Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kumbe fella ananyambulika kama iniesta...basi city anakaa hakuna sare
 
Mambo matano muhimu.

1. Rooney kiwango kimeshuka sana,hata kuitwa timu ya taifa ni moja ya maajabu katika soka.Pass yake iliizaa goli lakini hiyo pekee yake haitoshi kumbakiza katika kikosi cha kwanza.Nadhani Rooney angeitendea haki jezi namba 10 labda angestaafuu timu ya taifa ili kujipa muda zaidi wa mapumziko na pengine kutasaidia kuinua kiwango chake hasa tukizingatia umri umeanza kumtupa mkono.

2. Marcus Rashford anastahili dakika nyingi uwanja kuliko bench,Kwanza ana uwezo mkubwa wa kufunga,pia ana uwezo mkubwa wa kuwatoka wachezaji wa timu pinzani.Tusisahau kijana bado kinda sana ana miaka 18 tu lakini vitu vyake si haba.

3. Matatizo ya ndoa yake kinda mwinge Anthony Martial yamechangia kupunguza makali yake ndani ya uwanja.Ni vyema Martial akatatua matatizo yake ya ndoa pengine anaweza kurejea katika hali ya kawaida kimchezo.

4. Mourihno kasajili wachezaji wanne kati yao wote wako vizuri nashindwa kusema yupi bora zaidi ya mwingine,Mlinzi Eric ni balaa fedha aliyonunuliwa ni ndogo ukilinganisha na thamani yake uwanjani.Zlatan,Mkhitaryan & Pogba wote wamecheza vizuri na viwango vyao vipo juu kweli kweli.Nikiambiwa ni chague mmoja hakika nitapata taabu kweli kweli labda Eric sijui Mikhitaryan duh hapana wote wako vizuri.

5. De Gea amekuwa mchezaji bora miaka 3 mfululizo hakika msimu huu hana chake kabisa mchezaji bora anaweza kuwa Eric,Rashford,Mikhitaryan au Zlatan.

Mwisho nimelipia Dstv mpaka mwakani mwezi wa pili,hakika nitaongeza hadi mwezi wa May bila kinyongo chochote.

Wasalamu Ngongo safarini Ngorongoro.
 
Martial ananipa wasiwasi pia hvyo aanzie bench.

Nachoona Rooney pamoja na kuchoka kwake acheze anapocheza Martial then Micky acheze katikati alipo Rooney. Aisee itakuwa bonge ya combination. Nani anabisha?
 
Umemaliza mkuu.
 
aanze ANDER HELELA kiukweli FELLAIN ni mzito hajui kutoa pass za haraka kwenye kushambulia ila anajua kukaba tu
 


mkuu fanyia marekebisho picha ya kikosi ingozea na ngao ya jamii hapo.
 
game ya leo itakua game ya mwisho ya fundi bastian akiwa na timu yake ya taifa
[HASHTAG]#simplylegend[/HASHTAG]
 
Homa za deadline hzo, afu apo K. Navas ashakatiwa tiketi ya ndege aje Manchester huku machozi yanamtiririkaa aiseee...

Hapa hua nampongeza sana van gaal kwa hii dili ya de gea kwa kutuma document feki
Noma man, nakumbuka hyo siku naenda kulala najua kabisa de gea ni mchezaji wa madrid, ile nashtuka night flani hivi kuja kuambiwa dili limebuma hahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…