Huyu jamaa huwa ananifurahisha sana, ni moja ya watu wanaoendeshwa kwa matukio na mihemko mno. Huwa napitia posts zake kuna kipindi alikua kwenye kila post ana mdisi Klopp hadi wakawa wanatofautiana na malafyale, alipokuja Mosdef kaweka hisia zake juu ya Klopp na FSG jamaa alifanya turnaround moja ya hatari kama si yeye aliekua anamtukana Klopp.
Kelvin msimu huu ndio unaweza ukawa ndio the best season kwake ever, kama ilivo kwa salah, kama ilivokua kwa mane last season (kuna viumbe walifikia kumfananisha na hazard), kama ilivokua kwa mahrez msimu ule wanachukua ubingwa, kuna dogo anaitwa Asensio msimu uliopita kila akigusa mpira kama sio kufunga basi ana assist, mashabiki wa madrid waka m-hype to the maximum.
Pogba kipaji chake kilishaonekana tangu mdogo anashinda Golden boy, FIFA U-17 world cup Golden boy na amekua akichukua tuzo since then wakati the best moments kwa kelvin ni kua top assist provider na kuwa kwenye pro XI 3rd team.