Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ukiondoa magoli matatu tuliyowapa wale jamaa kuna kipi cha maana sana walichokifanya kwenye hii mechi


Ila progerss ipo wadau ni suala la muda tu
Hakuna cha maana mkuu,kwenye football cha maana ni kufunga magoli tu hakuna kingine labda utuambie wewe cha maana kina weza kuwa kipi ukiondoa kufunga magoli.

Hakuna cha maana zaidi ya kufunga magoli ,ndio kinachowafanya walipwe mishahara hiyo.
 
Higi huyu ni kocha kweli?
Huyu ni dalali pia anamiliki kampuni kubwa ya udalali amemuweka mwanae kama msimamizi mkuu.
Ila li Masingeli lilikua linatusanua sana kuhusu huyu muhuni ni vile tu management imeamua kukaza shingo.
Nina imani Baba Ubaya Christmas hii itamkutia kwao.
Sema mwamba nae ana mikwara si ya kitoto, bwanyenye Jim Ractliff alikua ameshapanga kabisa kumkula kichwa ila huu mkwara wake ndio uliofanya akabakia United.
'If they don't want me anymore, I go anywhere else to win trophies'
 
Hii timu mimi nazitupa lawama kwa fergie moja kwa moja.....
Babu hakutaka mabadiliko ya kiuchezaji kwenye soka lake means hata mfumo wa soka la kisasa hakuutengeneza
Babu alituachia timu mbovu ambayo isingeweza kumaintain kwenye ubora hata miaka miwili mbele na hili tumeliona
Babu aliacha structure mbovu mno ya kiuchezaji ambayo mpaka leo makocha wanahaha kuiondoa klabuni na kuleta structure ya soka la kisasa

Mateso yote haya chanzo ni fergie tu lawama nazitupa kwake kwa asilimia mia...........wenga kaacha msingi mzuri mno wa kiuchezaji kiasi kwamba makocha waliokuja hawajateseka sana kimfumo wao waliamua kusajili wachezaji wanaoendana na mfumo walioukuta ingawa kubeba makombe kwao ni mtihani......klopp anasepa liverpool ameiacha timu ikiwa na stucture yake ya kiuchezaji kocha mpya hapati tabu kutembelea huu mfumo alioukuta na hata pep akisepa akija kocha hatopata tabu kabisaaaaa...

Fergie aliiacha united ikiwa na mfumo wa pasi tatu goli hakutaka kabisa kubadilika kiuchezaji wakati mwenzie wenger tayari alishaachana na huo mfumo na kuijenga aseno hii ya kisasa kiuchezaji waliomuita profesa hawakukosea............

Timing nzuri ya kubadilika kiuchezaji fergie alipaswa aianze pale tu alipotetemeshwa wembley na barcelona leo hii makocha wapya wasingeteseka hivi kutengeneza structure ya kiuchezaji na wala tusingebadilisha makocha hovyo hivi kama nguo
 
Ni miaka mingapi tokea babu aondoke?
 
Inabidi twende na 4_3_3, jana imetuonesha ni namna gani nyuma ya middfield tunakuwa outnumbered.

Ila all in all fukuza ten hag, miaka 3 hakuna hata style of play.

Rashford aanzie bench.



Dogo yoro akirudi tujaribi pia na 3 5 2
 

Attachments

  • ReactNative-snapshot-image7986741661338084005.png
    1.2 MB · Views: 14
Tuwe honest nature ya united si 433, they cant play hiyo formation. Unite imekuwa heavily rely ilon 442 miaka mingi, why wana force formation ambazo si productive
 
Tuwe honest nature ya united si 433, they cant play hiyo formation. Unite imekuwa heavily rely ilon 442 miaka mingi, why wana force formation ambazo si productive
Sasa 442 kwa modern football utapotea, 4231 ndio hii tunakuwa dominated behind the midfield
 
Lawama za kindezi kabisa kwa Sir Alex Ferguson, kwani Liverkuku hakuwa na philosophy la counter attack football enzi za akina Gerrard, mbona wamebadili mfumo na sasa wako vizuri tu?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Katika kitu ambacho najuta duniani ni kushabikia timu bovu kama Manchester united tena najuta Sanaa sababu nililipenda kutokana na Broo alikua analipenda na nilikua naenda nae kibandaumizakipindi kile mzee Ferguson anatafuna big g mbele ya messi Sasa Hilo timu baada ya mzee Ferguson kuondoka limeonekana halina mpango mpaka Jana tulivyochezea kichapo na Liverpool nimehama rasmi Mimi ni shabiki wa Liverpool kilichonifanya niipende ni siku ya Jana nimeshuhudia timu langu la zamani bovu likipigiwa mpira na kudharirika tukiwa nyumbani rasmi Mimi nashabikia Liverpool najiandaa kwenda kuchukua jezi zangu zote 3 za Liverpool najua wengi mtaongea ila msinipangie maisha Manchester united imeshajifia na haitofufuka kwenye ulimwengu wa hii dunia
 
Utafukuza makocha wangapi na kumbuka kila kocha anakuja na style of play yake.....kitendo cha fergie kutoswitch kutoka kwenye 442 yake na kucheza hii mifumo mnayotaka ikasaidia hata kwa hawa warithi wake ndio chanzo cha mateso yote haya
Moyes kaja na style of play yake
Vaan gaal kaja na style of play yake
Carrick na giggs care takers wamekuja na style of play yao
Mou kaja na style of play yake
Sosha nae kaja na style of play yake
Na huyu wa sasa kaja na style of play yake

Halafu unategemea tutatoboa sahau kwa kweli

Hiyo list hapo juu ni makocha wawili tu wanaopaswa kuvumiliwa sana ili kuendana na style of play ya kisasa vaan gaal ten hag mmoja tushatimua na huyu mmoja fans wa simba na yanga mnataka aondoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…