Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wakati mwingine Wenger huwa anatoa madai ya ajabu sana.....QUOTE]

Mkuu, Wenger anapofungwa au kutoa draw huwa anakuja na maneno yasiyoeleweka kabisaaaa, dalili flani za kuchanganyikiwa.

Arsenal alipobamizwa 3 kwa mtungi na Chelsea, alisema ati hakuona kitu chochote alichofanya Drogba uwanjani na ati vijana wake walimdhibiti vizuri!

Sasa mtu amepiga gori mbili na ameleta confusion mpaka mnajifunga gori la tatu bado Wenger haoni alichofanya mtu huyo, kama si kuchanganyikiwa ni nini?

well its true! na am not sure kama ni Wenger peke yake! and to be honest si kama namtetea! Fergie msimu huu pia amekua mlalamishi sana, (but wanazi wa man utd hawaoni hilo) huyu mzee kila mechi anayofungwa ama kutoa draw ni kelele tu, even mechi ya juzi juzi tu waliofungwa na Villa alisema eti time management ilikua mbovu. na hivi bado anakesi ya kuwazodoa marefa!

ofcz i knew hii thread niliweka nikijua wanazi wa man utd will never accept anything, hata pale panapofuka moshi
 
Haiingii akilini Man U kununua mechi ya Wolves badala ya kununua ya Arsenal au Chelsea. Utasema hao nao wanataka ubingwa, basi angenunua ya Aston Villa ambaye ubingwa hawezi ila anatafuta nafasi nzuri tuu za juu. Wolves wasingeuza mechi kwa sababu hawatapenda kushuka daraja baada ya msimu mmoja. Kwa hiyo propaganda za Wenger hazitamfikisha mbali bora acheze mpira tuu.
 
hata 5 wanaweza kutufunga, nadhani hili ni fundisho kwa SAF na ni bahati mbaya kwamba wachezaji wengi i majeruhi.
 
duuh poleni wakuu humu ligi ngumu mwaka huu kelele za 2 horse race haziwafikishi popote hizo bado mapema sana kuanza kuaongea uchafu.
 
SAF kachemsha ... beki yake haikuwa makini, anaweza kuwa na excuse ya majeruhi. Maana hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba beki alikuwa mmoja tu (Fabio).

Pia kiungo kilipwaya sana, kiasi kwamba hakukuwa na coordination kati ya safu ya ulinzi na safu ya mashambulizi. Sijui Anderson alikuwa ni kiungo ama beki, Scholes ambaye alisababisha goli la kwanza alipwaya sana.

De Laet alizidiwa sana na hakuwa na ujanja, angalau Fabio Da Silva alipoingia kukawa na nafuu.

Pole Man U kwa kuwa jamaa walio juu ya meza kesho wanaweza kuzidi kutanua pengo la point. Majeruhi wenu wapone haraka ili mambo yawe mswano.

Kama hali ya majeruhi itaendelea kuwa kama ilivyo sasa, kuna haja ya kumshauri SAF atumie window ya January kupata beki mmoja ama wawili, vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya sana.

Kwa mwendo huu na timu kama hiyo mwezi February ukifika, AC Milan wanaweza kuchekelea ushindi/kusonga mbele hata kabla ya kuingia uwanjani.
 
Back
Top Bottom