Tetesi
MAN UTD YAMTOLEA MACHO CRISTANTE
Manchester United inataka kumsajili kiungo wa Atalanta, Bryan Cristante kuwa mrithi wa Marouane Fellaini, kwa mujibu wa The Sun .
Mashetani Wekundu wapo tayari kumpoteza Fellaini na kiwango cha Cristante akicheza kwa mkopo Serie A kimemshawishi Mourinnho kuamini kuwa mchezaji huyo ni mbadala sahihi kwa Fellaini.
Atalanta wana uwezo wa kumsajili Cristante kutoka klabu yake mama Benfica kwa paundi milioni 10 mwisho wa msimu, na kisha kumuuza kiungo huyo Man United kwa paundi milioni 31.