Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Tonali anaenda spurs,scott bado haieleweki man u wanachungulia pochi, baleba amedrop man u, hawawezi kubet, yule dogo wa moroko, na ile mido madrid ndo karata ya mwisho ya utd otherwise wasahau kushindania ubingwa wa epl.
Tonali ameshaenda spurs tayari, united hawakua seriously kumchukua. Tchouamen wasahau kabisa hata huyo bouaddi nae wasahau unafikiri madrid na lile hawataki hizo Β£100m.
 
Tonali ameshaenda spurs tayari, united hawakua seriously kumchukua. Tchouamen wasahau kabisa hata huyo bouaddi nae wasahau unafikiri madrid na lile hawataki hizo Β£100m.
Wakikosa hao utd msimu ujao kilio ni kilekile
 
United naona wameandaa kiwango Fulani cha pesa kwaajili ya wachezaji Fulani, there is no way united ingetoa kiasi kile cha pesa Kwa Fernandez then mchezaji alisema timu itakayo kuwa na dau kubwa basi ndo atakwenda hiyo hiyo hapo united ndo wakakimbia kabisa maana mchezaji hajui anataka kucheza timu gani...Naona wako na Falsafa ya kuwa mchezaji utake kucheza timu yetu Kwanza halafu mambo ya pesa ndio yanafuata na sio kuweka fees kama kipaumbele, nowadays soko limeharibika Sana...
 

Kwa EPL, tuliwahitaji sana wachezaji wa pale pale katika ujenzi wa Msingi imara wa timu hasa idara ya Kiungo..

Tayari tumekosea..sijui Mpango ni upi..

Niliwaona
Tanguy Ndombele
Timeoe Bakayoko
Thomas Lema
Wakiwa Monaco, wa moto sanaa..

Mmoja akaenda Spurs
Wa pili Chelsea na
Wa mwisho Atletico..

Hawakuwahi kuwa wale wa Monaco Tena..

Benardo na Fabinho ni Exceptionals, Walienda timu ambazo zimeshakomaa, walimu Bora pia..

Hivyo, tulipaswa tusajili watu wa pale pale..

Na sasa Spurs wanamchukua na Tonali..

Wanataka kufanya nini Hawa Jamaa?
 
Mimi si mtabiliπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ila kuwakosa hao jamaa wawili tayari gari imeyumba sana..

Tumeishi misimu minne ya kuwaombea njaa Arsenal.. mwisho wa siku wamebeba ubingwaπŸ˜‚

Maumivu ni makali sana kwa kweli
 
Ukweli katika maisha, chochote kizuri huwa kina gharama zake..hakuna namna ya kupata mchezaji mzuri kwa pesa za kibahili.. haiwezekani...awe kinda ama aliye komaa,, mchezaji mzuri unampata kwa pesa nzuri..

INEOS hii itikadi Yao itawafukuzisha kazi watu wengi sanaa,,

By the way, Berrada yeye sio kama Mawaziri wakuu wa UK?πŸ˜‚ Fasta tu wao Wana achia kiti..
Miaka hiyo ya redio nimemsikia sana Tony Blair, Kisha nani nani Gordon na baadae Cameroon..baada ya hapo ni miezi tu mtu anaachia kiti
 
Kama eneo la kiungo limeonyesha uhitaji wa wazi kabisa lakini bado tunajibana kutoa hela, beki wa pembeni si ndio itatakiwa tumuombee Dalot apandishe kiwango msimu ujao!
Sina Maarifa mengi katika Soka, ila Nina amini Msingi wa timu imara na Bora yeyote unaanzia kwenye Kiungo..

Kama hapa wataleta mzaha(ambao tayari wameufanya) basi tutangoja sana..

Nimeishuudia Chelsea ya kwanza ya Jose Mourinho..(Lampard, Essien, Ballack, Obi, Makelele) wengine wamenitoka, hii timu hata ile Barcelona ya Deco, Gaucho na Eto'o wakipata shida mno..

