Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Sikatai na wala sipingi Mou kuendelea kuwa kocha wa Man United kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kibiashara, na ninapoongelea Soka la Kushambulia na kasi simaanishi soka la Asernal or Liverpool, naongea Falsafa, Barca wanacheza Sexy football na wana makombe ya kutosha.

Man United kwa kikosi cha Msimu huu haina sababu ya kujilinda au kucheza kwa kuhofia/kupack basi, tuna kikosi kizuri na kikubwa.

Tuna Kipa ambaye kwa sasa ndio Kipa namba moja duniani, mabeki wazoefu na wazuri, Viungo na washambuliaji wa uhakika, kinachotukwamisha ni Falsafa yetu tu.

Tunapack bus had kwa Benley? Tunafunga na timu ndogo, timu kama Crystal Palace nayo ni ya kuipakia bus.

Tuache wachezaji wafunguke, tushinde goli nyingi na soka liwe la uhakika hata hizi timu ndogo zitatuogopa kama ilivyokuwa enzi za SIR Alex.

Tulikuwa hatufungwi na timu za kijinga jinga au dro kama tunazopata sasa.

Mfumo wa kujilinda unazifanya hata timu ndogo kutudharau, soka lina kuwa sio la uhakika, ushindi unakuwa wa tabu au shida.

Wachezaji wanapoteza confidence na Radha ya Mpira, waone akina Martial, Mikh, Rashford n.k

Rashford alikuwa anakuja vizuri lakini mfumo unamfanya apoteze Confidence, akiwa timu ya taifa anakuwa tofauti na akiwa kwenye Club.

Martial amepoteza nafasi timu ya Taifa n.k

Enzi za SIR wachezaji wa timu yote walikuwa wanaitwa kwenye timu zao za Taifa.

Mbinu, Itikadi na Falsafa za Mourihno zinaenda kuua confidence na vipaji Old T tuwe wakweli.

Ni shabiki wa Man U since msimu wa 97/98.

Naijua vizuri, sawa tutachukua makombe lakini sio kwa mbinu sahihi.

Magwiji na Mafundi wa Soka wote wanamlaumu Mourihno kwa mbinu zake, tumeona kwa Scoles, Gary Nevel, Gigs na hata Sir Alex.

Ni kweli heshima yetu imerudi nje ya uwanja na si uwanjani, uwanjani bado tunasumbuliwa na timu ndogo.

Hatuna uhakika wa ushindi kwa match zaidi ya tano.

Bado tunashumbuka kupata ushindi hata kwa timu kubwa za top 4.
 
Hapo pia bodi nzima na mashabiki watamchukia sana hadi aone dunia ngumu sana kwake. Nampenda pia mshikaji ila kwa uhusiano Wa sasankati yake na kocha kwa maendeleo yake ni heri aondoke tu


Hivi Kuwa Ni wewe Ndiye Mchezaji Wa Mpira Ukotayari Kupelekwa Arsenal??
Micky hataki Kwenda Kulipwa Pesa ya Karanga.
 

Kweli kabisa nakubaliana na wewe Mourinho anaua vipaji, mfano mzuri ni Lingard. Uyu ajawai kufunga magoli 10 ndani ya msimu mmoja lakini msimu huu kafunga magoli 11.
Mourinho akiendelea hivi, Lingard atafikisha goli 20+ na kipaji chake kitakua kimekufa kabisa.
Bila ya kumsahau Martial ambae mpaka sasa kafunga magoli 10, 8 kwenye Epl.
 
Sanchez and Mkhitaryan deals are almost complete, both players will be registered to play for their new teams at the weekend. [bein sports]

BREAKING:Alexis Sanchez has agreed a four year contract with Manchester United, worth £14m. (source: Telegraph) MUFC

BREAKING: Alexis Sanchez is now a Manchester United player.[Daily Mirror]. MUFC AFC
 

Kuna MTU humu anaongea mno kuwa eti cjui tunawalipa wachezaji wetu hela ya Karanga....Anaongea hivyo kisa kitimu chake kinapata matokeo siku za karibuni...
Anasahau ya kuwa kitimu chake miaka kedekede hakina hata kikombe cha uji....
Nimemzidi kila sekta..hata uko kwenye mshahara anapochekelea nimemzidi....
Hana hata kikombe kimoja cha the really EPL.., anachojua yy ni kuja kuungana na timu nyingine zilizomuacha mbali na kuanza kuponda timu zilizomzidi...
 
nani huyo aisee ajue tu ukoo wake wote unaweza kulishwa na rashford kwa miaka 20
 
Moja ya post ya hovyo kabisa kuwahi kuisoma humu jf.

