Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

MANCHESTER UNITED , REAL MADRID

Baada ya Manchester United kupata matatizo ya "Munich Air Disaster", Real Madrid ilikua timu ya kwanza kujitoa kujaribu kuisaidia kifedha na kutaka kuwatoa wachezaji wake wa tano akiwamo gwiji ALFREDO DI STEPHANO, Di Stephano alikua ndo Mchezaji bora kwa wakati huo huenda ukilinganisha na wakati huu labda wangemtoa Cristiano Ronaldo.

Kwa Miaka kadhaa kumekua na urafiki chanya baada ya tukio lile kiasi Man United waliwauzia Real Madrid wachezaji wake Wengi tu kwa Mfano beki Gabriel Heinze kwa ada ya Paundi 6M tu, Huku Liverpool walikua wanataka kutoa Zaidi ya Paundi 9M, David Beckham alipelekwa Real Madrid ilihali alishafanya mazungumzo binafsi na Barcelona, Ruud Van Nisterlooy tena aliondoka akiwa Mchezaji Muhimu kabisa ndani ya Manchester United, Javier Hernández "Chicharito" aliyepelekwa kwa Mkopo mwaka 2014 baada ya Forward line ya Real Madrid kuhitaji mtu wa kum-back up Karim Benzema,

Na ule Usajili Mkubwa wa Cristiano Ronaldo licha ya kwamba Uligharimu pesa ndefu lakini United ilimuachia kwa Roho safi kabisa

Maisha yalianza Kubadilika mara baada ya Real Madrid kumtaka Moja kati ya Makipa bora kabisa Duniani anayecheza Manchester United, I Mean David De Gea, Man United hawakutaka kumuuza na waliliweka hilo wazi, Ingawaje kulikua na Ushawishi mkubwa na pressure kubwa kutoka kwa De Gea mwenyewe lakini iko wazi kwamba Real Madrid Waliforce sana dili la De Gea.

Kuna kipindi ililipotiwa kwamba waliongea na wazazi wa De Gea waweze kumshawishi mwanao, wakamtumia hadi Mchumba wa De Gea mrembo Edurne ambae ni Mwanamuziki anayefanyia kazi zake pale kwenye Jiji la Madrid, hili lilifanikiwa kwa namna flani ingawaje De Gea alishaanza taratibu ku-develop Mapenzi yake kwa Man United tukasikie kuna kipindi alijaribu kuondoka, Ingawaje mambo yalienda sawa na Man United wakendelea kusisitiza Msimamo wao wa kutomuachia David kuna kipindi ilikaririwa kwamba Usasajili wa De Gea umekamilika Ila United wamecheelewesha kwa makusudi Fax ya De Gea kwenda Real Madrid na usajili ukashindwa kukamilika, kitu kilichoonekana ni ushindi kwa Man United na ni Loss kwa Real Madrid. Baada ya Porojo zote kupita David De Gea alisign mkataba mpya Ndani ya Manchester United, Mkataba wa Miaka 5

Maisha yakaendelea kwa Real Madrid kua kinara wa Club zote ndani ya Uwanja huku Manchester United ikipata mafanikio makubwa na kua kinara wa Club zote nje ya uwanja hasa kwenye swala la Promotion na Biashara na waka wapiku Real Madrid kama Club yenye thamani kubwa duniani kwa sasa.

Kuna kipindi Man United ilikosa mvuto kabisa hasa baada ya kuondoka kwa Sir Alex Ferguson, Hivyo ilihitaji Baadhi ya World class players kitendo kilichowafanya kugonga kwa Ndugu zao Real Madrid kuhitaji huduma ya Angel Di Maria, huyu Madrid walitaka Paundi 60M huku man u wakitaka kutoa 50M mazungumzo yalienda vizuri na Man U walikubali yaishe wakatoa Paundi 59.7M.

Baada ya miaka kadhaa Man United wakagonga hodi tena kwa Ndugu zao Real Madrid sasa hvi wakihitaji huduma ya Alvaro Morata na james Rodriguez ingawaje Jose Mourinho hakuthibitisha bid ya James. Kwa Morata Madrid walitaka Paundi 70M kwanza Man United wakatoa Paundi 60M, ikakataliwa na huku mazungumzo yakiendelea Madrid walipandisha na kutaka Paundi 79M huku man u wakiishia Paundi 65M dili ikagoma kwani Real Madrid na Frolentino Perez wao walikua na kisasi kwenye Ishu ya De Gea. Man United kuamua kumgeukia Lukaku waliemnunua kwa £75M ambayo United walikua radhi kuipa Madrid kwenye Usajili wa Morata.

