Kukulela leo kamtia Amadinho kwenye mfuko wa shati, yaani anamtambia kabisa anamwambia "huku mbele leo haupiti wewe wala mpira"
Ila huyu Ujirangi hapana haiseee, striker gani bana hajui hata kujiposition, mipira yote inamkuta yupo offside, kama vipi bora arudi nyuma akae beki halafu Maguire acheze mbele.
Huyu babu acha afilisike tu, ikiwezekana aishiwe kabisa akose hata pesa ya kununulia viatu awe anatembea peku mjinga huyu, ameleta figusu mpaka Mwarabu kanyimwa timu kwa sababu yake kenge huyu.
Wachezaji wetu banaa raha sana, yaani tayari mmeshagongwa, dakika 90 zimeisha mnaongezewa dakika 7 wenyewe wanagonga back passes tu kwa raha zao, haya inabaki dakika moja mpira uishe wenyewe sio shida zao ni mwendo uleule wa back passes, tena wanarelax kabisa kama vile wao ndio wamebeba points3
Kushabikia timu la dunia raha sana aiseee, yaani leo linakupa furaha halafu kesho linakupa presha.
Tukutane San Mamés May21 tukashuhudie fainali ya kiume kabisa kutoka kwa watoto wa Ange Postecoglou dhidi ya vijana machachari wa michuano ya Europa ambao tokea michuano imeanza mpaka wanaingia fainali hakuna timu yoyote iliyodiriki kuwafunga.
Ila aliemroga Hojlund amhurumie basi japo kidogo, mwamba anateseka kinoma katika, Kwenye kutafuta tiba kaenda mpaka Bagamoyo kaambiwa Rashidi ndie aliemroga, kapewa hirizi aivae wakati wa mechi halafu kaifunika na bandage, lakini bado gps imesoma refa akamwambia akaivue
Katika kuzuga anajitetea kua aliyovaa ni smart watch sio hirizi, sasa tokea lini smart watch inavaliwa kisha inafunikwa na bandage?
Mimi nilikua najua haya mambo ni huku kwetu Africa tu, kumbe mpaka ulaya watu wanapigana misumari.