DOKEZO Udhaifu katika Mamlaka ya Mapato (TRA) Songwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
UDHAIFU KATIKA MAMALAKA YA MAPATO YA TRA SONGWE

kumekuwa na utendaji KAZI m'bovu wa mamalaka ya ukusanyaji mapato ya TRA songwe Kwa kudai Kodi zaidi ya makadirio yaliyofanywa Kwa mteja.

Ni zaidi ya miaka mitatu ya makadirio ya mapato Hali hii inajitokeza Kwa upande wangu

Mfano hai ni hili lililonitokea Mimi binafsi

Tarehe 16/09/2022 majira ya asubuhi nilifika katika ofisi za TRA mkoa wa songwe Kwa lengo la kujua deni langu lililobaki na ninalodaiwa ili niweze kulipa. Kwa bahati njema Mimi ni mlipaji mzuri wa Kodi Kwa serikali. Baada ya kuniomba TIN NUMBER yangu mfumo ukaonyesha natakiwa kulipa deni la muhula wa mwisho yaani September - December 2022. Papo hapo wakanitengenezea namba ya ankara (control number) nikalipa. Wakanitolea TAX CLEARANCE ya September - December kuwa sidaiwi. Hivyo nitapaswa kulipa Kodi tena baada ya makadirio mapya ya mwaka utakaoanza wa 2023.

Kwa masikitiko makubwa Leo tarehe 21/09/2022 asubuhi nimepigiwa simu kutoka ofisi ya TRA mkoa huo (songwe) kuwa nadaiwa Kodi ya muhula wa mwisho yaani September - December 2022.

Kiukweli imenisikitisha Sana na kunifadhaisha. Hivi hizi ndizo mamlaka tunazozipa Imani kwaajili ya shughuli zetu zinazo tukandamiza na madeni ya Kodi tusiyostahili?

Au shida ni mifumo Yao ya Kodi. Kama ni mifumo, imewezaje kujua deni langu lililobaki hapo kabla ikanitaka nilipe na nikalipa na TAX CLEARANCE ikatengenezwa lakini bado inaonyesha kuna deni?

Halafu unapigiwa simu kuwa ufike ofisini. Mimi nilishatekeleza wajibu wangu wa kujua deni langu na nikalipa. Hili suala la kudai Kodi ni wajibu wa Nani? Au KAZI ya afisa mkusanyaji Kodi ni kukaa Tu ofisini? TRA hebu tupeane thamani tusipelekeshane Kwa namna hii. Tutarudi Zama za umachinga sasa.

Nimeandika.
 
Nadhani ingekuwa vizuri kama ingekuwa vizuri Muine Meneja hapo tra Songwe najua atakusaidia sana mimi alishawahi nisaidia na nikalipa kodi yangu.
 
Back
Top Bottom