Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kurudi enzi za Fergie bado mkuu. Kwanza lazima David Gill arudi FA, pili mjue jinsi ya kudefend. Msimu mzima defence yenu ipo ipo, enzi za Fergie mlikuwa mnajua kudefend hata mkiwa pungufu.

Defence yetu mbovu ila ni timu tatu tuu kwenye ligi zimefungwa magoli machache kuliko sisi

David Gill alipokuwa yupo FA alikuwa anafanya kazi zake kwa Haki... sio kama David Dein alipokuwa FA ..alikuwa anahakikisha mechi za Arsenal zinachezeshwa na marefa wanazi wa Arsenal
 
rubaman tafuta mahesabu ya timu zilizopewa penalti nyingi kwenye Premier ndio utapata ukweli wa nani anabebwa if that is what you are insuniating. Arsenane kwa mdomo ubingwa mnao. Vipi msimu ujao ubingwa kama kawaida ni wa kwenu kwa mdomo na kwenye mitandao. Experts wa failure.
 
Nipo sana tatizo mida ninayoingia hapa nyie mnakuwa hampo

Timu yako inacheza lini?
Jumatatu vs Swansea kwetu

Hawa wakaanga sumu watatuelewa tu ngoja kikosi kikae vizuri......

Dada msimu wote mnasema hivi ngoja kikae sawa kikae sawa. Matokeo ni yale yale tu. Mnaning'inilia nafasi ya 4. Mkiendelea hivi mnaweza msikwalifai group stage ya CL.
 
Kurudi enzi za Fergie bado mkuu. Kwanza lazima David Gill arudi FA, pili mjue jinsi ya kudefend. Msimu mzima defence yenu ipo ipo, enzi za Fergie mlikuwa mnajua kudefend hata mkiwa pungufu.

Ona naye huyu....same old stories...nilishaambiwa kuwa United ilishinda EPL mfululizo wakati David Dein akiwa makamu mwenyekiti wa FA, na pia akiwa pia mwakilishi wa vilabu vya soka kwenye uongozi wa FA....sasa sijui Dein (aliyekuwa mmiliki wa goons) aliibeba United?!?

Saa nyingine watu uwa mnafurahisha na kuhuzunisha sana kwa kuleta story za kwenye vijiwe vya kahawa humu...kwa utaratibu wa FA, lazima kuwe na uwakilishi wa professional clubs kwenye bodi na uongozi wa FA...sasa D. Gill ni mmoja wa wawakilishi hao, ambao uchaguliwa na timu zinazoshiriki ligi mbalimbali za Uingereza....kuna kipindi kigogo wa Rentboys alikuwa katika bodi ya FA, Benetiz akawa analalamika anaipendelea Chel$ki$

Kwa mfano sasa bosi wa FA ni Greg Dyke (jina lake halisi wala siyo masihara), aliyewahi kuwa kigogo wa United miaka ya 1990...kazi ya mwisho walikuwa bosi wa BBC...CEO ni jamaa ambaye alishawahi kuwa kwenye bodi ya Leicester City...sasa sijui kwanini Greg hasiibebe United sasa hivi, wakati yeye ni kigogo mkuu???

Chanzo: http://www.thefa.com/about-football-association/structure
 
David Gill na mamluki wengine wa United walikuwa na more influence FA kuliko D. Dean pekee yake. Majority rule au umesahau?
 
Hawa #WakaangaSumu nimeshawaambia kuwa United ilishinda mataji mengi wakati Dein ni makamu mwenyekiti wa FA, na baadaye akiwa mwakilishi wa vilabu (nafasi iliyochukuliwa na Gill)...Dein pamoja na njama zake zote, hakufua dafu!!

Yaani mtu wa Arsenal anavyosema United ilibebwa na FA wakati wa SAF, uwa nashindwa kuwaelewa, kama wanafahamu historia na mfumo wa uongozi katika FA baada ya uundwaji wa EPL...
 
