Ukiiangalia timu yetu jina la mchezaji mmoja mmoja kama shabiki unajua tuna timu mbovu. Bahati mbaya sana tumekaa na hawa wachezaji si chini ya misimu 3 hadi 5 lakini hawabadiliki kiuchezaji, hawafuati mbinu za walimu na hawana ubora katika maeneo yote uwanjani. Lakini ukipata taarifa ndio wachezaji tunaotegemea kuwaona tena msimu ujao kama backbone ya timu, unaanza kukata tamaa kabla hata ratiba ya mechi ya msimu ujao haijatoka.