Manchester United (Red Devils) | Special Thread

kwa niaba ya wana blues tunapenda sana kuwashukuru manyumbu kwa kuweza kutusaidia kupunguza kizingiti cha sisi kucheza michuano ya ulaya msimu ujao kwa kuichapa vilivyo club kongwe kabisa uingereza hongera sana ndugu zetu kwa sasa tunawaomba muwaambie na newcastle club kongwe kabisa watuchapie Tottenham yani wasikubali kufa pekeao sisi kama blue kazi yetu ni kushinda mechi zetu tu. nafasi za kupanda chat mnatupa nyie wakubwa zetu πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Siyo hivyo, bali ameshirikiana naye sana na anamjua vizuri kuliko makocha wengi. Hivyo anaelewa kuliko wote kwa nini Kipara hapaswi kupewa upenyo hata mdogo kiasi gani katika mapambano ya ubingwa.

Arsenal msipo chukua kombe nitawashangaa sana. Misimu miwili mpo on fire lakini mnatoka bila hata kombe la chai?

Mnaotofauti gani na Chelsea ambaye hayupo kwenye form?

Na Chelsea anaweza kupona akabeba kombe hata kabla yenu mlioko kwenye form
 
UTD imefeli kwa sababu ya kutojua ni Muda gani sahihi wa kufanya Dili zake na wachezaji kuhusu Mikataba na Ishu ya Sajili Pia.

Herrera, Mata, De Gea, Pogba, Lingard, Matic, CR7, Zlatan, Cavani, Varane, Martial,
Hakuna hata Mchezaji Mmoja UTD imepata hata senti kwenye kuondoka kwao. Wote wameondoka kama FREE AGENTS.

Bruno ni Mzuri sana lakini huwezi tengeneza timu kumzunguka Ligi ikianza anaingia Miaka 30, Shaw anafika 29, Rashy 27 na hamna namna unaweza tengeneza timu kumzunguka hana Mentality ya Kuibeba timu.

BRUNO, SHAW, RASHY ni Muda sahihi wa Kuwauza kipindi hiki wanauzika.
 
Huo ndio ukatili wa mpira wa miguu πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„. Ila yote maisha tu.
 
@MZANZIBAR
 
Bruno na Rashy hawapaswi kuuzwa. Kitu bora itakuwa kusajili wachezaji bora kwenye hayo maeneo.

Hao ni wachezaji wazuri kuongeza ubora wa kikosi. Ukiwauza hao maana yake unaanza upya kutafuta wachezaji 4 na bado kikosi kizima kinahitaji maboresho.
Zikipatikana Ofa Nzuri sidhani kama kuna Haja ya kuendelea kubaki nao. Umri sio Rafiki kwao na Rashy haonyeshi Dalili zozote za Kukua.

Msimu Ukianza Bruno anakuwa amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake, Yupo kwenye Gbp 240k Weekly, Rashy 375k, Shaw 200k. Hawa ukifanya Mazungumzo ya Mkataba Mpya Inabidi Uongeze Dau kitu ambacho kinaathiri Mazungumzo ya Mikataba na Wachezaji wengine huko Mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…