Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mimi naona jamaa ni mtaka matokeo na mara nyingi anafanikiwa kuyapata. Jamaa alikuwa bingwa na Ajax, au siyo? Jamaa last season aliipandisha man utd mdogo mdogo kimasihara mpaka nafasi ya 3. Kwa sasa anaonekana anaelekea kuikosa top 4 kwa sababu ligi imekuwa ngumu kwake ama ligi iko vile vile ila yeye na ugeni wake kutoka Ajax msimu wa kwanza kuna timu zilikuwa bado hazijamjulia na zikakosa matokeo kwake.

United waendelee tu kumuamini. Nadhani msimu ujao ndiyo atakuwa katika kiwango bora. Akishindwa hivyo sisi tutaendelea kufurahi kwa kupata matokeo kwake.
 
Manjesta hapa kocha mlipata


Most shots conceded in the Premier League this season:

◎ 456 - West Ham
◎ 447 - Sheffield United
◉ 444 - Manchester United
◎ 440 - Luton
◎ 410 - Burnley
 
Mikel hadi anafika msimu wa 2 tayari alishakuwa anajulikana anacheza mfumo gani na anataka nini

Mikel Arteta hadi kufika msimu wa 2 round ya 2 tayari timu ilikuwa ina control mechi vzr tu ,hapa chini ni mechi 13 za round ya 2 ,amefungwa na mancity na Liverpool tu ,Tena hizo mechi zote 2 alienda nao toe to toe
Hivi Khamisi kwa nini huwa unapenda Kuongopa!?
Arteta Yupi alikwenda "Toe to Toe" na Pep? Imemchukua Arteta Misimu 5 kupata Matokeo Mbele ya Pep katika EPL mechi takribani 8 kafungwa zote hana hata Suluhu.

Mechi Arteta anamfunga Pep hakuna hata Mchezaji Mmoja aliyeanza wakati anacheza Mechi ya kwanza na kufungwa 3-0 nje ya SAKA. ETH ana mapungufu ila Msimu wa kwanza tu alipata Matokeo kwa Hao "Giants" wawili wa Ligi kwa kipindi hiki.

Mechi hii ni Msimu wa 3 wa Arteta anacheza na "BACK 5" Mechi nzima ana Shambulizi 1 na hana ON-TARGET hata Moja! Wewe na Castr mlishakataaga mwalimu wenu hajawahi tumia Mabeki 5, sasa hapa alitumia wangapi?

Hoja yako kwamba wewe Ulisema ETH sio Mwalimu, Itazame Ajax tangu ameiacha hali yake na imeshaweka walimu wangapi, Hawezi kuwa Daraja la PEP ama Klopp, ila kwa Muundo sahihi toka Juu anaweza badili kitu UTD {Mpaka sas UTD ina wachezaji wa Tangu Fergiee} Arteta ameshasajili wachezaji zaidi ya 25.

UTD ilipofika Matatizo ni mengi sana kuanzia Juu. De Zerbi, TT, Poch ulikuwa unawajaza sifa wote humu ila Mpira uwanjani unasema tofauti. Tuna shida ya Kufunga tangu OGS, Tizama GD hapo msimu umeisha bado ilikuwa ni 0!
 
Nadhani hamis anachosema ni Arteta alisajiliwa 20 Dec 2019, hivyo huu ni msimu wake wa 5 (19-20, 20-21, 21-22, 22-23, 23-24). Mimi napenda kusema ni msimu wa 4 kwa sababu wa kwanza alikuja December na huu bado haujaisha 😀.

Hayo matokeo ya hapo nakumbuka ndiyo wakati Arsenal fans karibia wote kwenye jukwaa letu tulikuwa tunataka Arteta aachishwe kazi ila nadhani Hamis peke yake ndiye alikuwa anamtetea. Tulikuwa tumeanza kujipata licha ya matokeo mabovu mfululizo. Tulikufa 2-0 kwa Brentford, 2-0 kwa Chelsea, 5-0 kwa City.

Tukawa chini kabisa hatuna point, hatuna goli, tumeshapigwa 9. Ila tulianza kunyanyuka na mwishowe tuliboronga tukaingia Europa. Kabla ya hapo tulimaliza wa 8 mara mbili, yaani ule nusu msimu, na msimu mzima wa kwanza wa Mikel. Baada ya hapo kuna mechi angalau moja ambayo tumempiga City msako (Hamis alikuwa anauita huu msako 'utatoa hotoi'), Partey alitawala dimba, ila tulipoteza mechi dakika za mwisho kabisa.

Tulizingua tukafungwa nyingine ila hapo tulikuwa tumeanza kukataa kuwa wateja kwa City. Kwamba tutawachezea mtindo wetu hata tukifungwa. Nadhani hii ndiyo 'toe to toe' anayoongelea Hamis na kweli tumeanza kuona mwanga baada ya muda mrefu. Shida hii tumeipata kwa United kiasi fulani, Liverpool na hata Chelsea na Tottenham ambao walitunyang'anya ufalme wa London kwa muda ila tumepambana kurejesha utawala wetu na tukikaa vizuri tutaumiliki mazima tena.

Arteta alipewa kazi ya kurejesha Arsenal katika kupambania ubingwa. So far ameweza kufika hapo. Sasa kazi yake ni kushinda mataji. Mtihani huu bado hatujui kama atauweza ila ameonyesha kuwa anauwezo huo.

Tukija kwa Ten Hag, kweli amepata matokeo na giants na msimu wa kwanza alishika nafasi ya 3. Hamis huwa anasema pamoja na kupata matokeo, aliita style ya Ten Hag 'pira janja janja' ambao hauwezi kuwasaidia mara nyingi na kwamba anavyoendelea nao, matokeo yatazidi kuwa mabaya kwake kadri ligi inavyomzoea.

Ukiangalia mwenendo wenu wa sasa, maneno ya Hamis yanaonekana kutimia.

Binafsi naamini baba ubaya ni bonge la kocha ila kuna vijimambo vidogo vidogo vikiclick ataleta usumumbufu mkubwa sana.
 
Umetumia muda gani kujificha na kupata data 😅😅😅

Am joking.

Ngoja nikuulize kitu.

City ya sasa inacheza na mabeki 5?

Kama hoja ya Ajax kua mbovu baada ya Erik kuondoka na unaitumia kuhalalisha kusema Erik ni kocha ndiyo tuseme Lampard ni kocha mzuri? Gerrard ni kocha mzuri?

Matatizo ya Ajax ni zaidi ya kocha. Kaangalie wachezaji wake first XI wangapi hawapo. Also jitahidi kuangalia ugumu wa ligi.
Pochettino was above average France ila EPL?

And yes nasema Arteta hajawahi kuchezesha mabeki 5.
 
Huyo jamaa muache abwabwaje ,

Hao ni fans wanaotembea na matokeo tu basi wanaamini kazi imeisha


Arteta msimu wake wa pili ,tayari alikuwa na playing style inayoeleweka

Round ya 2 naweka mechi hapa alikuwa tayari anatumia 4-3-3 ,na alipocheza vs Liverpool na Mancity alifungwa ndio

Lakin ni mechi ambazo hakukaa nyuma alibishana nao ,Moja wapo ile mancity pale Emirates anapelekewa moto ,Refa anakuja kutoa Red card

Vs Liverpool, Arsenal alifungwa 2-0 lakini alienda toe to toe na Liverpool .


Baada ya hizo mechi ,nikasema msimu ujao tunagombea ubingwa ,wanaokumbuka wanakumbuka vzr sana,na kweli ndio kilichotokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…