Mamlaka ya Hali ya Hewa yasema kipindi cha Novemba 2023 hadi Januari, 2024 kinatarajiwa kuwa na mvua nyingi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
mvua.JPG
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi mwelekeo wa mvua za Msimu kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka ambayo ni mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Ruvuma na Kusini mwa Morogoro.
Mvua tena.JPG

IMG-20231031-WA0040.jpg
Taarifa hiyo imesema kipindi cha nusu ya msimu (Novemba 2023 hadi Januari, 2024) kinatarajiwa kuwa na mvua nyingi ukilinganisha na nusu ya pili (Februari hadi Aprili 2024), uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za Msimu.

“Mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo ya Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, mikoa ya Iringa, Lindi, Mtwara, Singida, Dodoma, kaskazini mwa mkoa wa Katavi, Kigoma na Tabora.

Aidha, mvua za Wastani hadi Juu ya Wastani zinatarajiwa Kusini mwa Mkoa wa Katavi, mikoa ya Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma”.

Dkt. Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu TMA na Makamu Mwenyekiti Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC) amesema athari zinazoweza kujitokeza ni vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo, vilevile, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka.

Pia, Dkt. Chang’a ametoa ushauri kwa wadau mbalimbali kuzingatia matumizi endelevu ya uhifadhi wa rasimali maji.

Dkt. Chang’a amefafanua kuwa Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2023 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba) utabiri wake ulitolewa tarehe 24 Agosti, 2023.

Mvua hizo zimeshaanza katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani ya Kaskazini na baadhi ya maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki kama ilivyotabiriwa.

Ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba, 2023. Vilevile, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika mwezi Januari na Februari, 2024.
 
Hawa nao ni kama wano bet sportspesa tu. Walianza na mikwara ya mvua nyingi toka Oktoba, utabiri ukabuma.

Waufyate tu, mvua zikianza tutaziona na kama kawaida yao wadandie treni kwa mbele pale mvua za kweli zikinyesha waendeleze utabiri wao wa kunjunga.

Ukute jitu limekaa bar lishaelewa kisungura likiona mawingu linatweet kuwa kutakuwa na mvua kubwa.
 
jamaa wametuingiza mkenge walah.

bora wapige kimya mana naona kama wanazidi kuchemsha
 
Wana lipwa mshahara wa bure kabisa.

yaani imefika hatua tabiri zao zina puuuzwa. hata wakisema watu wahame mabondeni..hakuna anaye hama..

Mamlaka iwezeshwe... waache tabiri za kina Yahya
 
Hawa nao ni kama wano bet sportspesa tu. Walianza na mikwara ya mvua nyingi toka Oktoba, utabiri ukabuma.

Waufyate tu, mvua zikianza tutaziona na kama kawaida yao wadandie treni kwa mbele pale mvua za kweli zikinyesha waendeleze utabiri wao wa kunjunga.

Ukute jitu limekaa bar lishaelewa kisungura likiona mawingu linatweet kuwa kutakuwa na mvua kubwa.
Mvua zikiwa ndogo. Watadandia treni kwa mbele wataamka na utabiri "mvua za mwaka huu ni chache wananchi wapande mazao himilivu"
 
Huo utabiri wenu wa kisomi endeleeni kuutoa sisi wengine tuna utabiri wetu wa asili usiokosea. Tukisema mwaka huu utakuwa na mvua nyingi hatukosei kwa kuwa kuna viashiria vya hali ya hewa kwa ujumla tuna sense kwa kutumia miili yetu na kuangalia hali ya anga ikoje kwa siku nzima au mwezi mzima. Tunajua mawingu ya mvua ni yapi na upepo unavumaje. Tunaangalia jua na mwezi vinaonekanaje kuhusu kuwepo kwa mvua. Tunajua majira ya mvua rasmi ni miezi ipi. Huu utabiri wa kisomi ni nyongeza tu wala hatuufuati ni wa kubahatisha na unatuchanganya
 
Mvua zikiwa ndogo. Watadandia treni kwa mbele wataamka na utabiri "mvua za mwaka huu ni chache wananchi wapande mazao himilivu"
ndio zao. wasanii tu. wanasoma alama za nyakati kwanza ndio wanakuja na tabiri zao za kipumbavu.

Safari hii mvua zimewaumbua, zinabipu kidogo halafu zinasepa huku wenyewe washadandia mchuma kwa mbele na maonyo mengi kwa wanaokaa mabondeni.
 
UTABIRI = PROBABILITY

Acha inyeshe tuone panapovuja, ila hawa nao mamlaka wanakuwaga na mikwara sometimes unaweza usiende kwenye mishe zako ukiogopa mvua kubwa
 
  • Thanks
Reactions: apk
Mikwala mingi Sana. Wanatufanya ss wajinga
Juzi kati hapa walitabiri kutakuwa na mvua kubwa aisee, ilifika saa 5 asubuhi jua kali lilinipiga nikajisemea hawa mamlaka wametupanga bure hamna cha mvua wala nini!
 
Hawa watu siyo wa kuaminiwa, wakulima mpaka sasa tumeshapata hasara ya kufungia mwaka
 
Back
Top Bottom