Kwa James Rodriguez, Real Madrid hawakuonesha nia ya kumuuza moja kwa moja kama United walivokua wanataka na wakampeleka kwa mkopo Bayern Munich na wanauwezo wa kumnunua Paundi 35M tu ila sidhani kama hii ndo bei ambayo Man United wangeambiwa. Club ya Chelsea ilifikia makubaliano na Real Madrid kwenye usajili wa Alvaro Morata kwa £75M, bei ambayo Man United walikua radhi kulipa kabla hawajapandishiwa.

Huu ni muendelezo wa Ushindani, Ujeuri na Kukomoana unaoendelea baina ya timu hizi huenda De Gea alitaka anataka kwenda Real Madrid, Morata alikua anataka kwenda Man United ila kutokana na Ujeuri unaoendelea baina ya timu hizi Mbili Uhamisho wao Ulikwama.
 
Nijaribu kukujibu ingawa kuna mdau ameelezea vizuri kwenye post zilizopita kuhusu Pereira kwenda Valencia kwa Mkopo.

Sasa kwa nini Lingard amebaki kwenye squad ya Man United?linaweza kuwa swali zuri.

Kwanza tuelewe hawa ni wachezaji wawili wanaocheza nafasi tofauti uwanajani,Andres Pereira ni kiungo mkabaji (CM)ambapo kwa sasa kwenye timu kuna Nemanja Matic, Paul Pogba,Under Herera, Fellain na Mkongwe Carric,kwa kuangalia haraka haraka unaona kabisa Matic na Pogba wakianza kikosi cha kwanza huku Fellain akiwa plan B ya Mou as Regulator au Catalyst kwenye eneo la kati, kusaidia kushambulia na kusaidia kukaba kwa wakati mmoja na ikiwezekana kufunga huku Herera na Mkongwe Carric wakitokea Banch au wakianza kikosi cha kwanza kutokana na aina ya Match ila sioni hili likitokea kwenye EPL na UEFA mana ndiyo target yetu msimu huu kushinda yote au kushinda moja na moja kufanya vizuri.

Huku match chache zenye kuhitaji Viungo wakabaji watatu wakianza Pogba,Herera na Matic huku Caric akiwa Bench,sioni match hizi zikiwa nyingi msimu huu au sioni kama kutakuwa na haja ya kuwa na CM watatu kutokana na kikosi chetu so ni mara chache sana.

Kwa Mipango ya kocha naona tumkitumia sana Herera kwenye UEFA na makombe ya FA na Calling Cup kama ilivyoluwa kwa Ramos msimu uliopita,huku Caric akitumika sana kwenye match zenye kuhitaji wachezaji wazoefu na yeye akicheza sana kwenye FA.

Naona kikosi cha Kwanza kwenye EPL kikiendelea kuwa hichi hichi tulichoanza nacho mabadiliko machache yakiwa katika eneo la ushambuliaji.

Hivyo Mwalimu ameona kuna nafasi finyu ya kumtumia Pereira kwa sasa kwenye mipango yake na huku akitaka kumuona uwanjani akicheza na ndio mana amemtoa kwa Mkopo akiwa na matumaini ya kumrudisha Mwakani kama ataparform vizuri huko Valencia kumbuka kuwa kule kuna uwezekano akacheza kikosi cha kwanza ambacho ni kitu kizuri kwenye carrier yake, uzuri Adres Pereira ameshatuonesha kuwa ana uwezo na kumbuka uchezaji wa Pereira hauna tofauti kubwa na uchezaji wa Matic,kukaba,kushambulia na kupiga pasi za mwisho lakini anakosa uzoefu na match fitness kama Matic hivyo anahitaji kucheza match nyingi zaidi kitu ambacho asingeweza kukipata kwa sasa pale United.
Ni imani yangu kuwa Mou ana Malengo na Pereira msimu ujao mana hatutokuwa na Carric,huku Herera na Matic umri umeshaenda,tuondoe wasiwasi juu ya Pereira na tufatilie uwezo wake akiwa Valencia,nadhani sasa nitaanza kuingalia Valencia,Pereira alinionesha kitu kwenye match za maandalizi hivyo nalazimika kuendelea kumfatilia naona akija kuwa Matic mpya or Countihno kama atabadilishwa nafasi uwanjani.

