Screenshot_2017-09-28-00-12-02.png
 
Na huko Moscow na huko moscow urusi na huko moscow cska wana bao moja cska wana bao moja na Manchester United wanaongoza kwa mabao manne anakwenda matic anatoa pande kwa lukaku aah
Nb.nimewarudisha nyuma enzi za radio watangazaji walikuwa na mbwembwe hizo hapo mshabiki ambae haipendi united angetukana sana akidhani cska wanaongoza
 

Martial alikuwa anasepa na kijiji ndo kwanza kina miaka 21 dogo akiendelea na hii fom atakuwa mtu hatari sana

Sifa ya mourinho ni kujenga timu ngumu sana hapo bado anavyosema yeye na tunashinda hivi scholes alisema apewe sajili tatu kuirudisha timu ktk hadhi yake sajili mbili tu moto wake ni mbaya GGMU.
Tulichelewa sana kumpa timu saiv usingizi wa kutosha old trafod sio sehemu salama tena ukija unapigwa tu
 
Niiongelee kidogo game yetu ya Moscow,nimekosa nafasi ya kufanya hivi kwenye game ya Everton na wale wagumu Stoke City ila nitajitahidi kwa pamoja kuziongelea hapa.

Sio Mou tu aliyeshangazwa na kasi ya Ufungaji wa Lukaku,sote tunafahamu kuhusu ubora wa Lukaku lakini sio kwa kasi hii ya kufunga magoli kila match,inabidi sasa tumwangalie kwa jicho la tatu,katika uchezaji wa Lukaku namuona El nino Ronaldo De Lima mpya kwenye zama hizi,kasi,nguvu na njaa ya kufunga kila match,Lukaku Huyu wa Man United namkumbuka De Lima wa Barcelona,yule aliyefunga zaidi ya magoli 36 msimu wake wa kwanza,akifunga tena magoli zaidi ya 34 msimu wa pili katika La liga.

Hadi sasa Jezi namba 7 haijapata mchezaji wa kuivaa,lakini ningekuwa Mou kwa Heshima na kutambua uwezo na kipaji jezi namba 7 tungempa Antony Martial.

Niliwahi kuandika huko nyuma kama tunataka timu iwe na mchazaji wa aina ya C.Ronaldo,mchezaji atakayeweza kuingia kwenye tuzo za Balon De or tuzo mbalimbali basi tuwekeze kwa Antony Martial,ona anachokifanya tangu kuanza kwa Msimu huu,amesahau matatizo yake Nje ya Uwanja,ameamua kucheza mpira,uzuri wa Matial anajitambua anajuwa ana kipaji na anataka kumuonesha Mwalimu kuwa ana uwezo na kipaji ili aendelee kumpatia nafasi,kumbuka Martial ndio kwanza ana miaka 21 tu.

Mou anatakiwa kumuini na aanze kumuandaa Martial ili kupata mrithi wa CR7 ndani ya United,alimuongelea vibaya sana msimu uliopita hadi Martial kupoteza hamu ya kucheza mpira kutokana na matatizo yake ya ndani na nje ya uwanja,naamini Mou anajutia sasa maamuzi yale,tuone assist zake na magoli anayofunga msimu huu,hana papara na hana haraka,anakupa radha halisi ya mpira,Mou hana jinsi ni lazima ampende tu.

Wenzetu Chelsea wana Hazard,Madrid wana Isco,PSG wana Mbape na sisi tuna Martial,tumuamini na kumkabidhi jezi namba 7.

Henrick Mikhtaryan,bado naendelea kusubiri kitu kutoka kwake amekomaa vilivyo ndani ya uwanja na ana uwezo ni zaidi ya Hazard,ni zaidi ya Isco,tunamdai Mikh bado hajafikia ubora wake ule aliouonyesha kwenye Ligi ya Bundasliga, tukiamini Ligi ya Bunda Sliga ni Ligi ngumu kuzidi Ligi ya EPL.

