NIMEWAZAAA NIKAGUNDUA.
Tatizo lililopo Man Utd halitaisha kirahisi sababu ni mambo mengi yaliyochangia na yanachangia timu kufanya vile.
Mimi sio mkuubwa kiumri na Manchester sijaanza kuiangalia zamaaani.
Ila kuna vitu nimevijua pale.
Ferguson alipata mafanikio Manchester sio kwa kutumia dawa.
Ila aliwajenga wachezaji kuwa na uchungu na team na kuwa na Morali.
Ndio maana aliweza kuchukua ubingwa akiwa na kina Cleverly, Welbeck na Macheda .
Ilikuwa ukikosea anainuka anakuita,anakwambia ulipokosea,anakuelekeza na unarudi uwanjani.
Kingine ni kwamba akina Giggs na Scholes walikuwa ni Manchester kwa maana kwamba wao tangu wadogo wapo United na walikiwa kweli wanaipenda team.
Walikuwa na feelings ambazo tunazipata mashabiki kama timu ikifungwa.
Walicheza jihadi kwa uwezo wao na uleeee aliowaongeza Ferguson(Spirit).
Mambo yapo tofauti leo.
VAN GAAL.
Yeye huyu ukikosea anakufukuza aisee.
Nakumbuka barua ya Hernandez ya Kwanini aliondoka.
Tena baada ya kukosa penalty.
Barua ya Rafael.
Very sad.
Martial analazimishwa kucheza Winger na Alikuwa na Winger mwenye uwezo(Di Maria) na akamuuza.
Anatolewa Rafael ili Young na Jackson wacheze Full Back.
Anafanya mambo ambayo hata mimi au Wewe unaesoma hii post usingeyafanya kama ungekuwa ndio kocha wa Manchester United leo.
Unawaondoa kina Patrice,Nemanja.
It's okey,uwezo wao ulionekana kupungua lakini wao wangeweza kuwahamasisha waliopo.
Kocha hata akija Mourinho au Amina Pep.
Still shida itakuepo sababu wachezaji waliokuwa na uchungu na team washaondoka.
Kabaki Carrick na Bro Rooney.
Sipondi ila ukweli ni kwamba team inapofungwa kuna mmoja anaumia kama wanavyoumia mashabiki na mwingine anaumia kama aibu tuu.
Uchungu anaoupata Mpira njia Depay,Blind na Bastian ni tofauti na anavyoumia Rooney.
Kamtoa Hernandez ambae alishapikwa akaiva.
Amefikia kwenye Piki ndio anaonekana galasa.
NI SAWA NA UMEPANDA MTI WA MATUNDA NA KUUMWAGILIA KWA MUDA MREFU AF MATUNDA YAMETOKA,YANAANZA KUKOMAA WE UNAUKATA UUFANYE KUNI.
Kwanini still yupo hadi leo mimi nawewe hatujui.
Inawezekana terms za mkataba aliosaini ndio zinamfanya aendelee kuwepo ambazo naamini kipengele kimojawapo kilikuwa ni kuipeleka team Champions league.
Alifanikiwa kusema ukweli ila NAHISI KAMA KAIPELEKA NA ANAITOA MAANA MMMH.
Ukimuuliza mtu ni team IPI inawachezaji wazuri Kati ya Man Utd na Leicester City directly utajibiwa ni Man Utd.
Ila Kwanini Leicester wapo vizuri msimu huu?
Unaona kabisa wale jamaa wanacheza kwa spirit na Morali .
Sasa ile team inahitaji kocha anaeweza kuwapa wachezaji Ari.
Hata Liver pia hawana wachezaji wazuri ila kocha kawapa morali.
Wakifunga anashangilia nao hadi anaangusha miwani.
Ndio mana Henderson akifunga goli anapata hamu ya kumkimbilia kocha wakashangilia pamoja.
Hapa kwetu hata kujaribu wanaogopa.
Hilo ni tatizo vibayaaaaaa.
No Morality.
No Spirit
No Motivation
No Plans
Poor substitutions.
Too many defeats.
Van Gaal Out.