Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mi jana kocha wangu sikumuelewa kabisa yani madogo walifanya presing ya hali ya juu mno sikuona umuhimu wa ibra,martial na rashford kuendelea kuwepo uwanjani sema kwa kuwa kuna mech kubwa mbele ilibid tuvumilie tu
 
makombe yaliondoka na fagason....sasa hivi man u ni debe tupu
Tupo kwenye mpira mbovu ambao siku zote wanacheza vibaya nimekuuliza makombe wanachukuaje unakimbilia ferguson sasa huo mpira mbaya ni wawap?


Europa na fa nalo alikuwepo eee pale unapojilazimisha akili yako iamini kile unachokipenda
 
Habari zenu wadau wa Soka

Hivi Manchester united kutolewa kwenye mashindano kombe la ligi na timu ndogo namna hii tena wao Manchester wakiwa kama mabingwa wa tetezi. Inamaanisha Manchester imeshuka kiwango, morinyo ameishiwa mbinu au Manchester wanaikimbia Chelsea?
 
Jose Mourinho amedai kuwa Bristol City walikuwa na bahati kwa kushinda 2-1 dhidi ya Manchester United kwenye robo fainali Kombe la EFL kwenye uwanja wa Ashton Gate.
Goli la dakika za majeruhi kutoka kwa Korey Smith liliwatoa mabingwa hao watetezi kwenye michuano na kujikatia tiketi ya nusu fainali tangu kampeni za 1988-89.
Mechi hiyo ilienda muda wa ziada baada ya Zlatan Ibrahimovic kufunga goli akisawazisha goli la Joe Byran la dakika ya 51.

Walikuwa na bahati lakini walipambana sana kubahatisha," Mourinho aliwaambia waandishi. "Kila mmoja alikuwa akisubiri sisi tufunge kwa hiyo walikuwa na bahati. Tuligonga mwamba mara mbili.
"Lakini walicheza vizuri sana, walipambana kana kwamba ni mechi ya maisha yao, yawezekana ilikuwa. Siku nzuri ya soka. Timu kutoka kutoka ligi ya chini imeshinda. Siku kubwa kwao.

Kipindi cha kwanza tulikosa ustahimilivu waliokuwa nao wenzetu. Kifiziki na kiakili. Ilikuwa siku moja zaidi ofisini kwa wachezaji wangu. Siku ambayo wengine hawakupenda kuja ofisini."

Bristol City wanaungana na Chelsea, Arsenal na Manchester City nusu fainali ya michuano.
 
Ndugu unaumia sana
vibaya mno tumekuwa na timu ya uoga sana

Mou ni muongeaji sana lakini maneno yake sio dawa uwanjani

bora apatiwe giggs hii timu tuone enzi za SAF zikijirudia napenda mpira wa kushambulia na mpira wa kulazimisha matokeo positive
kiukweli mou amepambana juu ya hili lakini ameshindwa
Giggs Apewe mkoba tu
 
Sijui mnashindwa kunielewa lakini..... Hapa sipo kufurahisha mtu, hapa naongea ukweli tu na kukubali kuwa upepo umebadilika. ni Style ya uchezaji wetu ndio inawapa imani ya KUWEZA KUTUFUNGA. KUAMINI KUWA WANAWEZA, KUAMINI, KUAMINI, KUAMINI INAWEZA IKAWA KWELI AU SI KWELI... LAKINI KUAMINI, KUNA WATU WANAAMINI KUWA WAGANGA WANAWASAIDIA ILA SIKWELI BALI NDIO WANAOWATIA MATATIZONI NA PIA WANAONA MAFANIKIO AMBAYO WANAAMINI KUWA MUNGU KASHINDWA KUWAPA, KWA TIMU ZIKIJA KUCHEZA NA MU ZINAAMINI, ZINAAMINI, NASEMA TENA ZINAAMINI ZINA UWEZO WA KUCHOPOA POINT 3, ZIKIJA KUCHEZA NA MU WANAICHUKULIA KAMA TIMU NYENGINE TU KWA JINSI TUNAVOCHEZA, HATUNA TOFAUTI NA STYLE YA VIBONDE....

Lakini bado hamjanielewa
 
Morinyo kila timu iliyomfunga anadai walibahatisha,alifungwa na chelsea alidai wamebahatisha,mancity alidai wamebahatisha,jana Bristolcity nao anadai wamebahatisha ila yeye akishinda hajabahatisha.huyu mzee mbumbavu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…