David Gill na mamluki wengine wa United walikuwa na more influence FA kuliko D. Dean pekee yake. Majority rule au umesahau?

Chifu naona unaleta mzaha...unaleta stori za vijiweni hapa..

Ebu toa source inayoonyesha kuwa Gill aliinfluence decisions....

Gill na Dein hawajawahi kuwa pamoja katika FA, Dein alimwachia Gill mwaka 2006...na kabla ya hapo wakati Dein ndiyo mwakilishi wa vilabu na makamu mwenyekiti wa FA (kabla), United ilishinda EPL kwa mara 3 mfululizo..

Nimesema wawakilishi uchaguliwa na CEOs wa timu zingine...sasa itakuwa ni ajabu CEOs wa #WakaangaSumu wote wamchague mtu ambaye atawa-bully viongozi wa FA...na uwakilishi kutoka kwenye vilabu ni sehemu mojawapo tu ya structure ya uongozi wa FA...

Unavyosema majority rule unamaanisha nini katika muktadha wa uongozi wa FA?!?
 
everlenk, Nzi, DonDonald.. Ushindi wa kindondokela umewapa kelele leo. Last three weeks ilikuwa kimya sana. Hadi mnarisechi magazeti ya vijiweni. Next week ukimya utarudi hapa.
 
everlenk, Nzi, DonDonald.. Ushindi wa kindondokela umewapa kelele leo. Last three weeks ilikuwa kimya sana. Hadi mnarisechi magazeti ya vijiweni. Next week ukimya utarudi hapa.

Mkuuu ulitaka tulie ?? Sema nyie leo ndo mmeshindwa kuweka kigodoro humu....BTW pamoja na kipind kigumu tulichopita jukwaa halikuwah kulala tupu bila mwanaMu yeyote kupitia hapa .....
 
everlenk, Nzi, DonDonald.. Ushindi wa kindondokela umewapa kelele leo. Last three weeks ilikuwa kimya sana. Hadi mnarisechi magazeti ya vijiweni. Next week ukimya utarudi hapa.

Mkuu umesahau "kuna watu" wanakuwa wana deactivate account zao "timu yao pendwa ikifungwa", na watu hao sio mashabiki wa Man Utd

cc Pazi
 
Last edited by a moderator:
Mkuuu ulitaka tulie ?? Sema nyie leo ndo mmeshindwa kuweka kigodoro humu....BTW pamoja na kipind kigumu tulichopita jukwaa halikuwah kulala tupu bila mwanaMu yeyote kupitia hapa .....

Hahahahah wanawekaga kambi hapa, na kujipa matumaini hewa....

Malafyale alisema mechi za Man Utd kushinda zimeshaisha.... sijaona leo akiizungumzia kauli hiyo
 
Hahahahah wanawekaga kambi hapa, na kujipa matumaini hewa....

Malafyale alisema mechi za Man Utd kushinda zimeshaisha.... sijaona leo akiizungumzia kauli hiyo

Kesho ana kibarua kizito darajani. Uzuri tunacheza nae bila presha yoyote. Tunacheza kurinda heshima tu. Huo mpira tutakao mchezea LFC kesho mtasimulia wenyewe!
 
Kesho ana kibarua kizito darajani. Uzuri tunacheza nae bila presha yoyote. Tunacheza kurinda heshima tu. Huo mpira tutakao mchezea LFC kesho mtasimulia wenyewe!

Ameshasema "hata nyie mnajua kabisa hamuwezi kucheza na majogoo yakiwa 11 kwa 11 uwanjani", "hata nyie mnajua kabisa majogoo yanakufunga kirahisi kabisa"
 
Ameshasema "hata nyie mnajua kabisa hamuwezi kucheza na majogoo yakiwa 11 kwa 11 uwanjani", "hata nyie mnajua kabisa majogoo yanakufunga kirahisi kabisa"

Hahahaha hizo story zake hazina mashiko maana jogoo likichinjwa utasikia mi sikutizama mpira nilikua ikwiriri shamba. Malafyale kiboko aisee.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…