Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

25 years ago he became a red devil
26061f56b6254c91f14de156e2fc7622.jpg
 
Roho yangu inaumia sana kuzidiwa point 8 na majirani zangu ,huku nikiwa sioni tunachofanya cha ziada pale tunapozidiwa
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu kufuatia kuondoka kwa Wayne Rooney wakati wa majira ya joto, lakini ushinda dhidi ya Burton Albion kwenye kombe la EFL ndiyo mechi pekee ya kimashindano ambayo Carrick alivaa kitambaa cha ukapteni.
Carrick alifafanua Ijumaa iliyopita kuwa kutokuwepo kwake kutokana na matatizo ya moyo , lakini nyota huyo anaendelea vizuri na Mourinho amethibitisha kuwa kuna nafasi katika klabu kwa ajili yake hata baada ya kuachana na mpira.
"Michael kama mtu ni muhimu zaidi kuliko Michael kama mchezaji. Hivyo tutampa muda wa kupumzika, kupona na kutafakari. Kwa kufanya uamuzi kama anataka kuendelea kucheza, au anataka kuacha," aliwaambia waandishi wa habari.
"Anajua kwamba kwenye ofisi yangu kuna kiti kwa ajili yake ikiwa anataka, kama anataka. Kiti chake kipo pale ofisini .Nataka hivyo, bodi nayo inataka hivyo , wamiliki wanataka hivyo.
"Lakini anataka kuwa mchezaji hadi mwisho wa msimu na sasa anajisikia vizuri kurejea kwenye mazoezi. Chaguo moja zaidi kwetu.Tunahitaji wachezaji na ikiwa Michael atataka, nitafurahi na hilo."
Carrick alijiunga na United mwaka 2006 na amecheza michezo 460 katika klabu kwenye mashindano yote.
 
SHAW MBIONI KUONDOKA UNITED KWA MKOPO


Beki wa kushoto wa Manchester United Luke Shaw anajipanga kujiunga na Newcastle kwa mkopo kwa mujibu wa habari kutoka the Daily Mirror .
 
REAL MADRID KUTOA DAU LA £80M KUMSAJILI MARTIAL


Real Madrid wapo tayari kutoa kitita cha £80 milioni kwa ajili ya kumsajli Anthony Martial msimu ujao majira ya joto, kwa mujibu wa The Mirror .
 
DORTMUND WANAMTAKA MKHITARYAN


Borussia Dortmund wanatamani kumrejesha mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan klabuni mwao, kwa mujibu wa BBC .
Mkhitaryan aliondoka Dortmund kwenda United kwa dau la paundi milioni 30 majira ya joto 2016, lakini amepata wakati mgumu kuonyesha uwezo wake Old Trafford.
Jose Mourinho amemlaumu Mkhitaryan kwa kupotea mchezoni na sasa Dortmund wanataka kumsajili tena Mwarmenia huyo.
 
Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku huenda akapigwa marufuku mechi tatu - ikiwa ni pamoja na debi ya Manchester - iwapo FA wataamua kumuadhibu mchezaji huyo wa miaka kwa 24 kwa kile kinachoonekana kuwa kama kumpiga teke beki wa Brighton Gaetan Bong. (Daily Mail)
 
Back
Top Bottom