Tuje kwa Jesse Lingard,kwa nafasi yake uwanjani Lingard ni kiungo mshambuliaji akitokea pembeni hasa Wing ya kushoto,kwa kuangalia kikosi chetu kwa sasa hatuna Mawinger,tunaye Ashley young na Antony Martial tu na Huyu Lingard kwa upande wa kushoto na hatuna Wing upande wa kulia lakini tukiwa na Viungo washambuliaji wengi na ndio mana unaona tukiwatumia left n right back wetu kama Mawinger wakati timu inashambulia,muangalie Valencia,°Darmian, Rojo,shaw au Blind na ndio mpira wa kisasa ambao unaachana na Mawinger wa asili wanaopiga cross na kutumia sana mabeki wa kushoto na kulia kama Mawinger huku ukijaza Viungo wengi wa ushambuliaji uwanajani hasa kuanzia namba 7,8,10 na 11.

Lingard anapata nafasi ya kubaki kwa nafasi yake kama nilivyoeleza hapo juu wapo wachache,lakini pia Lingard ana uwezo wa kukaba kiasili kama ilivyo kwa Young tofauti na Antony Martial katika nafasi wanayocheza na saa nyingine Mou akimtumia kama Mkata upepo katika eneo la Mbele kwa timu pinzani inayoshambulia kutokea pembeni na Mou ni muumini wa wachezaji wenye uwezo wa kukaba.

Na Lingard ni mchezaji wa wastani mwenye kipaji sio aina ya hawa watoto wanaotokea Ameriaka ya kusini au Africa,ni imani yangu Mou atamtumia sana kwenye mashindano ya F.A na Calling Cup kama Winger,sifa ya ziada Lingard kama ilivyo kwa Fellain ni wachezaji wenye kutekeleza kile kitu ambacho kocha huwaagiza uwanajani,hucheza kwa maelekezo ya kocha na kwa nidhamu ya Hali ya Juu.

Tuishie hapa kwa Leo ingawa naona kwenye maelezo yangu nimegusia kidogo uwepo wa viungo wengi wa ushambuliaji na wings wachache,nitakuja kuuelezea kwa nini hili afu Tuwe na mjadala wa kuwachambua makocha na vikosi vyao kwenye EPL.

Kwa uchache ndio aina ya soka lilopo kwa sasa duniani, na waasisi wa mtindo huu ni Barca ya Guadiola ambayo ilikop mtindo wa total football ya AFC Ajax ya uholanzi kwenye miaka ya 1980's na kuuongezea vionjo,Van Gaal akiwa mmoja wa waasisi wa mfumo huu pale barca ingawa hakupata nao mafanikio ila aliweka miundombinu mizuri kwenye La Masia, mtindo ambao ulikuja kusumbua sana dunia ya mpira ulipokubali na hata barca walisumbua sana kwenye Pick yao kumbuka Barc ile iliyotufunga mara 2 kwenye fainal na sisi tukiwa kwenye uwezo wa Hali ya juu na soka let u la Kiingereza,kumbuka Shughuli ya Iniesta na mwenzake ambao wao wawili tu walikuwa na uwezo wa kupiga pasi zaidi ya 600 kwa match moja,timu inakuwa haina kabisa wings na inakuwa na mshambuliaji mmoja tu.

Guys kwa Man United ya sasa baada ya Match 10,tutakuja kuongea mengine hapa Mou anakisuka kikosi hatari sana msimu huu,Chemistry ikikubali na viungo wetu wa ushambuliaji wakiwa wepesi naiona united ikija kuwa timu tishio pale Uingereza.

Shukrani.
Scofield.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa Mkuu, ila Pereira km sijakosea sio mkabaji per sei ila anacheza sehemu nyingi..mfano msimu uliopita alikuwa Granada kwa mkopo na alicheza km winger na alikimbiza vizuri sana...na sshv amepewa no 11 na Valencia i hope atakuwa anacheza kwny right position yake..

Ugiligili
 
Najaribu kuwaza tuu Kwa saut ivi mou hawez kuja kutuacha kama alivyozoea akibeba vikombe anasepa? Anaweza kuwa Wa kudumu kama farg

Sent using Jamii Forums mobile app

alisema anapenda kukaa miaka 15 zaidi hata usajili wake sio wa vipindi vifupi wengi kawachukua chini ya miaka 24 ukiacha matic na mkhitaryan + zlatan wakat hapo kuna pereirra,tuanzebe,angel gomez,mensah na mctominay katika hizo nafasi ni vijana wanaoendelezwa na Jose Mourinho.
 
Yeah sure pale EPL nawaona Liverpool tu ndio watakaoambulia angalau sare hii round ya kwanza.

Na totenham kidogo ndio watakaotusumbua angalau kuambulia sare na sio kuondoka na Point,ila hawa wengine sioni atakayetoka salama.

