Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

bado sio official. na inawezekana hata asije.

city walikuwa wanatingisha kiberiti na walikuwa wanawaforce Arsenal na Agent wa sanchez kwa terms zao.

Man u kaingia kati kakubali hela anayotaka arsenal na atalipa mshahara wa sanchez anaoutaka.

tetesi za mchana huu pep, soriano na txiki wana kikao huwenda na wao wakaongeza dau na kumchukua.

maana pep na aguero haziendi na jesus ameumia wapo hali mbaya na wao.
Screenshot_20180115-184022.png

Imeripotiwa kuwa mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez amefikia makubaliano na Manchester United kwa ajili ya uhamisho wa Januari.
Sanchez atakuwa amemaliza mkataba wake Emirates Stadium ifikapo mwisho wa msimu huu na Arsenal wanaaminika kuwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile mwezi huu, hata kama ni kumuuza kwa washindani wao wa ligi.
Manchester City imekuwa timu inayopewa nafasi kwa muda mrefu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na kulikuwa na makubaliano baina yao majira ya joto kabla ya Arsenal kugeuza kibao, lakini United wameibuka kuwa mstari wa mbele kwa sasa.

Taarifa nyingi kwenye Twitter zimedai kuwa mchakato huo umeshakamilika, United wakita tayari kumlipa Sanchez £350,000 kwa wiki pamoja na adau ya uhamisho ya £30m.
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa mustakabaliwa Sanchez utafahamika ndani ya saa 48, ingawa hakuna tamko rasmi kutoka kwa klabu yoyote baina ya hizo mbili.
Sanchez alijiunga na Arsenal 2014 na amefunga mabao 80 katika mechi 165 kwa klabu hiyo.
 
Tetesi

Manchester United wako tayari kumpa kipa wa miaka 27 David de Gea mkataba mpya amboa utamweka katika klabu hiyo katika taaluma yake yote.(Mirror)
 
Ryan Giggs ametangazwa kuwa kocha wa Wales. Ongera kwake, nenda kapate uzoefu uje urudi nyumbani kuifundisha Man united
 
Tetesi

Pamoja na kutaka kumsajili Sanchez, Manchester United pia wanataka kumsajili Mesut Ozil, 29. (Sunday Mirror)


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kuacha kumsajili Antoine Griezmann, 26, kutoka Atletico Madrid mwisho wa msimu na hata Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid, ili amsajili Sanchez na kumpa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki. (Mail on Sunday)

Manchester United wamempa Alexis Sanchez hadi siku ya Ijumaa kuamua kama anataka kwenda Old Trafford au la, vinginevyo wataachana naye. (Sunday Express)
 
Tetesi

Liverpool wapo tayari kupambana na Manchester City na Manchester United katika kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 29. (Sunday Mirror)
 
Tetesi

Arsenal wako makini kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan 28, kama sehemu ya makubaliano ambayo yatamleta mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29, huko Old Trafford. (Guardian)
 
Back
Top Bottom