Kuna Arsenal ya Mzee Wenger, miaka flani Alexander Song alichanganya, Fabregas, Ramsey, Wilshare, Nasri, walikuwa moto sana..

Vipi Barcelona ya Sergio, Xavi na Iniesta?πŸ˜‚πŸ˜‚umefanya tuichukie sio tu Barcelona, Bali Jimbo Zina la Catalonia..

Pep Guadiola, timu zake zote huwa anaimarisha Kiungo na ubunifu kutokea pembeni..

Sasa sisi tunaleta mzaha?
Tujipe muda tuone itakuwaje hiyo September
 
Tchouamen, huyu ni design ya wapambanaji anaowapenda kocha mzalendo The Special One..😁😁
Ataruhusu aondoke? Labda tu iwe iliamuliwa baada ya tukio la kugombana na Fede
 
Unachosema ni uKweli kabisa, mchezaji kashuka daraja akiwa na Southampton na westham. Haoneshi msima wa kuja united bado hajaitwa kombe la dunia kuichezea ureno kwanini utoe Β£85m. Hivyo kupitia kwa omar berrada ngoja tuone kama hii falsafa yao ya usajili itaisaidia united.
 
Huenda wameona wawe seriously si unakumbuka kauli za Diego conte na mourhino kuhusu uongozi wa Tottenham hasa kipindi cha levy.
 
Huenda wameona wawe seriously si unakumbuka kauli za Diego conte na mourhino kuhusu uongozi wa Tottenham hasa kipindi cha levy.
Wamenishangaza sana Spurs..

Muuzaji kugeuka kuwa mnunuzi wa Bei mbaya..
Nawatakia Kheri..

Soko limeshaharibika sasa..sijui sasa tetesi zinaelekea wapi..
 
Tchouamen, huyu ni design ya wapambanaji anaowapenda kocha mzalendo The Special One..😁😁
Ataruhusu aondoke? Labda tu iwe iliamuliwa baada ya tukio la kugombana na Fede
Huenda hii ndiyo sababu mojawapo, lakini tujiulize France akibeba world cup madrid watamuuza je vipi likitokea battle la club nyingine kubwa Manchester United wataweza kushinda na kumchukua Tchouamen hapo bado mshahara wake na kwa kauli za omar berrada sizani kama watatoa Β£100m plus so bado giza ni nene sana kwa Manchester United.
 
Mateus kaniuma ila Tonali kaniuma zaidi...
Heartbreak kama hii nilishawahi ipata kwa Demu wa Kwanza kabisa nilimpata Form 3 akaniacha niko Form 4 karibu na NECTA naona maumivu yana shabihiana kabisa kudadeq πŸ˜‚, nilikuwa nimemkasilikia Fernandes kabla sijamsamehe Tonali kaingilia kati hizi siku mbili naishi kwa Taaaaaaabu sana ndugu zangu tuombeeane uzima tu ila msimu ujao Man u bila kunituliza na kikombe chechote aisee..... watakuwa wamenyonga kabisa.
 
Hii timu itakuja kutumaliza mapema kwa shinikizo la damu.
 
Kuna fan wa utd ametoa mawazo kwamba, ikiwa Mbeumo, Sesko na Cunha wanalipwa 150k-180k kwa wiki na wamepambana hadi timu imerudi champions league itakuaje Matheus na Tonali wagekuja na kulipwa 200k- 250k?

Hii ingeleta shida dressing room kama ilivokua kwa Pogba na Sanchez! Nimejaribu kumuelewa hoja yake.
 
Pole sana Mkuu..lakini kitu kimoja Nina Imani nacho, Manchester United ipo karibu kurejea.. timu zote Zina Anza upya kujipanga
 
Naskia Kuna mchezaji wa Brazil kasajiliwa United lkn toka world cup ianze sjaona akipewa hata dkk πŸ˜†πŸ˜†
inamaana tuliesajali anauwezo mdogo had anazidiwa na babu casemiro? Au guameres

Kazi ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…