Na kadri muda unavyooenda Mou anakwambia ndio anavyozidi kuona makali ya wachezaji wake.

Now tunatafuta Match Fitness na Chemistry ya wachezaji wetu,baada ya Match kumi moto utakuwa sio wa kusogelewa.

Bado natamani kuona tukifungwa na kusawazisha na hatimaye kushinda,bado natamani kuuona ule ushindi wa dakika za mwisho kama enzi za Sir.

Mou amewaambia wachezaji wake hasa washambuliaji na viungo msimu hataki Pressure,ni kumaliza mchezo ndani ya dakika 30 za mchezo kipindi cha kwanza,ili kutoa nafasi kwa timu kurelax na sisi mashabiki kuendelea kuagiza vinywaji bardi kwa raha na wengine kuendelea kununua Popcorn au kusoma Mwanasport.

Mabeki wameambiwa wahakikishe De Gea anakuwa likizo ndani ya mchezo,amefanya kazi kubwa sana misimu mitatu iliyopita now anatakiwa kupumzika akiwa uwanjani ikiwezekana awe ananingia na simu au magazeti aendelee kuperuzi kuhusu yanayoendelea duniani hasa ya kuapishwa kwa wabunge wa CUF,watengeneze ukuta kuuzidi ule wa Rio na Nemanja.

Pale kati,Matic ameomba pale aachiwe yeye,Pogba ametuhakikishia furaha na nadhani tumeanza muona Pogba wa Juve (New Scolse),yale magoli ya Nje ya 18 yalikuwa adimu tangu aondoke CR7 now sasa tutaanza kuyaona.

Yale magoli ya ajabu ajabu ya Dimitri berbetov soon Ibra ataendelea kutukumbusha.

Rashford sitaki hata kumuongelewa alichowafanya jana Slovakia sio mchezo naona Mou ataanza kufikiria kumpanga kati kama namba 10 na Mikh kurudi namba 7 tuone pasi za mwisho za kideo,mana sio attack zake.

Bado Form kwa Mikh na Matta hawa wakiwa on fire basi hamna haja ya kumuangalia Isco na Assecio mana ni wachanga kwa hawa mafundi,Mkubwa Fella Leo simzungumzii kabisa namuacha apumzike mana hata sijui ile namba anayocheza pale ni ngapi lakini ndio hivyo ibaki kuwa kiungo Holding Midfield wa juu.

Banch sitaki kuligusa mana Match ijayo tutaanza muona Ibra akiwa Banch.

Mou anatamani match zingekuwa zikichezwa kila baada ya siku mbili.

Mou anasema "We're on Fire).

[HASHTAG]#This[/HASHTAG] is our season.
##GGMOU.

Scofield.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu Bado Mapema! Oh! By The Way... Hii ni EPL na sio La Liga!! Unaweza Ukamfunga Chelsea, Liverpool, Man City, Spurs na Arsena, Lakini ukaja Ukafungwa na Swansea...
 
mkuu nimejikuta nacheka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marcus Rashford’s temperament is his biggest quality, insists Phil Neville

Phil Neville hailed Marcus Rashford as a ‘superstar’ following his match-winning performance for England against Slovakia and says the striker’s temparement is his biggest quality.

Rashford was at fault for Slovakia’s opening goal but he assisted Eric Dier to level the match and scored the winner in the second half.

And Neville believes Mourinho has got a ‘gem’ on his hands with Rashford because the striker has the right mentality to reach the top.

Neville names Rashford's biggest quality after match-winning England performance
Rashford bagged his second England goal against Slovakia
‘His biggest quality is his temperament,’ Neville told BBC 5Live.

‘He never looks flustered, he can miss a chance and never looks flustered.

‘He’s improving every time I see him. He’s getting stronger, he’s getting fitter and I just think we’ve got an absolute gem on our hands.
Rashford burst onto the scene in the final months of Louis van Gaal’s reign at Old Trafford and has emerged as a crucial figure under Mourinho at the Theatre of Dreams.

The teenager’s rapid rise to fame certainly could have gone to his head but Neville says Rashford remains down to earth.

‘He’s got brilliant technique and the best thing about him is he’s got his feet on the ground.

‘He goes and watches his mates play on a Sunday, goes out on the streets playing football with his mates.

‘He doesn’t really post things on Instagram or Twitter that you think ‘he’s getting carried away things’

‘I just think if you’re managing Marcus Rashford at the moment, you’ve got a little superstar.
 
Huyu Neville ni genius wa uchambuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FB_IMG_1504626098593.jpg
 
Back
Top Bottom