanaoongea kireno kina kleberson, Anderson, Ronaldo, Nani na wengineo mpaka tunakuja kuipata man u ya 2018 tukatawala UEFA miaka 5 fainali 3 na nusu mbili kama sijakosea. fergie huyu huyu kwanini alishindwa kwa kipindi hiki? Inaonesha ukocha sio playstation kwamba unasajili na kupanga tu, ukocha una mambo mengi.
-moyes katutoa uefa katupeleka nafasi ya7 sijui 6
-lvg katurudisha uefa kisha akatutoa
-kaja mou katurudisha uefa, katupa makombe 3, tumefika knockout stage toka fergie astaafu, tumeshika nafasi ya pili ligi etc mafanikio yote hayo ndani ya miaka 2 unaanza vipi kusema kocha hafai? Unataka aje kocha mwengine kwa sasa timu irudi tena nafasi ya 7? Ndio furaha yenu hii kubadili makocha?
Hao liverpool walikuwa kama madrid na barca leo hii ni timu ya kawaida sana sababu ya kubadili makocha kila mwaka. Ngoja fukuza fukuza itokee man u na baada ya miaka 10 tuwe kama Everton ndio roho zenu zitatulia.