Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakuu Huu Usajili Wa Zlatan Una Manufaa Kwetu? Kuna Wataalamu Wetu Wachanga Wanaweza Kupoteza Namba Wasiwasi Wangu Kwa Timu Yetu Nilikuwa Naona Tupate Winga Mmoja Mzoefu Mwenye Mbio Ngoja Tuone Ila Sina Imani Nae Hata Kidogo.
Hamna mchezaji pale, na kama mou atamtegemea kama msimu uliopita tutegemee maumivu mengine kwa kua na striker butu, tutegemee tene droo nyingi za 1:1, 0:0, sijui kwanini mou anamg'ang'ania
 
Hamna mchezaji pale, na kama mou atamtegemea kama msimu uliopita tutegemee maumivu mengine kwa kua na striker butu, tutegemee tene droo nyingi za 1:1, 0:0, sijui kwanini mou anamg'ang'ania
Rotation lazima iwepo kwenye kikosi msimu uliopita ndo kitu kilichotuponza mimi naona sio mbaya Cadabra kurudi OT.
 
24556bd937b8ec5b5156569549c76091.jpg
tukutane 16 bora
 
Wakuu Mimi nataka niongelee swala la Zlatan

Uwepo wa Zlatan ni muhimu sana kama ilivyo kwa uwepo wa fellain pale man utd.Washabiki wengi wanaponda sana kuhusu Zlatan kurudi man utd,lakini mourinho anajua anachokifanya.

Mpira ni mahesabu,na Mourinho anajua mahesabu ya mpira.Kuna hawa wachezaji wafuatao ambao huwa na special kesi pale Man utd...[HASHTAG]#Darmian[/HASHTAG]...[HASHTAG]#Lingard[/HASHTAG]....na [HASHTAG]#Fellain[/HASHTAG].Hawa uwa mashabiki wengi awawaelewi lakini nyuma ya pazia mourinho anajua kwanini hataki waondoke.

Mfano mdogo Darmian,atakaa bench sana tuu lakini big match unamuona uyo...msimu uliopita kacheza big match zote.Mourinho anawachezaji wa aina tofauti tofauti ukilinganisha na wapinzani wake,kuna wachezaji wengine unaona hawafai kuendelea kuwepo pale man utd lakini wanakitu adimu ambacho kinawafanya waendelee kuwepo pale.

Ferguson alichukua Uefa na mwaka uliofata aliingia tena fainali uku akiwa hana majina makubwa sana.Hii ilitokana na kuwa na wachezaji tofauti tofauti...mfano Park ji Sung atasugua wee lakini big match ndani.

Sasa basi, Zlatan anakitu cha pekee ambacho Lukaku hana...Rashford hana wala Martial...Usitegemee Zlatan kucheza Dk nyingi kama msimu uliopita.Mourinho atamtumia Zlatan kwa mechi sahihi ,ataingia uwanjani kwa wakati sahihi na atakuwa anaenda kufanya kitu kitakachokuwa kinawashinda Lukaku na Rashford kufanya.

Ukiiangalia timu ya Mourinho,ni timu ambayo inawachezaji wenye vipaji tofauti tofauti. Nafaida ya kuwa na kikosi kama hicho ni kuwa na plan A,B mpaka C
 
Back
Top Bottom