Kwa kiungo cha Matic na Pogba na Fellain,Mikhtaryan huu utakuwa msimu wake ameanza kugain ingawa ana kazi ya kufanya,anatakiwa kupunguza uzito tu na kuongeza jitihada,Mou anatakiwa kumpa majukumu binafsi kama ilivyo kwa Lukaku,yeye msimu huu atupe goli zisizozidi 15 au 20 na assist zisizopungua 20.

Marcus Rashford, Rashford ni mzuri zaidi akicheza nyuma ya Lukaku,Rashford ni namba 10 kiasili,kucheza namba 11 ni kumkomaza na kumfanya hapo baadaye kazi iwe nyepesi kwake atakapopewa nafasi ya Mshambuliaji wa kati,tumeona Shughuli yake akiwa na timu ya Taifa ambapo huchezeshwa nyuma ya mshambuliaji zaidi,tukumbuke Timu inamuandaa Rashford kuja kuwa Striker hatari sana duniani.

Matic,sitaki hata kumuelezea anajua hadi anapitiliza sasa kama ilivyo kwa De Gea,kabla ya kusajiliwa kwake Man United nilitabiri Mou kumsajili Matic,niliona Chemistry ya Mou na Matic wakiwa Chelsea,ni kosa kubwa sana kwa Chelsea kutuuzia hii machine,Huyu ndio Uti wa mgongo wa Man U kwa sasa.

Nimuongelee kidogo Hererra,game ya jana hatukuwa na Fellain,Pogba na Carric,watu muhimu katika eneo la kati kwa sasa,tumeona Performance ya Fellain this season,tumeona ujio mpya wa Pogba lakini uzoefu wa Carric ni muhimu kwenye UEFA Championship,Mou hakuwa na jinsi jana zaidi ya kumuanzisha Fundi Hererra na Matic.

Sitaki kuongelea Performance yake ya game ya jana,hamna asiyejuwa kazi ya Herera akiwa dimbani, akiwa ndani ya Jezi ya man U,naamini ana game tatu hadi 4 zaidi kabla ya Pogba na Fellain kurudi uwanjani ,tutampima kwenye game yetu na Liverpool ambayo huwezi mweka nje Hererra.

Hererra ni mzuri kwenye show ya Man to man,mwambie Salah asitembee Leo,utaiona kazi yake,Mwambie Mane Leo asitembee au Countihno,Shughuli yake sio mchezo.

Game yetu na Stoke City,haikuwa game nyepesi kwetu,Stoke ndio timu ya Kiingereza halisi,ilikuwa kipimo halisi kwetu,Stoke wabishi,wajeuri, wanapambana muda wote na hawakati tamaa mwanzo mwisho hasa wanapocheza na timu kubwa,wametupa picha halisi,wametupa kipimo cha kucheza na timu aina ya Chelsea na Man City,naamini Mou kuna vitu ameona kwenye game ile.

Niulize tu hivi Marcus Rojo na Ibra wanarudi Lini.

Nimemiss sana Huyu muhuni kutoka Argentina,ile game ya Stoke ilitakiwa Rojo awepo uwanjani.

Scholes alisema Mou apewe misimu mitatu kuifanya Man U kurudi katika hadhi yake,Man United hii inarudisha heshima yetu ilitopotea England na Ulaya,kuizua man United hii ni Nusu Final Kwenye klabu bingwa Ulaya.

Raha ya kikosi chetu ni kikosi kipana sana chenye mchanganyiko wa wachezaji wenye uwezo na talanta tofauti,ona Fellain yupo Nje ,Pogba na Carric afu bado tuna kikosi chenye uwezo wa kushinda goli 4.

Bado tuna nafasi ya kusajili January kwenye mapungufu yatakayojitokeza ingawa hadi sasa siyaoni zaidi ya kumtafuta mabadala wa Valencia.

#Go Go Man United.

Hii makala ni Heshima kwa Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa yaliyomtokea,naamini atapona na kuweza kurudi kwenye shughuli zake za kila siku,Mungu ampe nafuu na kumuangazia Nuru ya milele.
 
Back
Top Bottom