Hawa jamaa wana mpira wa kudefence sana, hata formation wanayotumia nyuma wanabaki watano, Wanapiga mashuti ya mbali pia japo kwasasa united itajivunia umahiri wa De gea, Kwa United pia kumkosa Bailly kwenye first leg pia ni kikwazo angesaidia sana speed na mipira ya vichwa wanayo tegemea sana hawa jamaa, Rostov pia wana uwanja mbaya na hali ya hewa ambayo wameizoea inaweza kuwapa advantage pia
Kwa upande wa style Man u style wanayotumia ku attack (kumtumia Zlatan tu mbele) haitakuwa rahisi sana kuwafunga hawa jamaa atleast siku hizi Mikhi na Martial wanaingia na wanajaribu ,wakipewa uhuru kwa njia gyo inaweza kusaidia, Mata ni muhimu sana kwenye hii mechi japo Mou na akili yake anaweza kutompanga kwa kisingizio cha urefu na mipira ya juu. Uzembe mdogo mdogo wa mabeki kama Smalling unaweza kucost team.
Mwisho. Rostov sio timu ya kubeza