Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

kama winga wako hajawahi kupiga hatrick EPL usipite kwenye page yetu
IMG_5026.jpeg
 
Kwa jinsi nionavyo mchezo unavyoendelea hapa wachezaji wa utd wanamentalit ya timu ndogo hivyo wanapokutana na timu kubwa kama Liverpool, Man City na Arsensl wanakamia game ila wakikutana na wadogo wenzao kama Southampton wanacheza kwenye kiwango Chao halisi na hapa ndipo unapata picha ya kikosi tulichonacho. Hii nafasi ya 14 hatupo kwa bahati mbaya bali ndio uwezo wa aina ya wachezaji tulionao. Mchezaji kama Maiono mimi sioni ubora ambao watu wanamsifia kila wakati ni back past mara apigishe wapinzani mpira. Tunahitaji wachezaji wenye kujiamini sio hawa ambao wanawasiwasi hadi miguuni.
Maino ni zigo 😄😄😄

Chezaji lina miaka 19 ila zito kukimbia km ndio linakaribia kustaafu 😄😄
 
Tunahitaji watu kweli, tujikongoje hivi hivi Hadi summer tuone tutaongeza mashine za kazi ngapi, wasiwasi wangu ni je tutaleta watu sahihi?, mambo ya kupigwa tushachoka nayo, uzuri naona kocha yupo direct.

Huyu kocha anajitahid sana tatizo ni wachezaji tu, Zirkzee Jana ndio game changer, sub ya Anthony pia ilikuwa fantastic pia. Mipira mingi aliyokuwa anapewa Zirkzee ana control vizuri(Kwa suala la control huyu jamaa nampa mkono), tofauti na rasmus control chumba na sebule.

Hapa tutafute mido moja ya kazi, namba kumi ya kazi, winga moja ya shavu la kushoto ya kazi, beki ya kati moja ya kazi, namba Tisa ya kazi, hapa tunaweza tukaanza msimu Kwa matumaini.
 
Back
Top Bottom