Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam

Hawa wafanyakazi hawakupaswa kupewa jukumu la kuchagua TPA au DP World. Nionavyo mimi ilitakiwa TPA kukabidhi wafanya kazi wote waliokuwa chini ya TPA kwa DP world, Muundo wa TPA uvunjwe na ubaki uongozi wa TPA kusimamia tu uendeshaji wa DP world na kuhakikisha hawa DP World hawatanyanyasa wafanyakazi na kuhakikisha malipo yao yanafuata makubaliano ya mkataba, na kuhakikisha mkataba wenyewe unaenda kama ulivyopangwa.

Sasa TPA inabaki kufanya nini ilkiwa DP World anapewa Bandari ya Dar es Salaam na zingine na za maziwa yote, kama sikukosea mkataba ulikuwa unasemaje.

TPA iji disolve yenyewe, wafanyakazi wote waende kule DP World kwa mama Kizimkazi.
sio rahisi kwa ule mkataba mmh
 
Mm ni mmojawapo ninaeona bora watu weupe waendeshe bandari. Nna mzigo tokea January 7 2024 mpk leo March mwishoni hailujafika. Kwa haraka haraka mzigo wangu una siku 80 haujapakuliwa bandarini. Sasa si ushenzi huu.
 
Watasamnazwa bandari zingine kama Tanga,Mtwara,Mbambay na nyinginezo.
Kwani hizo DP World kazikataa? Mkataba ulisema ataendesha bandari zote za bahari kuu, na za maziwa yote. Au walibadirisha baadaye?
 
Hebu tueleze mkuu upogaji wa TPA ni upi!?
Mtu anayehusika na kuchukua kodi ni TRA hao TPA wanapiga madili gani!?
Au ndio hearsay
Watu wana amini TPA kila kitengo unapiga pesa. TPA inatoa huduma ya kushusha mizigo wao wanakusanya Port charges,handling charges na wharfage.

Anayekusanya ushuru ni TRA, uwezi kutoka kwenye geti la bandari bila kulipa kodi hata ukiwa umelipa gharama zote za bandari
 
Mm ni mmojawapo ninaeona bora watu weupe waendeshe bandari. Nna mzigo tokea January 7 2024 mpk leo March mwishoni hailujafika. Kwa haraka haraka mzigo wangu una siku 80 haujapakuliwa bandarini. Sasa si ushenzi huu.
Mkuu mzigo umeshuka, hapo itakuwa changamoto ni kuutoa. Clearing Agent wako alipata documents na akaanza mchakato mapema wa kuutoa.

Pia mzigo wako inawezekana agent kakamilisha baadhi ya hatua, ila alicho declare upande wa TRA na uhalisia wa mzigo ni tofauti hapo inabidi mkono uwe mwepesi au kama ni vitu vinahitaji ukaguzi wa TBS au TFDA kuna sehemu hapako sawa. Siku 80 hasara kubwa sana, hapo mzigo wako utatakiwa ulipe storage charges ya siku 70+, sheria ya mzigo wa ndani kukaa ni siku 7 baada ya hapo unalipa kila siku
 

UFAFANUZI KUHUSU HALI YA AJIRA ZA WATUMISHI KAΤΙΚΑ BANDARI YA DAR ES SALAAM
Ijumaa 22 Machi, 2024 DAR ES SALAAM

Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilitoa taarifa kwa Watumishi wake kuhusiana na mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Gati namba sifuri (RoRo) hadi Gati namba saba.

Mabadiliko hayo yanatokana na Mkataba kati ya TPA na Kampuni ya DP World ya Dubai kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa Gati namba 0-7 za Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka thelathini (30) kuanzia tarehe 22 Oktoba 2023.

Kutokana na mabadiliko hayo katika usimamizi na uendeshaji wa maeneo tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam walitakiwa kuchagua ama kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na DP World papo hapo.

Menejimenti ya TPA ilitoa taarifa hiyo kwa Watumishi baada ya kukamilisha pro- gramu maalum ya kuwaelimisha na kutoa ufafanuzi wa kina na taarifa sahihi kuhusiana na mabadiliko tajwa kwa Watumishi wake.

Katika taarifa ya Menejimenti, Watumishi watakaoridhia kujiunga na DPW kwa hiyari walielekezwa kuwasilisha taarifa zao (Notice) katika Ofisi zilizopo ghorofa ya 32 katika Jengo la Makao Makuu ya TPA (One Stop Centre) kabla au ifikapo tarehe 29 Machi, 2024. Aidha, Watumishi ambao hawatapenda kujiunga na DP World watabaki TPA kwa kuwa Mamlaka itaendelea kuhitaji Watumishi watakaotoa huduma katika Bandari zake zinazoendelea kuboreshwa katika maeneo mbalimbali Nchini.

Kwa kuzingatia ufafanuzi hapo juu, Menejimenti ya TPA inapenda kuujulisha Umma kwamba, taarifa inayosambaa ilitolewa kwa ajili ya Watumishi na TPA ilifanya hivyo ili kukamilisha taratibu za kuhamisha huduma kwa DP World.

TPA inauhakikishia Umma kwamba, itaendelea kuwathamini Watumishi wake ambao ni rasilimali muhimu zaidi katika Mamlaka na katika utekelezaji wa zoezi hili, maslahi ya pande zote husika yatazingatiwa kikamilifu kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Masoko na Uhusiano,
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (ΤΡΑ)

Pia soma:
- DP World wadaiwa kuanza mchakato wa kuajiri, Wafanyakazi wa TPA wadaiwa kutakiwa kuchagua kwenda DWP au kubaki TPA
Serikali na baadhi ya wananchi bendera fuata upepo walipuuza sana hoja za wakili Mwabukusi kuhusu haya yanayotokea mpaka watakiri hadharani kwamba kuna kosa kubwa sana serikali ilifanya kuhusu mktaba wa DPW kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla watageuka manamba ndani ya nchi yao.
 
Back
Top Bottom