Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Leo nimeendelea kugundua katika hii timu kila idara imekufa. De Ligt anarudishwa nje kufutwa damu mara tatu na bado madaktari hawaoni kuna umuhimu wa kumfunga kitu kichwani.

Hahaha, kweli timu yetu imeoza!
 
Masingeli siku hizi haungalii mpira?
Hebu nitajie mechi moja tu uliyomuona Jesus akicheza baada ya kufanyiwa hili tukio la kidhalilishaji.
Last mechi mbona kacheza ,wewe ndio huangalii mechi
 
Naona mna goal difference ya 53 dah! Man u mnafunga magoli.
 
ETH uishi miaka mingi, sio kwa Raha hizi tunazopata wapinzani
Masingeli kwani Bournemouth kafanya nini, mbona matusi yamekua mengi kwenye jukwaa la Asaninyau?
Uwepo wa Masingeli kwenye hili jukwaa la Mashujaa hua ni baraka kubwa sana upande wetu, maana dua zake mbaya juu yetu hua zinabadilishwa kua neema, halafu yale mabaya anayotuombea yanahamia kwao.
Binafsi sijawahi kuchukia uwepo wake kwenye hili jukwaa, maana natambua yule anaempa uwezo na nguvu za kuingia humu lengo lake ni kumfedhehesha ikishafika mwisho wa msimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…