Unasifia striking force ya liverpool hivi unajua wamefunga magoli mangapi zaidi yetu?

Inakuaje timu inayopaki basi na kuua vipaji ikafunga magoli mengi zaidi ya arsenal, Chelsea, spurs na wapuuzi wengine.

Unazungumzia sexy football, hivi tangu aondoke Ferguson ni lini tulishawahi cheza mpira wa kushambulia? Au umezimisi side pass na back pass za van gaal?

Hakuna kitu kizuri kwenye mpira kama makombe mzee, mbinu za mreno ni kukupa makombe, mashabiki wa ass no wanabweka kila siku Mr bean aondoke wakati ni moja ya timu zinazocheza mpira wa kuvutia sana England.
 
na pia wana ma super star wa kutosha
martial=messi
lukaku = suarez
mata= coutinho
hapo bado kuna kina dembele sub

kocha ndio anajua acheze mfumo gani, yeye ndio kazi yake hio na sio sisi. hao mabeki wazoefu wazuri ni wapi? hebu nitajie

Tunapack bus had kwa Benley? Tunafunga na timu ndogo, timu kama Crystal Palace nayo ni ya kuipakia bus.
umedanganya na huangalii mpira kwa hii comment unaonekana unahadithiwa tu. kwanini nakwambia hivi?
-crystal palace tulimfunga 4-0 na stats ni hizi

-burnley tulitoka droo 2-2 na stats ni hizi

sasa kama sisi tumemiliki mpira asilimia 71 halafu unasema tumepaki basi sijui nikuambie nini.

kifupi sijamuona mou akipaki basi na timu ndogo, inatokea sometime timu imeshinda ana defend dakika za mwisho, ila sijawahi ona eti tunacheza na timu ndogo mwanzo mwisho kakaa nyuma,

na kwa taarifa yako kama hujawahi iona man u ya fergie ilikuwa hivyo hivyo kuna muda timu inaongoza 1-0 anamtoa striker au kiungo mshambuliaji anaingiza beki tunadefend hadi mechi inaisha. kuna mwaka vidic alikuwa mchezaji bora epl. kaangalie tulikuwa tunachezaje.

hao makocha waliokuja baada ya fergie na wakawa wanashambulia walishinda nyingi eeh.

hebu nitajie mwaka ambao martial au rashford wamecheza vizuri kuliko msimu huu, sikuelewi ujue rashford huyu huyu ambae ana goli 9 na assist 5? martial huyu huyu ambae ana goli 10 na assist 6? hawa jamaa wapo kwenye form ya maisha na wanacheza vizuri kushinda miaka yote waliyowahi cheza. ili labda uelewe Eden Hazard ana goli 6 na assist 4 msimu huu. amepitwa na wote hao wawili.

Enzi za SIR wachezaji wa timu yote walikuwa wanaitwa kwenye timu zao za Taifa.
si kweli, carrick alikuwa mara anaitwa mara haitwi, jones na smalling pia hivyo hivyo, butner, bebe, de gea wote walikuwa hawaitwi.

Mbinu, Itikadi na Falsafa za Mourihno zinaenda kuua confidence na vipaji Old T tuwe wakweli.
kama nani kipaji chake kinauliwa?

Ni shabiki wa Man U since msimu wa 97/98.

Naijua vizuri, sawa tutachukua makombe lakini sio kwa mbinu sahihi.

Magwiji na Mafundi wa Soka wote wanamlaumu Mourihno kwa mbinu zake, tumeona kwa Scoles, Gary Nevel, Gigs na hata Sir Alex.
lini sir Alex amemponda mou? link please. na hao wachezaji wa zamani uliowataja ni ma pundit, kazi yao ni kuponda wanalipwa wafanye hivyo, kama unachukua opinion za pundits na kuzifanya ni fact nakuonelea huruma. maana utahangaika kila siku.

Ni kweli heshima yetu imerudi nje ya uwanja na si uwanjani, uwanjani bado tunasumbuliwa na timu ndogo.

Hatuna uhakika wa ushindi kwa match zaidi ya tano.

Bado tunashumbuka kupata ushindi hata kwa timu kubwa za top 4.
si ndio maana tumekaa mechi zaidi ya 40 bila kufungwa OT,[/quote]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…