Kwanini useme martial ndo alikuwa mbovu,wakati hakuna mchezaji aliyecheza vizuri hata mmoja??..sipingi kuwa martial second half kaboronga..angalia rashford kafanya nini,pogba,mata wote walikuwa ovyo.
Wewe unachuki zako tu na Martial jana nani kacheza vizuri zaidi ya De gea? Wanapoteza mipira hovyo pasi hovyo, Rashford kumpa mwenzie pasi hawezi anahangaika tu na mpira wewe kwanini umuone Martial tu?.
Timu nzima mpaka kocha hawafai kuwepo manchester United kasoro De Gea tuuze wote kuanza upya sio ujinga
halafu wakiwafunga Chelsea mechi ijayo mtawashangilia na kuwapa sifa kumbukeni hakuna timu ilitengenezwa ishinde mechi zote. kufungwa pia ni moja ya kujifunza na kupata picha nini kifanyike ktk misimu ijayo.
kungekuwa na timu perfect basi tangu kuumbwa mpira ingekua yenyewe ndio inabeba makombe tu
Mi naona sana sana ni Rashford maana nimeona kuna jamaa akimquote kuwa alisema ''Now you see why we always play Lukaku'' na hapo jana nafasi ya Lukaku imechezwa na Marcus Rashford
Yeah ni kiburi na dharau alafu hajaanza leo hakuna kitu kibaya kama ku-single out mchezaji/wachezaji fulani pale timu inapopata matokeo mabaya,unadhani Utd ingeshinda angesema fulani ni bora kuliko Lukaku au angepiga kimya kwa nafasi yake sio vema kusema hawa ni mizigo na wale ndio wanabeba timu yeye ni mlezi pia.