Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameitoa timu yake kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu huu baada ya kukubali kipigo cha goli 2-1
United waliadhibiwa mara mbili baada ya kushindwa kuokoa mipira vizuri kwenye eneo la hatari na kupelekea magoli ya David Silva na Nicolas Otamendi huku upande wa United goli lao likifungwa na Marcus Rashford.

Baada ya ushindi huo vijana wa Guardiola sasa wapo juu kwa alama 11 dhidi ya timu inayokamata nafasi ya pili klabu ya Manchester United
City wamepoteza alama mbili tu msimu mzima, na Mourinho amekubali kuwa upande wake hauwezekani kulifikia gepu hilo ambayo sasa huwatenganisha na wapinzani wao wa ndani.

Alipoulizwa kama mbio za ubingwa zimefika tanati, Mourinho aliiambia BBC Sport: "Labda, ndiyo Manchester City ni timu nzuri sana na inahifadhiwa na bahati, na Miungu ya soka ipo nyuma yao."
City sasa imeshinda mechi 14 za Ligi Kuu mfululizo, sawa na rekodi iliyowekwa na Arsenal mwaka 2002.
Manchester United itaikaribisha Old Trafford klabu ya Bournemouth siku ya Jumatano usiku
 
Yaani Man U sasahivi wanategemea tu magoli ya kubahatisha ya Counter Attack baasi

Yaani wamekuwa mdebwedo kuliko lipuli.
tangu lini umeanza kuishabikia man city?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…