Mamlaka naomba iunde kikosi maalumu kichunguze tukio la kupotea kwa Askari Emmanuelle Govella

'Labda atakua ameenda kutembelea ndugu na jamaa....'.majibu ya askari wapenda haki walipopotea kipindi Cha magu..
Wanaweza sema "kajiteka" au kamtembelea mpenzi wake.

Huwa hawakosi majibu ya papo kwa hapo
 
Uliulizwa ulikuwepo ndani wakati wa upekuzi ukawa unakosa jibu alafu sasa unaeleza pochi ilikuwa na pesa mingi umeshuhudia au hadithi umepewa? Mimi nipo 4 ways hapa nakuja maeneo ya chama tukutane njiani unipe abc coz utasaidia Polisi bro nitakusindikiza
Anajiongezaje anaacha wallet inapesa nyingi pamoja na kadi ya benki mpaka vitambulisho vya bima ya Afya? Sizani
 
Anajiongezaje anaacha wallet inapesa nyingi pamoja na kadi ya benki mpaka vitambulisho vya bima ya Afya? Sizani!! Pia siku walipokuja kutoa vitu vyake ndugu zake walidai kukuta mpaka vyeti vyake vyote vya shule.
Ukiamua kufanya na system hakikisha unafuata vigezo na masharti. Tofauti na hapo utapotezwa na hakuna hata mfupa wako utakaoonekana.
 
Watu wanapotea kila siku,huo mji wa serikali umejaa mashushushu kibao,Kama huyu Askali alikuwa anafanya ujasusi kwa niaba ya nchi nyingine,ndio imetoka hiyo,
 
Ukiamua kufanya na system hakikisha unafuata vigezo na masharti. Tofauti na hapo utapotezwa na hakuna hata mfupa wako utakaoonekana.
Usitutoe kwenye njia hakuna system inayofanya kazi kienyeji kwa kiwango hicho mkuu.
 
Nani kaniuliza?
 
Usitutoe kwenye njia hakuna system inayofanya kazi kienyeji kwa kiwango hicho mkuu.
Unajitoa mwenyewe, unadhani Askari officer WA nyota mbili anawezaje kupotea kienyeji hivo, zingatia maelezo hapo juu alikuwa mkuu wa Kituo fulani,alikuwa hapendelei kuvaa uniform akienda kazini badala yake alikuwa akibeba begi jeusi mgongoni, jiulize Kwa nini alikuwa anaficha identity? Defenitly was an agent undercover, jiulize Askari wa level officer commanding station anawezaje kupotea polisi wasitoe tamko mpaka ndg zake ndo wamtafute? Anzia hapo kujiuliza kama alivuruga mission huyo ndo umsahau, formula ni moja tu kwamba if the law doesn't work, Eliminate.
 
Kama mpka polisi wanapotea mimi ni nani nisipotee
hapana hapo kuna kimchezo kimechezeka inavyoonekana.
vinginevyo askari wenzake wangepiga makelele nchi nzima tungejua.
Ukiona wapo kimya ujue wanajua aliko.
Ukiwa mkuu wa kituo ni mtihani sana hasa pale unapotaka kutenda haki,kuna polisi wa chini yako ambao ni wakongwe wa madili wanakuangalia wewe,kuna wakuu wa polisi wilaya wanakuangalia wewe

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Nafkiri mimi na wewe wote hatujui ZAIDI ya kubashiri ndiyo maana nikaomba mamlaka zifanye uchunguzi tupate ripoti ya kweli.
 
Huwa wanapotezwa milele au kuna muda ukifika wanaachiwa?

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…