leo nimetimiza mwaka mmoja na siku moja tokea niwe mwanachama rasmi wa jamiiforums,ni jambo la furaha kwangu mimi kwa sababu nimejifunza na naendelea kujifunza mambo mbali mbali kupitia majukwaa tofauti na member tofauti japo kuwa si mchangiaji sana, ila bahati mbaya yule aliyekubali kunileta hapa jamiiforums yupo kwenye kipindi kigumu sana na sababu amekataa kutoa taarifa za watoto wake, naamini maxence melo atashinda pambano hili na jamiiforums itaendelea kuwepo.
Kesho tunacheza na west bromwich ni mechi ngumu ila ushindi wa man utd upo mikononi mwa jose felix mourinho, natumaini mourinho na benchi lake la ufundi watakuwa na mawazo kama yangu mimi kwa ajili ya kikosi cha kesho.ningependa kuona ule utatu mtakatifu kesho ukiendelea kucheza pamoja (michael carrick16 +pogba6 +ander 21) kwa sababu nahisi ndio ufunguo wa ushindi wa timu yetu.
pia natumai antonio valencia atarudi kwenye nafasi yake ya upande wa kulia,kiukweli uwepo wa valencia unamfanya namba saba wetu awe na uhuru uwanjani,pia amenifanya niondokewe na stress za kuuzwa kwa rafael dasilva na lvg.
naamini kesho juan mata ataendelea kucheza huku tukiendelea kuomba mkhityaran awe fiti.
moja kati ya tatizo nililoligundua kwa timu yetu ni upande wa kushoto,tokea waondoke watu kama patrice evra,ryan giggs,luis nani pamoja na ji sung park (mwanadamu pekee mwenye mapafu matatu) hatujapata warithi wao na kadri siku zinavyokwenda napoteza matumaini kwa antonio martial nahisi kijana anapotea kimpira,pia tunakosa mlinzi hodari wa kushoto kwa sababu mourinho hamuamini luke shaw.
tunahitaji kiungo wa pembeni mwenye uwezo wa kufunga magoli angalau 15 kwa msimu mmoja najua duniani viungo kama hawa wamepungua sana ila kwa nguvu ya united chini ya mtendaji mkuu ed woodward na mourinho tunao uwezo wa kumsajili yeyote yule aliye tayari kucheza "THEATRE OF DREAMS" zile enzi za sir alex ferguson na david gill zimerudi tena na natumai wanaweza kutuma ofa kwa
antonio griezmann
aubameyang pierre
marco reus japo kuwa ana record mbaya ya majeruhi
gareth bale
dyabala
icardi mauro
pia umefika wakati baadhi ya wachezaji waondoke kwa sababu hawaendani na timu yetu tena kwa mtazamo wangu jose anapaswa kuwapiga bei
ashley young
fellaini
depay
schneiderlin
chris smalling:
najua wengi mutapinga ila jamaa ni mzigo hana hata ordinary diploma ya ulinzi,tukumbuke team yetu wamepita wanadamu wabishi kama vidic15, ferdinand5,jaap stam6,steve bruce,pallister. mimi namfananisha smalling na mlinzi wa zamani wa arsenal alikuwa anaitwa pascal cygan kiukweli nilikuwa nafurahi sana nikimuona uwanjani akicheza pamoja na kolo toure au felipe senderos kwa sababu nilikuwa na uhakika ruud van nistelrooy atafunga goli tu.
pia ningependa kumuona mourinho akipuuza tetesi za kuwasajili wachezaji wa kiingereza kwa sababu MUNGU kawanyima waingereza wote
pass 3 za B ukimuondoa Paul scholes, leighton baines na wilshere
ball skills, ball control, ball balance.
pia kama club inataka wachezaji wa kiingereza wafanikiwe basi wale reserve team kama will keane,wilson wawapeleke kwa mkopo kwenye ligi ya hispania kwa sababu wachezaji wote wa la liga wana B 3.
natumaini mechi ya arsenal na man city itaisha kwa suluhu kwa sababu ndio matokeo bora kwetu sisi kuliko hata mmoja wapo kufungwa.kwa sababu kama watatoka suluhu tutakuwa tumepunguza pointi tano kwa arsenal na man city ndani ya wiki mbili.
[HASHTAG]#glory[/HASHTAG] man utd
[HASHTAG]#jose[/HASHTAG] turudishie heshima yetu
[HASHTAG]#tulipoteza[/HASHTAG] mapambano ila hatukupoteza vita
[HASHTAG]#natumaini[/HASHTAG] maxence melo atakuwa huru
[HASHTAG]#natumai[/HASHTAG] ben sanane atakuwa hai