SuchNoble
Member
- Apr 13, 2014
- 13
- 11
Nafikiri kwa msafiri yoyote anayesafiri kwa kutumia either mabasi ya abiria au usafiri binafsi atakubaliana na mimi kuwa vyakula katika hoteli za njiani (stop overs) vinauzwa at a very premium prices.
Sasa hoja yangu sio bei ya kuuzwa kwa vyakula hivyo, hoja yangu kubwa ni je, Serikali inapata inachostahili kupata katika bei hizo ambazo raia wake tunaziingia?
Jana nilikuwa natoka Arusha naenda Dar es Salaam nikasimama kituo kimoja cha chakula hapo katikati ya Korogwe na Segera, baada ya kuhudumiwa kama kawaida huwa napenda kudai risiti kwasababu mimi ni mdau mzuri wa kulipa kodi. Nafurahia kuona pia wenzangu wanalipa kodi zao kwa maendeleo ya nchi.
Kilichonishangaza ni kuwa mtoa risiti alitafutwa zaidi ya dakika kumi kana kwamba nihairishe kudai risiti ili basi lisiniache, kwa bahati nzuri nilikuwa na private kwahiyo nilimsubiri hadi alipoamua kutoka alipojificha, na kwa muda wote niliokuwa nimesimama hapo watu walikuwa wakihudumiwa na kuondoka.
Sasa kwa mstakabali huu najiuliza, zile nguvu kazi zilizowekwa kwenye maduka na masoko kwanini zisisambae kwenye barabara hizi watu walipe kodi? Kwasababu ukweli ni kwamba, nchi inapoteza bilions of money monthly kwa uzembe huu kwakuwa sio kila msafiri ana uelewa wa kudai risiti.
Mwisho nitoe wito kwa wafanyabiashara, tutoe risiti hata kama tunaibiwa na wanasiasa, sisi tutimize wajibu wetu ili utakapofika muda wa kuwawajibisha tuwawajibishe kwa usahihi.