Zirkzee
JF-Expert Member
- Mar 3, 2010
- 1,026
- 2,074
pichani anaonekana Thiago Alcantara akishangilia goli.Klabu bingwa la ligi kuu ya England wanaripotiwa kupeleka ofa ya paundi millioni 15 kwa ajili ya kupata saini ya kiungo wa Spain na Barcelona Thiago Alcantara.Thiago amekuwa akitumika na Barca katika harakati za kutaka kumrudisha Cesc Fabregas Nou Camp kwa kumtoa kwa mkopo au kumuuza kwa Arsenal kwa mkataba utakaokuwa na kipengele cha kuwawezesha wao(Barca) kumnunua watakapomhitaji tena, sasa amekuwa gumzo katika dirisha la usajili barani ulaya akifuatilwa na timu kama Chelsea na Bolton.
United wanamuona Alcantara kama moja ya viungo wanaoweza kuziba pengo la Paul Scholes hivyo kumfanya Sir Alex Ferguson kufungua pochi kwa ajili ya kinda huyo ambaye aliifungia timu yake ya Spain bao la ushindi katika fainali ya EURO under 21, weekend iliyopita.
Wakati huo huo taarifa za ndani kutoka katika klabu hiyo ya Mashetani Wekundu zinasema kuwa Manager wa United anatarajiwa kupeleka ofa nzuri ya paundi million 20 kwa Arsenal kwa ajili ya kiungo mfaransa Samir Nasri.
Man United ambao wamekuwa wakihusishwa na kuihitaji huduma ya Nasri tangu mchezaji huyo alipokataa kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal kutokana na masuala ya mshahara, sasa man u wanaonekana kuwa serious na kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kabla ya kuanza kwa matayarisho ya ligi ya msimu ujao.